Posts

Showing posts from May, 2022

TAARIFA MAALUM KWA WAANDISHI WA HABARI

Image
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAOMBI YA WAANDISHI KWA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. HUSSEIN ALI MWINYI Awali ya yote napenda kutumia fursa hii kwa niaba ya Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), kuwajullisha ya kwamba baadhi ya mambo yaliyowasilishwa na waandishi wa habari mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kikao cha tarehe 18/05/2022 yameanza kufanyiwa kazi. Katika kikao hicho cha faragha kilichofanyika katika Ikulu ya Zanzibar, waandishi wa habari walipata fursa ya kuzungumza na Rais mambo mbali mbali yanayohusu mwendendo na hali halisi inayohusiana na tasnia ya habari nchini, hali tunayoamini imeongeza uelewa wa kiongozi huyo wa nchi na wasaidizi wake juu ya mazingira ambayo waandishi wa habari wa Zanzibar wanayofanyia kazi. Pamoja na maelezo ya waandishi ambayo baadhi yao yalipatiwa majibu na kutolewa ufafanuzi wakati wa kikao hicho, pia waandis

Waandishi watakiwa kuwa makini matumizi mitandao

Image
NA ASYA HASSAN WAANDISHI wa habari wametakiwa kutanua wigo katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kurahisisha utendaji wao wa kazi na kuleta tija. MWENYEKITI wa klabu ya waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), Abdallah Abdulrahman Mfaume, alisema hayo alipokuwa akifungua kongamano la wadau wa habari ikiwa ni miongoni mwa shudhuli za maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ngazi ya klabu. Alieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kubadilisha jamii kutumia mitandao hiyo kwa faida badala ya hasara kutokana na jukumu kubwa la kuelimisha jamii na kuleta mabadiliko katika nchi. Sambamba na hayo Mwenyekiti huyo aliiomba serikali kuendelea kushirikiana na wadau wa habari kufanya mapitio ya sheria, sera na kanuni zinazosimamia sekta ya habari ili kuondosha changamoto zinazokwaza uhuru wa Habari na Uhuru wa kujieleza. Hata hivyo aliwasisitiza waandishi wa habari kuzalisha habari na vipindi bora ili vyombo vya habari viendelee kuwa daraja la kupashana Habari