Posts

Showing posts from April, 2022

Majaliwa: Zingatieni weledi, maadili ya vyombo vya habari

Image
LINDI WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ili  kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi  vyombo vya habari havina budi kufanya kazi kwa k uzingatia maadili na weledi  pamoja na kutanguliza uzalendo na maslahi ya taifa. Pia, Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Serikali itaendelea k usimamia matumizi ya mitandao ya kijamii ili pamoja na kuongeza upatikanaji wa habari kuwepo na uzingatiaji wa maadili na weledi. “ Ni matarajio yetu kuwa moja ya majukumu yenu ni kulisemea Taifa letu.”   Ameyasema hayo Aprili 14, 2022  wakati akizindua vituo vya kurushia matangazo ya redio vya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wilayani Ruangwa, mkoani Lindi kwa niaba ya vituo vingine vya wilaya za Ludewa (Njombe), Mlimba (Morogoro) na Ngara (Kagera). Amesema SERIKALI itahakikisha uhuru wa vyombo vya habari nchini unaimarishwa na kulindwa hivyo wamiliki na wanahabari wanatakiwa kuzingatia maadili ya kazi zao ili wananchi waendelee kupata taarifa sahihi, kwa urahisi zaidi na kwa wakati. Waziri Mkuu

Ujerumani kusaidia utafiti wa maji Z'bar

Image
ZANZIBAR SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Shirikisho la Ujerumani zimetiliana saini mkataba wa ruzuku ya utafiti na upembuzi yakinifu katika sekta ya maji unaolenga kujua ubora na wingi wa maji yanayopatikana Zanzibar. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk. Juma Malik Akil (kulia), akisaini makubaliano ya ruruku kwenye utafiti na upewa majihayo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Dk. Salha Kassim (kushoto) na Naibu Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kibenki la Ujerumani, Andrea Hoeltke (katikati). Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Johannes Sperrfechter ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi na ushirikiano wao ambao unalenga kujenga maisha bora ya Wazanzibari. Alisema hatua hiyo ni mwendelezo wa ushirikiano mpya wa kimaendeleo kati ya Ujerumani na Zanzibar uliozinduliwa mwezi Januari 2022 kwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi na Balozi wa Uje

Serikali, NMB zasaini makubaliano kukuza kilimo

Image
DODOMA WIZARA ya Kilimo na Benki ya NMB, zimeingia makubaliano ya kukuza sekta ya kilimo nchini ambapo benki hiyo imetenga shilingi bilioni 120 kwa ajili ya mikopo ya ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao vijijini na kukuza kilimo nchini. Akizungumza katika hafla ya kusaini makuliano hayo iliyofanyika katika hoteli ya Morena mjini Dodoma, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliipongeza benki ya NMB kwa juhudi za kusaidia ukuzaji wa sekta ya kilimo nchini. Alisema moja ya changamoto wanayokabiliana nayo wakulima nchini ni mazao yao kupoteza ubora kabla ya kufika sokoni kutokana na mazingira mabaya ya kuhifadhi hivyo makubaliano hayo yanakwenda kupunguza changamoto hiyo. “Kule vijijini ukiona magunia mengi ya mazao yamewekwa kwenye eneo la mashine za kusaga, usifikiri kuwa ni mali ya mwenye mashine hiyo. Magunia hayo ni mali ya wakulima yamehifadhiwa hapo baada ya kukosa ghala la kuhifadhia na yanapofika sokoni, yanakuwa yamepoteza ubora na thamani yake,” alisema Bashe. Aidha Waziri Ba
Image
Andikeni habari zinazochochea ulipaji kodi kwa hiyari – ZRB NA MWANDISHI MAALUM KAMISHNA wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Yussuf Juma Mwenda (pichani), ameviomba vyombo vya habari kuandika habari zinazochocheo ulipaji kodi kwa hiyari. Mwenda alitoa rai hiyo alipokutana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tunzo za umahiri wa uandishi wa habari Zanzibar (EJAZ) na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD), ofisini kwake Mazizini Unguja. Alieleza kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na vyombo vya habari kuelimisha jamii, mkazo zaidi unapaswa kuwekwa kwenye kuhamasisha matumizi ya mashine za kutolea risiti za kielektroniki ili kuongeza ufanisi kwenye ukusanyaji wa kodi za serikali na biashara nchini. Aliongeza kuwa waandishi wa habari pia wanaweza kuandika habari zitakazoonesha umuhimu na faida ya kodi kwa wananchi ili wawe na utamaduni wa kudai na kutoa risiti wanapofanya mauziano. "Tungependa kupitia habari zenu mtushauri namna gani tunaweza kuifanya ZB
Image
Wizara yahimizwa kukamilisha ujenzi ofisi za ZBS NA MWANDISHI WETU KAMATI ya bajeti ya Baraza la Wawakilishi imeitaka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa ofisi za Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) ili kuipa uwezo wa kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi. MWENYEKITI wa Kamati ya bajeti, Abdalla Hussein Kombo (kulia) akiongoza kikao cha kamati na viongozi wa W izara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda.  Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa ZBS Yussuph Majid Nassor, katikati ni Katibu Mkuu  Dk. Islam Seif. Akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo, uongozi wa wizara na taasisi hiyo, kilichofanyika katika ofisi za ZBS Amani, Mwenyekiti wa kamati hiyo Abdalla Husein Kombo, alieleza kuwa iwapo taasisi hiyo itaongezewa uwezo, mapato na ufanisi utaongezeka. Alieleza kuwa ujenzi wa ofisi za taasisi hiyo unaojumuisha maabara za kupimia na kuchunguza ubora wa bidhaa mbali mbali ni sehemu muhimu ya mafanikio ya taasisi hiyo hivyo ni vyema ikazingatia umuhi