Posts

Showing posts from February, 2021
Image
Taifa limepoteza kiongozi jasiri, mzalendo – Dk. Mwinyi NA MWANDISHI WETU MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amefariki dunia. Akitangaza kifo cha mwanasiasa huyo aliezaliwa Oktoba 22, 1943, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, alieleza kuwa Maalim Seif amefariki dunia jana katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. “Majira ya saa 5:26 asubuhi, makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad. Maalim amefariki wakati akiendelea na matibabu katika hospitali ya muhimbili alipokuwa amelazwa tokea tarehe 9 mwezi huu,” alieleza Dk. Mwinyi katika taarifa yake kupitia televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC). Aidha Dk. Mwinyi alitoa pole kwa familia ya marehemu, viongozi na wanachama wa chama cha ACT Wazalendo, wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla akiwataka kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu. Maalim seif ambae hadi mauuti yanamkuta alikuwa mwenyekiti wa chama cha
Image
  Mohammed Seif Khatib azikwa, Dk. Mwinyi aongoza maelfu ya wananchi NA R AJAB MKASABA, IKULU ZANZIBAR RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi jana aliwaongoza ndugu, jamaa, marafiki na wananchi katika mazishi ya Dk. Mohamed Seif Khatib yaliyofanyika Umbuji, wilaya ya Kati. Akisoma wasifu wa marehemu Dk. Mohamed Seif Khatib huko Umbuji, Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Khamis Abdalla Said alisema alizaliwa Januari 10 mwaka 1951 huko Umbuji, Mkoa wa Kusini Unguja. Alisema Dk. Khatib ambaye kifo chake kilichotokea juzi katika Hospitali ya Al-rahma   baada ya kuugua kwa muda mfupi, ameoa na kubahatika kuwa na watoto sita. Alisema alijiendeleza sana kielimu na   kutunukiwa shahada mbali mbali ikiwemo shahada ya Ualimu ya Chuo cha Ualimu Nkrumah Zanzibar, shahada ya   kwanza ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, shahada ya uzamili katika Sanaa na shahada ya Uzamivu ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma. Kat
Image
NUKUU MARIDHAWA   "Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuimarisha au kubomoa umoja wa kitaifa. Navipongeza vyombo vya habari vya zanzibar kwa kuchagua kujenga na kuimarisha umoja, maelewano, amani na utulivu wa nchi yetu katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020,". Ni kauli ya Mkuu wa mkoa wa Mjini Maghraibi, Idrissa Kitwana Mustafa, alipokuwa akifungua mafunzo ya waandishi wa habari juu ya kuandika habari za kuimarisha amani, uvumilivu wa kisiasa na utamaduni wa kupokea maoni tofauti kabla, wakati na baada ya uchaguzi yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar ( #ZanzibarPressClub ) kwa ufadhili wa #Internews Tanzania. #amani_yet_fahari_yetu #zpc_internews
Image
  Kijichi wapongeza kasi ya awamu ya nane NA MWANDISHI WETU WANACHAMA na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), jimbo la Bububu wametakiwa kuendeleza ushirikiano walionao ili kuongeza kasi ya maendeleo ya jimbo hilo na watu wake. Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya ya Magharibi 'A' ambae pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Suzan Peter Kunambi, alipokuwa akizungumza na wanachama hao katika tawi la CCM Kijichi. Alieleza kuwa serekali ya awamu ya nane imelenga kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hivyo ushirikiano baina ya viongozi, wanachama na wananchi ni muhimu ili kufikia malengo yaliyowekwa. “Mnaposhikamana na kushirikiana kama ilivyo katika jimbo lenu, mnaweza kwenda mbali zaidi na kufikia maendeleo makubwa katika kipindi kifupi. Na hilo ndilo lengo la serikali inayoongozwa na Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,” alieleza Suzan. Aidha Mkuu huyo wa wilaya ambae alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kask
