Posts

Showing posts from December, 2020
Image
  Wanahabari endelezeni uzalendo, kuhamasisha amani – RC Kitwana NA ASYA HASSAN MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa, amesema vyombo vya habari vina wajibu mkubwa wa kuendelea kushajiisha jamii juu kuongeza mshikamano, kutunza amani na kuvumiliana. MKUU wa mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana akifungua semina hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa ZPC, Abdalla Mfaume . Ameeleza hayo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari zinazohamasisha amani, umoja, mshikamano na mtangamano wa kijamii baada ya uchaguzi yaliyofanyika Kidongo Chekundu, Zanzibar. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kwa kushirikiana na Shirika la Internews Tanzania, ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kukuza amani katika jamii. Waandishi wa habari wanachama wa ZPC wakiwa katika mafunzo ya uandishi wa kuhamasisha amani. Alisema amani, umoja na mshikamano ni muhimu katika nchi yoyote kwan
Image
  Soraga aitaka ZBS kuzingatia maslahi ya umma, kudhiti ubora NA MWAJUMA JUMA KAIMU Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Mudrik Ramadhan Soraga, (pichani) amewataka watendaji wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS), kuweka mbele maslahi ya nchi wanapofanya ukaguzi wa bidhaa na   kuacha mapatano na wafanyabiashara   kwa bidhaa zisizokuwa haina ubora. Akizungumza na watendaji wa taasisi hiyo iliyopo Amani viwanda vidogo vidogo alisema kuwa ZBS ni taasisi inayosimamia viwango na watendaji wake wanapaswa kuwa makini na kutambua kuwa wanapaswa kuwa mstari wa mbele kulinda afya za wananchi na mazingira. “Katika hali ya kawaida nchi ya kisiwa inakuwa kama chambo kwa kuingizwa kila kitu, ikiwa bidhaa zinaingizwa pasi na kufuata utaratibu matokeo yake utakuta bidhaa hatarishi kwa afya za watu zinazagaa mitaani,” alieleza. Soraga ambae pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uwekezaji na Uchumi, alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaingiza bidhaa ambazo hazina viwango hivy
Image
  Miaradi ya TASAF ikidhi viwango - Waziri NA MWANDISHI WETU MFUKO wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF), imetakiwa kuhakikisha ubora na viwango katika miradi ya jamii inayoanzishwa badala ya kufuata utashi wa viongozi wa kisiasa. (Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (katikati) akieleza jambo alipokutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar walipofika ofisini kwake kabla ya kukutana na waziri wa Wizara hiyo Dk. Khalid Salum Mohamed). WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratatibu na Baraza la Wawakilishi, Dk. Khalid Salum Mohamed, amesema uwekezaji wa TASAF katika miradi hasa ya ujenzi wa majengo ya jamii unapaswa kuzingatia viwango ili kuepusha hasara ya mali na maisha ya watu. Akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislauds Mwamanga na ujumbe wake uliofika ofisini kwa Dk. Khalid Vuga jijini Zanzibar, hivi karibuni alieleza kuna ulazima wa miradi inayofadhiliwa na TASAF kuhakikisha kwamba inafikiwa viwango na isiwe kuwafurahish
Image
  Tumejipanga kuzikabili changamoto za wakulima wa mwani - Waziri NA MWANDISHI WETU, PEMBA IMEELEZWA kuwa mashirikiano ya wadau mbali mbali na serikali yatachochea kasi ya kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wakulima wa mwani na zao hilo kwa ujumla. Akifungua mafunzo ya wakufunzi wa wakulima wa mwani katika ukumbi wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC), Wawi Pemba, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Dk. Soud Nahoda Hassan, alieleza kuwa kupitia dhana ya uchumi wa bluu zao hilo litaimarishwa ili kuongeza uzalishaji. Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Mliasili na Mifugo, Soud Nahoda Hassan akifungua mafunzo ya wakufunzi wa wakulima wa mwani. Alisema changamoto nyingi zinatokana na mabadiliko ya tabia nchi, zimeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za kilimo hicho lakini wataalamu wameendelea kufanya utafiti wa kuzikabili ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa mbegu zenye uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na maradhi. “Juhudi zote hizo zinafa
Image
