Posts

Showing posts from January, 2024

Mama Mariam aelekeza namna ya ulaji vyakula vya lishe

Image
NA MWANDISHI WETU   MKE wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF),   Mariam Mwinyi, ameitaka jamii kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe hasa kwa watoto na mama wajawazito ili kuwa na afya bora. 1.        MKE wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na Msarifu wa taasisi ya zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, akihutubia wananchi wakati akifunga rasmi kampeni ya siku ya afya na lishe ya kijiji katika shehia ya Donge Vijibweni, mkoa wa Kaskazini Unguja. Mama Mariam alieleza hayo jana alipokua akifunga wiki ya afya na lishe ngazi ya shehia huko Donge Vijibweni wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, iliyoambatana na maonesho ya vyakula vya lishe na utoaji wa huduma na elimu ya afya. Alieleza kuwa ili kuwa na jamii bora kuna umuhimu wa kuimarishwa kwa elimu ya lishe katika ngazi ya jamii ili kuondoa changamoto ya utapia mlo na udumavu kwa watoto. Alieleza ku

Balozi Mpanda ahimiza ubunifu uhifadhi wa mazingira

Image
JUVIEKA, wadau wapanda mikoko 2,540 Mtopwani NA MWANDISHI WETU JUMLA ya miche ya miti ya mikoko 2,540 imepandwa katika eneo la Mdodo madema, Shehia ya Mto wa pwani mkoa wa Kaskazini Unguja ili kutunza mazingira ya eneo hilo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mratibu wa zoezi hilo ambaye ni kiongozi wa Jumuiya ya Vijana ya Uhifadhi wa Mazingira, Mbarouk Maalum, alieleza kuwa zoezi hilo lililofanyika jumapili iliyopita lilihudhuriwa na wanaharakati wa mazingira 117 kutoka taasisi na makundi mbali mbali ya jamii. Aliongeza kuwa miongoni mwa washiriki hao ni vikundi vitano vya wanufaika wa mpango wa MKUBA, wanachama na viongozi wa mabaraza ya vijana ya Shehia za Mtowapwani na Chutama,   wawakilishi taasisi za JUVIEKA, UNA, ZAFELA pamoja na Sheha wa Shehia hiyo na wananchi wake. Aidha maalum alieleza kuwa shughuli hiyo pia ilihudhuriwa na Balozi wa mazingira kutoka ofisi ya rais, Muungano na Mazingira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Khadija Yussuph Mpanda ambaye pia ni mion