Image
Wizara ya utalii, mambo ya kale yatoa muongozo kulinda maadili NA KHADIJA KHAMIS, MAELEZO - ZANZIBAR WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale,   Lela Muhamed Mussa, ametoa muongozo kwa wageni na watalii wanaoingia nchini  kufuata maadili yanayohusiana na mavazi ili kwenda sambamba na mila silka maadili na utamaduni wa kizanzibari . Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari alisema hivi karibuni kumejitokeza ukiukwaji wa maadili hususani katika suala la mavazi kwa baadhi ya wageni na watalii wanaotembelea nchini. Alifahamisha kuwa wageni na watalii wanatakiwa kufuata maadili ya nchi kwa kuvaa nguo za stara wanapokuwa katika  sehemu  za umma  ili kuepusha kero na maudhi kwa wananchi. Alieleza  kuwa kushindwa kuifuatilia na kuisoma miongozo ya maadili ambayo imekuwa ikitolewa na taasisi zinazosimamia utalii nchini ni miongoni mwa sababu zinazopelekea utaratibu mbaya wa mavazi kwa wageni hao. Waziri Lela, alisema hali hii haitoi sura nzuri na inaashiria kutokuwepo uwajibikaji wa pamoja na
Image
  SMZ yaahidi mazingira mazuri kuibua viongozi wanawake NA MWANDISHI MAALUM IMEELEZWA kuwa iwapo kutawekwa mazingira mazuri ya sera na sheria kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza idadi ya viongozi wanawake serikalini na katika vyombo vya maamuzi. Akizindua muongozo wa ‘ushiriki wa wanawake katika uongozi’, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) itafanya hivyo kuunga mkono juhudi asasi za kiraia zilizolenga kutoa kipaumbele kwa mwanamke katika nafasi za uongozi. Uzinduzi wa muongozo huo ulioandaliwa kwa pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Chama cha Wanasheria Wanawake (ZAFELA) na Jumuia ya Jinsia na Utetezi wa Mazingira Pemba (PEGAO), ulifanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil,   Kikwajuni mjini Unguja Februari 14, 2021. Mhandisi Zena, alisema serikali ya awamu ya nane itajitahidi kuondoa vikwazo vyote, ikiwemo urasimu ili kuhakikisha wanawake wanapewa fursa na
Image
J PM akitaka kiwanda cha mpunga kuitangaza Tanzania NA IMMACULATE MAKILIKA, MAELEZO RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  amekitaka kiwanda cha mpunga kinachozalisha bidhaa za  Korie kuwa na bidhaa zenye jina la kitanzania ili zisaidie kuitangaza nchi kimataifa. Rais Magufuli ameyasema hayo leo mkoani Morogoro wakati akifungua kiwanda cha Kukoboa Mpunga cha Murzar Wilmar Mill, kilichopo Kihonda  mkoani  Morogoro. “Natoa rai kwa muwekezaji kutengeneza bidhaa zenye jina linalohusu nchi yetu kwa sababu Tanzania tumekuwa tukizalisha vitu vingi lakini hatutangazi nchi yetu. Siwazuii kuendelea na jina la Korie lakini kuwe na jina jingine linalotangaza nchi”, alisema Rais Magufuli. Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa bila kuwa na viwanda hakuna uchumi, viwanda ndio sehemu pekee inayotengeneza ajira za watanzania, na kuwa alipoingia madarakani aliamua kuhakikisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano Serikali inajenga jumla ya viwanda 8,477, sambamba kufikia azma yake
