Posts

Showing posts from March, 2023

TANESCO yazindua programu kukuza usawa kijinsia

Image
NA SAIDA ISSA, DODOMA NA SAIDA ISSA, DODOMA SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limezindua programu ya miaka minne ya mpango wa kuimarisha usawa wa jinsia wenye lengo la kutatua changamoto za wanawake katika maeneo ya kazi ikiwemo ya vitendo vya unyanyasaji. Akizugumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, alisema mradi huo unalenga kutengeneza sera za shirika na kujenga uwezo kuhusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia.   Alisema mradi huo, utasaidia kuwepo kwa taarifa sahihi za unyanyasaji wa kijinsia katika shirika, kuruhusu fursa ya ukuzaji taaluma kwa wafanyakazi wanawake  na kuongeza mafunzo kwa vitendo kwa wafanyakazi wanawake waliopo kazini.   Alieleza kuwa mradi huu unatekelezwa na TANESCO lengo ni kuhakikisha watumishi wanaofanya kazi katika taasisi hiyo wanapata haki sawa, lengo ni kuhakikisha nafasi zinazojitokeza zinahusisha  jinsia zote bila ubaguzi na kujenga usawa.   "Katika mradi huo tumekubaliana kuunda kitengo

Masheha, Madiwani wapewa elimu miradi ya TASAF

Image
NA MWANDISHI WETU, PEMBA VIONGOZI wa Shehia na Wadi kisiwani Pemba wametakiwa kusimamia vyema miradi ya kuwaondolea wananchi umaskini ili itoe matokeo chanya. Ofisa Mdhamini Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Pemba, Abdullwahab Said Bakari, alitoa wito huo na kusema kufanya hivyo ni kutekeleza malengo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kupunguza umaskini kwa wananchi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi. Alisema serikali imepanga mpango wa kupunguza umaskini na kuongeza ukuaji wa uchumi jumuishi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) ambayo imeweka sifa kwa walengwa wake. Bakari alieleza hayo wakati akifungua mafunzo kwa Masheha na Madiwani wa mkoa wa Kusini Pemba yaliyolenga kuwajengea uwezo viongozi wanaosimamia shughuli za mpango wa kunusuru kaya maskini Tanzania, ulioandaliwa na TASAF Pemba. “Hivi sasa kuna changamoto nyingi nyinyi kutoka kwa walengwa, Masheha na Madiwani mnatakiw

Wajasiriamali wanakuza viwango

Image
NA MWANDISHI WETU SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema wajasiriamali wanamchango mkubwa katika kukuza viwango nchini na Afrika kwa ujumla. Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Abdulghulam Hussein alieleza hayo katika maadhimisho ya siku ya viwango Afrika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni. Alisema Rais Mwinyi amekuwa akiwawezesha wajasiamali wadogo kwa kuwawekea fedha ambazo zitawasaidia kuendesha biashara zao kwa ajili ya kujipatia kipato cha kuweza kujikimu. “Ujasiriamali unawezesha vijana kujiajiri wenyewe na kupata fedha za kujikimu kimaisha lakini pia kukuza pato na uchumi wa nchi ndio maana serikali imekua ikijidhatiti kuweka sera nzuri za elimu na mikakati thabiti ya kulinda na kukuza biashara za wajariamali”, alieleza Naibu Waziri. Hivyo alisema vyuo vikuu vinaweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza tasnia hiyo kwa kufanya tafiti pamoja na kuzalisha wataalamu na wabunifu watakaochochea maendeleo. Aliwataka wakuu wa vyuo vi

Maelfu wamzika Mwakilishi wa Mtambwe

Image
 NA MWANDISHI WETU MAKAMU wa Pili wa Raiswa Zanzibar,  Hemed Suleiman Abdalluh,  ameongoza maelefu ya wananchi na viongozi wa serikali na vyama vya siasa katika maziko ya aliyekua mwakilishi wa jimbo la Mtambwe Pemba,  Ali Mohammed (pichani). Mwakilishi huyo aliyefariki Machi 3, 2023 taarifa za kifo chake zilitangazwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid, muda mchache kabla ya kuakhirishwa kwa mkutano wa 10 na kikao cha baraza. Mbali ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Spika Zubeir, viongozi wengine waliohudhuria maziko hayo ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman Masoud Othman, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo anachotoka mwakilishi huyo. Akitoa salamu za serikali wakati akiakhirisha mkutano huo, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani, Hemed a lisema huo ni msiba mzito kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wananchi wa Zanzibar na familia huku akimuombea kwa Mwenyezi Mungu kumsamehe makosa yake na kumlaza mahali pema. M