Posts

Showing posts from July, 2020
Image
ZPC, CPS zakubaliana kuimarisha uhusiano, mashirikiano NA MWANDISHI MAALUM KLABU ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) na kampuni ya CPS Lives zimekubaliana kuendelea kushirikiana ili kufanikisha malengo ya taasisi hizo. Makubaliano hayo yamefikiaa katika mazungumzo yaliyofa baina ya uongozi wa ZPC na kampuni hiyo inayojenga mji mpya wa Fumba (Fumba Town Development). Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume aliongoza ujumbe wa klabu yake ulipofanya ziara katika ofisi kampuni hiyo ziliopo ndani ya mji huo unaojengwa Nyamanzi, wilaya ya Magharibi "B'. Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume (alievaa kofia) akiongoza kikao cha majadiliano kati ya ZPC na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya CPS Live Tobias Dietzold. Akizungumzia ziara hiyo, Mfaume alieleza kuwa ililenga kubadilishana mawazo, kumagua maendeleo ya ujenzi wa mji huo na kuimarisha uhusiano. “Kwa muda wa miaka minne sasa ZPC na CPS tumekuwa na mahusiano ya kitaasisi yaliyolenga katika kuimarisha utendaji wa pande zote mbili
Image
  TAARIFA MAALUM KWA WANACHAMA WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR - ZPC NDUGU WANACHAMA, Kwa niaba ya Kamati Tendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar [ZPC] ninawajulisha kuwa Kamati ilikutana Julai 7, 2020 katika ofisi zake Kijangwani na kujadili mambo mbali mbali na kufikia maamuzi yafuatavyo:- 1.    Mkutano Mkuu wa Wanachama wa ZPC ufanyike Agosti 8, 2020 kama ilivyopendekezwa katika vikao vilivyotangulia. Kutokana na uamuzi huo, taarifa rasmi inatolewa kwa Wanachama kama inavyoelekezwa na katiba ya Klabu kifungu cha 16(d) kinachotaka taarifa ya Mkutano Mkuu wa ZPC itolewe mwezi mmoja kabla ya siku ya Mkutano. Agenda za Mkutano huo zitatangazwa baadae pamoja na taratibu za uchaguzi wa viongozi Klabu ambao ni moja ya agenda za Mkutano huo. 2.   Kamati Tendaji imeteua Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi itakayoratibu, kusimamia na kuendesha uchaguzi wa viongozi wa Klabu inayoundwa na Wajumbe kutoka asasi za kiraia. Majina ya Wajumbe wa Kamati hiyo yatatangazwa baada