Posts

Showing posts from January, 2023

Dk. Mwinyi ahimiza uzalishaji, ulaji mbogamboga, matunda

Image
RAIS wa Zanzibar na Mweyekti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ame sema kuna haja ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga mboga na matunda ili kukidhi mahitaji ya soko la mazao hayo nchini. Ameeleza hayo jana wakati akizindua kituo cha taarifa na maarifa ya kilimo cha mazao hayo (Horticulture) kilichopo Mpendae Kwa Binti Hamran, wilaya ya Mjini Unguja akisema Zanzibar inahitaji tani 276,000 kwa mwaka ili kukidhi mahitaji kwa wananchi wake. Alisema takwimu zinaonesha kuwa kila mzanzibari anahitaji kilo 146 za mazao hayo kwa mwaka na kwamba uwepo wa  hoteli za kitalii, inakadiriwa  wastani wa tani 2,000 zinatumika kwa mwaka katika eneo hilo. Dk. Mwinyi akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo cha maarifa ya kilimo cha hortculture Aliongeza kuwa kiwango hicho kina thamani ya shilingi bilioni 1.6 kwa wastani wa bei za mwaka 2022 ambapo kutokana na kasi ya ukuaji wa watu ya asilimia 3.7 kwa mwaka na hivyo kufikia watu milioni 2.1 mwaka 2026 ambapo uhitaji huo utaongezeka