Posts

Showing posts from April, 2024

NBC yazindua kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako’ kukuza uchumi wa wateja wake

Image
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni mpya ya akiba inayolenga kuunga mkono juhudi za serikali za kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia huduma za kidigitali zinazotolewa na taasisi za kifedha nchini. Kampeni hiyo ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako’ inawahusu wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi ambayo itaambatana na   zawadi mbali mbali ikiwemo ya gari mbili aina ya BMW x1. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es salaam jana, Mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo, David Raymond, alieleza kuwa mpango huo unalenga kuimarisha ustawi wa kifedha miongoni mwa wateja wa benki hiyo na kuchochea ukuaji wa uchumi jumuishi kupitia huduma rasmi za kifedha. “Tunanalenga kuitumia falsafa ya mchezo wa soka ambao benki ya NBC ni Wadhamini wakuu wa ligi tatu. Tunapoingiza falsafa hiyo kwenye maisha ni wazi tunatambua wateja wetu wana ndoto, malengo na maazimio katika kufanikisha maendeleo yao kiuchumi yakiwemo ya ujenzi, kukuza biashar

Mfumo kidigitali anuani za makaazi wazinduliwa

Image
NA SAIDA ISSA, DODOMA SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Wizara ya nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI imezindua majaribio ya kutoa huduma ya barua ya utambulisho wa mkazi kupitia mfumo wa kidijitali wa anwani za makazi (NaPA). Hatua hiyo ilienda sambamba na kutoa vitendea kazi kwa watendaji wa Kata na Shehia zitakazofanyiwa majaribio kwa Tanzania bara na Zanzibar. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Khamis Abdullah (pichani) aliyesema mfumo wa anuani za makazi umetengenezwa kwa dhumuni la kimarisha utoaji wa huduma ndani ya serikali na sekta binafsi ili kuiwezesha nchi kunufaika na fursa za uchumi wa kidijitali na kuimarisha masuala ya utambuzi na usalama ndani ya nchi. Aidha alisema kuwa ‘operesheni anuani za makazi’ ilikuwa na mafanikio ambapo zaidi ya anuani za makazi milioni 12.3 zilisajiliwa na taarifa zake kuhifadhiwa kwenye mfumo anuani za makaazi wa taifa (NaPA).

Dk. Samia akemea viongozi wachonganishi

Image
NA MWANDISHI MAALUM, MUNDULI RAIS   wa   Jamhuri   ya   Muungano   wa   Tanzania,   Dk.   Samia   Suluhu   Hassan ameeleza kusikitishwa kwake na baadhi ya viongozi wasiotambua dhamana walizonazo wanaotumia   nafasi   zao   kuchonganisha serikali na jamii badala  ya   kuleta  maelewano. Rais Samia amesema hayo, wakati akizungumza katika Kumbukumbu ya Miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine huku akiwasisitiza viongozi kuiga mfano  wa Sokoine kwani alikemea jambo hilo kwa maneno na vitendo. Rais    Samia    amesema    Hayati Sokoine    alitumia    utashi    wake    wa    hali    ya    juu kuimarisha    mahusiano    kati    ya    serikali    na    jamii    aliyoiongoza    na    kuiwakilisha vyema jamii ya Wamaasai. Aidha amewataka    viongozi    wa    sasa    na    wajao   kutambua    kuwa    uamuzi ukifanyika ndani ya serikali ni wajibu wao kuutekeleza kama ulivyo hata ikibidi wao wawe mfano kwa wengine kama Hayati Sokoine alivyofanya. Kuhusu    umuhimu    wa    elimu  

Ujenzi wa ofisi, maabara za ZBS Pemba kukamilika mwaka huu

Image
TAASISI ya Viwango Zanzibar (ZBS) imesema ina mpango wa kutekeleza mradi  wa ujenzi wa ofisi na maabara mbali mbali za kisasa za ukaguzi huko Chamanangwe kisiwani Pemba ili kuongeza ufanisi. Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Yussuph Majid Nassor,  ameyasema hayo wakati akifungua Jukwaa la Vyombo vya Habari lililoandaliwa na taasisi hiyo kwa uratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) na kufanyika katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo, Maruhubi wilaya ya Mjini Unguja. MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS), Yussuph Majid Nassor, akizungumza wakati wa jukwaa la pili la viwango na vyombo vya habari katika ofisi za taasisi hiyo Maruhubi. Kulia ni Meneja Uhusiano na Masoko wa taasisi hiyo Aisha Abdulkheir na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), Tabia Makame Mohammed.  Amesema hatua hiyo imelenga kuongeza ufanisi wa taasisi hiyo kwenye ukaguzi, udhibiti na uthibitishaji wa viwango vya bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa nch