Posts

Showing posts from October, 2022

SMZ yajidhatiti kusimamia haki, ulinzi wa watoto

Image
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imejipanga kuimarisha ulinzi na kusimamia upatikanaji wa haki za watoto  katika ngazi ya jamii.  WAZIRI wa Maendeleo, Jinsia, Wazee, Wanawake na Watoto, Riziki Pembe Juma (pichani),   alieleza hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi wakati wa sherehe  maadhimisho ya miaka 77 ya Umoja wa Mataifa (UN) yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, Unguja.  Amesema hatua hiyo itasaidia kulinda haki, fursa na kuimarisha ustawi na maendeleo hasa katika upatikanaji wa haki za watoto pamoja na kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.  Amesema mikakati huo  utakuwa pamoja na kuwajengea uwezo wa kisheria   wanawake  ili waweze  kulinda na kusimamia haki na  mambo mengine ya msingi ya nayo stahiki kupatiwa watoto.  Mbali na hilo amesema  Wizara hiyo itafanya kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa  kwa kuhimiza na kushajihisha  wanawake kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ili kushika nafasi ya uong

Senyamule awaita watanzania kupokea matokeo ya sensa

Image
NA SAIDA ISSA, DODOMA MKUU wa Mkoa wa Dodoma,   Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kuhudhuria   kwa wingi katika viwanja vya Jamhuri kushuhudia uzinduzi wa matokeo ya   mwanzo ya sensa   ya watu na makazi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Senyamule wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato Oktoba 30, mwaka huu amesema   ni vyema wana-Dodoma na Watanzania   kwa ujumla kushiriki katika shughuli hiyo ya kihistoria kufuatia sensa inayofanyika kila   baada ya miaka 10. "Ni siku ya kipekee na hapa tuna siku moja kufika siku ya kutangaziwa matokeo na Mheshimiwa Rais   wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, nitoe shime wana Dodoma mje   kwa wingi kuanzia saa 12 asubuhi hapa kwenye viwanja   vya Jamhuri,” amueleza Mkuu huyo wa mkoa. "Leo (31 Oktoba) kuanzia saa 6 usiku tutakuwa na shamra shamra ya kupiga fataki zikiashiria kuwa Dodoma tupo tayari kuletewa matokeo ya   sens

Uzalishaji sukari kufikia tani 756,000 mwaka 2025

Image
NA SAIDA ISSA, DODOMA SERIKALI imesema imeweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa sukari   kutoka tani 380,000 inayozalishwa sasa nchini hadi tani 756,000 ifikapo mwaka 2025. Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa  Bodi ya Sukari  Tanzania, Profesa Kenneth Bengesi (pichani) alipokuwa akielezea  muelekeo  wa utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo  kwa mwaka wa fedha  2022/ 2023. Alieleza kuwa mpango wa serikali ni kuhakikisha kwamba mpaka ifikapo mwaka 2025/2026 nchi inakuwa na sukari ya kutosha pamoja na ongezeko  la viwanda vya  kuzalisha sukari. Alisema miaka ya nyuma nchi ilikuwa inaagiza sukari hadi tani 183,000 lakini serikali imefanya juhudi zilizopunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi kutoka tani 144,000 mwaka 2017 hadi tani 50,000 kufikia Juni, 2022. “Tangu tupate uhuru, ndio tumepata wawekezaji katika upande wa sukari ikiwemo kiwanda cha sukari Bagamoyo na cha Mkulazi kinachotarajiwa kuanza mwaka 2023. Kuna upanuzi mkubwa wa kiwanda cha Kilo

TEWW yawafikia wasichana 3,333 walioshindwa kuendelea sekondari

Image
  NA SAIDA ISSA, DODOMA TAASISI ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imefanikiwa kuwafikia wasichana 3,333 walioshindwa kuendela na masomo ya sekondari kutokana na mazingira magumu, kupata ujauzito na ndoa za utotoni. Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dk. Emanuel Ng'umbi (pichani) ambapo alisema kuwa idadi hiyo ni sawa na asilimia 111 ya lengo ambapo waliendesha mafunzo kwa nyakati tofauti kwa wasimamizi na watendaji, wawezeshaji na walimu wa madarasa ya mradi wa SEQUIP. "Kwa mwaka 2022/2023, TEWW itaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Tekonolojia kuandaa Juma la Elimu ya Watu Wazima, vile vile TEWW itahamasisha, kusajili na kufundisha wanafunzi 3,000 wa mradi wa SEQUIP kwa mwaka 2023," alisema. Aliongeza kuwa   TEWW inatarajia kupanua mpango wa IPOSA katika mikoa mipya sita ya Tanzania bara kwa kujenga karakana za kufundishia na kupanua mafunzo ya TEHAMA kwa wanafunzi wa IPOSA. “Kwa upande wa programu ya IPPE, TEWW inataraj

Mchakato ujenzi kituo cha biashara, mikutano kimataifa waanza

Image
NA MWANDISHI WETU WIZARA ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imeeleza kuwa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa uwanja wa maonesho ya biashara ya kimataifa na kituo cha mkutano na hoteli, kutaimarisha uchumi wa Zanzibar. Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya utekelezaji wa upembuzi yakinifu wa ujenzi wa uwanja wa maoenesho ya biashara na kituo cha mikutano kimtaifa katika ofisi za wizara hiyo Kinazini, Waziri, Omar Said Shaaban wa wizara hiyo alieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuirudisha Zanzibar katika hadhi yake kibiashara. Alieleza kuwa kusainiwa kwa makubaliano hayo kunakwenda kutekeleza ndoto za Zanzibar kuwa na kumbi za mikutano za kimataifa zinazoweza kuchukua idadi kubwa ya watu na vifaa vya kisasa kutekeleza dhana ya uchumi wa buluu. Alisema kuwa ukumbi huo pamoja na hoteli ya kisasa vitajengwa Mbweni wakati kituo cha maonesho ya biashara kitakachojengwa Nyamanzi, wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja, kinalenga kusisimua biashara na kuirudisha Zanzibar k

Tembo Warriors yatinga robo fainali kombe la dunia AMPUTEE

Image
Na John Mapepele TIMU ya taifa ya soka la watu wenye ulemavy ya tanzania 'Tembo Warriors' Oktoba 5, 2022 imeendelea kuishangaza dunia kwa  kuibamiza vibaya timu kali ya Japan katika mashindano ya kombe la dunia  yanayoendelea nchini Uturuki. Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini,  Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu wake Dkt. Hassan Abbasi  wameongoza kutoa hamasa na mikakati ya ushindi huo wakiungana na watanzania waishio Uturuki. Katika kipindi  chote Tembo Warriors wamekuwa wakicheza kama ndiyo  wanaanza mpambano hadi kipenga  cha mwisho. Hadi kipindi cha kwanza kilipokwisha mabao yalikuwa 1-1 huku Tembo wakiwa wa kwanza  kuliona goli la Japan katika dakika ya 19 ya mchezo ambapo Japan walilazimisha penalti iliyowapatia goli la kufutia machozi. Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Waziri Mchengerwa amesema timu hiyo imeonesha uzalendo mkubwa kwa Taifa lao kilichobaki ni kumalizia kutwaa kombe Kwa kuwa  wanauwezo mkubwa wa kurudi na kombe hilo nyumbani. Aidha, amefafanua ku