Posts

Showing posts from February, 2022
Image
Polisi, wanahabari wakubaliana kushirikiana NA MWANDISHI WETU WAANDISHI wa habari na watendaji wa jeshi la polisi wameahidi kuendelea kushirikiana katika utendaji wa kazi zao kwa maslahi ya taifa. Makubaliano hayo yalifikiwa katika mdahalo wa kitaaluma ulioyakutanisha makundi mawili hayo na kujadili wajibu na majukumu yao. Mdahalo huo uliokuwa na maudhui ya usalama kwa waandishi wa habari na mahusiano kati ya waandishi wa Habari na jeshi la polisi, yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kupitia   mradi wa usalama kwa wandishi wa habari unaotekelezwa na muungano wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na Shirika la International Media Support (IMS). Akifungua mdahalo huo uliofanyika katika jengo la ZURA mjini Unguja, Mwenyekiti wa ZPC, Abdalla Adulrahman Mfaume, alisema jeshi la polisi lina wajibu wa kuhakikisha waandishi wa habari wanafanya kazi katika mazingira salama na kuhakikishiwa ulinzi. Hata hivyo, alisema wakati mwengine hujitokeza cha
Image
ZBS yatekeleza agizo la Dk. Mwinyi kuwezesha wajasiriamali NA MWANDISHI WETU WAJASIRIAMALI nchini wametakiwa kuzingatia ushauri na maelekezo yanayotolewa na Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) ili kuimarisha uzalishaji na kuyafikia masoko. Wito huo umetolewa na mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo, Yussuf Majid Nassor, katika hafla ya utoaji vyeti vya ithibati ubora kwa wajasiriamali, iliyofanyika katika ofisi za taasisi hiyo Amani, mjini Unguja. Alieleza kuwa mchakato wa ukaguzi na kuwathibitisha wajasiriamali hao ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliyezitaka taasisi zinazohusika na wajasiriamali kuwasaidia na kuwaendeleza ili kukuza ajira nchini. Alieleza kuwa kabla ya hatua hiyo, wajasiriamali kutoka vikundi 10 walipatiwa mafunzo na kufuatiliwa kuelekezwa namna ya kuzalisha bidhaa zenye ubora ambapo vikundi vinne vimekamilisha hatua zote na kupatiwa alama ya ubora ya ZBS. “Hawa sita waliobakia bado
Image
Dk. Mwinyi atengua uteuzi wa Kamishna Mkuu ZRB NA MWANDISHI MAALUM RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (pichani), ametengua uteuzi wa Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Salum Yussuf Ali ili kupisha uchunguzi wa kina wa upotevu wa   fedha za makusanyo ya mapato zilizopotea. Rais Dk. Mwinyi amefikia maamuzi hayo leo wakati akiwa katika Ofisi za Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Mazizini Zanzibar ambapo alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Bodi ya Mapato, Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mapato   pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo. Dk. Mwinyi alifikia iuamuzi huo akiwa katika ofisi za ZRB na kuiagiza Bodi ya mamlaka hiyo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Usajili, Ukaguzi na Upelelezi wa Walipa Kodi, Hashim Kombo Haji kupisha ukaguzi wa kina wa maelekezo yake ya kuondoa taarifa za ukaguzi ambazo hatimae hazikupelekwa kwen
Image
  ZPC, CPS Ltd zaazimia kuimarisha ushirikiano NA MWANDISHI MAALUM KATIKA kuimarisha mahusiano na ushirikiano kati ya Klabu ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) na wadau wake, viongozi   wa klabu wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti,   Tabia Makame Mohammed (Februari   7, 2022)   wametembelea na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CPS Ltd Tobias Dietzold. kampuni ya CPS Ltd inayojenga Mji wa Maendeleo wa Fumba (Fumba Town Development) uliopo Nyamanzi, wilaya ya Magharibi ‘B’, Unguja imekuwa na mahusiano ya karibu ya kikazi na klabu hiyo toka mwaka 2016 ambapo zimekuwa zikishirikiana katika mambo mbali mbali. Katika   mazungunzo yao, pande mbili hizo zimebadilishana mawazo na kukubaliana kuimarisha mahusiano na kushirikiana katika utekelezaji wa malengo na majukumu ya taasisi hizo hususani kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuwa na makaazi bora kama ilivyo katika sera na mipango yanserikali. Aidha Tobias aliipongeza ZPC kwa kuendelea kuwa karibu na kampuni y
  Mtoni Kidatu wahimizwa kulinda maeneo ya skuli NA MWANDISHI WETU MKUU wa Wilaya ya Magharibi ‘A’ Suzan Peter Kunambi, amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanalinda rasilimali ya ardhi ya elimu ili kuona hayavamiwi kiholela. Kauli hiyo aliitoa wakati akizugumza na wananchi wa Mtoni Kidatu alipokuwa akisikiliza changamoto zinazowakabili walimu wa skuli ya Mtoni Kidato.   Alisema kuna uvamizi mkubwa katika maeneo ya skuli zilizomo ndani ya wilaya yake kutokana na wananchi kujenga makaazi ya kudumu. “Sio skuli hii tu iliyovamiwa, skuli vinazovamiwa ni nyingi hivyo ni wajibu wa wananchi mliopo karibu na maeneo ya skuli mnapoanza ujenzi msikae kimpya kwani mipaka ya skuli inajulikana na kuwasisitiza walimu kuacha kuazima maeneo ya skuli,” alisisitiza. Alisema ni vyema kuwa walinzi wa maeneo hayo kwani bado yana shughuli kubwa kwani bado miundombinu ya elimu inahitajika kujengwa ya kisasa. Aidha alisema maeneo mengi yanavamiwa na pale serikali inapotaka kujenga majen