Wajumbe wa ACT Wazalendo wala kiapo NA MWANDISHI WETU WAJUMBE wapya watano wa Baraza la Wawakilishi Zaznzibar, wameapishwa katika siku ya kwanza ya mkutano wa pili wa baraza hilo ulioanza Februari 10, mwaka huu. Spika wa baraza hilo Zubeir Ali Maulid, amewaapisha wajumbe hao kutoka kutoka chama cha ACT  Wazalendo akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui. Walioapishwa ni Mwanasheria wa Omar Said Shaabani, Nasor Ahmed Mazrui ambao ni wajumbe wa baraza hilo waliotokana na uteuzi wa Rais wa Zanzibar. Wajumbe wengine walioapishwa ni Habib Ali Mohamed, Mwakilishi wa Mtambwe, Hassan Hamad Omar kutoka jimbo la Kojani na Kombo Mwinyi Shehe, kutoka jimbo la Wingwi. Akizungumza mara baada ya kuapishwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe, Habib Ali Mohamed, alisema atafanya kazi hiyo kwa kuwakilisha wananchi bila ya ubaguzi pamoja na kutoa hoja zenye maslahi kwa maisha yao. Alisema wawakilishi wote wana lengo linalofanana na ni vyema wakashirikiana kwa pamoja ili
Image
  Dk. Mwinyi   abainisha ufanisi wa serikali ndani ya  siku 100 akiwa ofisini NA MWANDISHI MAALUM RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi, amesema katika kipindi cha siku 100 za uongozi wake amefanikiwa kuteekeleza mambo 10 kwa ufanisi zaidi. Dk. Mwinyi alieleza hayo ikulu mjini Zanzibar wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kutimiza siku 100 tangu aliapishwa Novemba 2 mwaka jana. Alisema katika kipindi hicho kifupi amefanikiwa kuleta umoja wa kitaifa kwa kuweka maridhiano ambayo yameongeza ushirikiano miongoni mwa wananchi na kule amani na utulivu. Alisema ameunda serikali yenye muundo wa umoja wa kitaifa ili kondosha yanayotokea kila baada ya uchaguzi mkuu na kwamba mshikamano amani na utulivu utaongeza kasi ya maendeleo ya nchi. Alifahamisha kuwa apanga kuona vyombo vya sheria vinafanyakazi yake vizuri ikiwemo kuipa nguvu Mamlaka ya Kupambana na Rushwa na Uhujumu (ZAECA), kwani imebaini kuwepo kwa wizi mkubwa katika Mik
Image
  DC Suzan ataka waliokopa warudishe mikopo kwa wakati NA MWANDISHI WETU MKUU wa Wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi (pichani), amewataka wanaushirika wa kuweka na kukopa Kibweni (Kibweni Saccos) kurejesha mikopo kwa wakati ili kuendeleza ushirika huo. Alisema hayo katika Skuli ya Bububu, wilayani humo alipofungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho na kusema umefika wakati kwa wanaushirika kutilia mkazo umuhimu wa kurejesha mikopo katika vyama vyao na faida inayopatikana iwanufaishe wote. Alisema tabia ya wanachama kuchukua mikopo kisha kushindwa kurejesha kwa wakati inasababisha vyama vya ushirika kushindwa kujiendesha wenyewe na na hatimae kusubiri wahisani. Kunambi alisema vyama vya ushirika ni muhimu katika maendeleo ya nchi na inasaidia kuinua uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja hivyo aliwataka wanaushirika kuibua miradi ya maendeleo kuendeleza vyama hivyo. Aidha aliwapongeza wana ushirika hao kwa kuanzisha ushirika imara ambao umekuwa mfano ndani ya wilaya hiyo
Image
  Skuli ya Upendo yapongezwa kutoa mwanafuzi bora kitaifa Yatoa wanafunzi watatu bora kitaifa mitihani STD 4, Veronica Mwendesha ashika nafasi ya kwanza Zanzibar NA MWINYIMVUA NZUKWI VIONGOZI wa jimbo la Bububu, wilaya ya Magharibi ‘A’, Unguja, wameeleza kuwa wataendelea kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya jamii ikiwemo elimu ili kupata taifa linalojitegemea kwa wataalamu. Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa wadi ya Dole, Juma Wiliam Sungwa, kwa niaba ya Mwakilishi wa jimbo hilo Mudrik Ramadhan Soraga, katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa skuli ya maandalizi na msingi, Upendo iliyopo shehia ya Kizimbani Unguja, iliyotoa mwanafunzi bora kitaifa katika mitihani ya darasa la nne iliyofanyika mwaka uliopita Zanzibar. Alisema mafaniko ya skuli hiyo kutoa wanafunzi watatu katika nafasi tano za juu kitaifa katika mitihani hiyo ni ya kupongezwa na inapaswa kuungwa mkono na kila mmoja miongoni mwa wananchi wa jimbo hilo. Alifafanua kuwa licha ya kuwa skuli hiyo kumilikiwa na taasisi b