  Vyama tisa vyapongeza CCM, ACT kuunda SUK NA MWANDISHI WETU VYAMA vya upinzani Zanzibar vimempongeza Rais wa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa hotuba aliyoitoa wakati wa hafla ya kumuapisha Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wakisema imeakisi dhamira yake ya kujenga Zanzibar mpya. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini ambae pia ni katibu wa umoja huo unaoundwa na vuyama tisa vya siasa, Ameir Hassan Ameir, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habar na kueleza kuwa kama kufanya hivyo pia ni kuitii katiba na sheria ya Zanziar. Alisema kitendo cha kumteua na kumuapisha kiongozi huyo wa chama cha ACT Wazalendo pia kunatimiza ahadi ya dk. Mwinyi aliyoitoa wakati wa kampeni na baada ya kuapishwa kuwa atashirikiana na vyama vya siasa ili kuunda serikali ya kitaifa itakayoleta maendeleo ya haraka kwa wananchi wake. “Kwa heshima zote Rais (Dk. Mwinyi) alimteuwa na kumuapisha Maalim Seif Sharif
Image
Waandishi watakiwa kutumia fursa kujiendeleza NA ASYA HASSAN WAANDISHI wa habari nchini wamesisitizwa kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa ili kuwajengea uwezo, uelewa, kujitangaza ili kuongeza ufanishi katika kazi zao na maendeleo ya taifa kwa ujumla. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari zanzibar (ZPC), Abdallah Abdulrahman Mfaume, alipokuwa akizungumza katika kikao cha pamoja cha wanachama na viongozi wa jumuiya hiyo kilichofanyika katika ofisi za klabu hiyo Kijangwani mjini Unguja. Baadhi ya wanachama wa ZPC waliofanya na kuwasilisha habari za kukuza uelewa juu ya maradhi ya mripuko wakiwa katika kikao maalum kilichofanyika katika ofisi za klabu hiyo Kijangwani, Zanzibar. Mfaume aliwasisitiza waandishi kutumia kalamu zao vizuri pamoja na kufuata sheria na maadili ya kazi zao ili kukuza ustawi wa jamii na kutunza amani iliyopo. Alisema uandishi wa habari ni kada inayotegemewa kuchochea mabadiliko na maendeleo katika jamii hivyo waandishi wanapaswa
Image
HAFLA YA KUMUAPISHA MAKAMU  WA KWANZA WA RAIS ILIYOFANYIKA DISEMBA 8, 2020  IKULU,  ZANZIBAR MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) akila kiapo cha uaminifu kwa katika na rais wa zanzbar mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.    RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, (kushoto) akimpongeza na kumkabidhi vitendea kazi Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamadi, baada ya kumuapisha kushika wadhifa huo. MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) akihutubia mara baada ya kula kiapo cha kushika wadhifa huo. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akihutubia waalikwa wakati wa hafla ya kumuapisha Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad. MAKAMu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla (kushito),wakibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, wakati wa hafla ya kuapi
Image
  Wadau wataka mjadala kuweka misingi ya amani NA MWAJUMA JUMA WADAU wa amani na uchaguzi nchini wameishauri na wadau wengine wa uchaguzi kuitisha mjadala wa pamoja utakaotoa suluhuhisho la hofu ya kuvunjika kwa amani kipindi cha uchaguzi. Wakizungumza katika mkutano  ulioitishwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), walisema pamoja na Zanzibar kuendelea kuwa na amani baada ya uchaguzi wa oktoba mwaka huu, ipo haja ya kutafutwa mbinu zitakazoondoa hofu ya kuondoka kwake kila ifikapo wakati wa uchaguzi. Mkurugenzi wa Jumuiya ya Vijana na Maendeleo Zanzibar (ZAFAYCO), Abdallah Abeid, alieleza kuwa ili kuimarisha misingi ya amani iliyopo, kuna haja ya wadau kushirikiana na serikali kutafuta kiini cha hofu ya kuvunjia amani kila inapokaribia kipindi hicho. “Imezoeleka kila inapotokea uchaguzi, hofu juu ya kuvunjika kwa amani inaongezeka hivyi ipo haja ya kutafuta chanzo cha hiyo hofu na kuiondoa,” alisema Abeid. Nae Maryam Chum alieleza kuwa kuna umuhi kwa jamii kuele
Image
  Bodi yatakiwa kutokuwa chanzo cha migogoro NA MWANDISHI WETU WAJUMBE wa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi Zanzibar, wametakiwa kutokuwa chanzo cha migogoro ya ardhi na badala yake kuwa watatuzi wa migogoro hiyo kuwa mujibu wa sheria zilizopo. Akizungumza na Wajumbe bodi hiyo ofisini kwao Forodhani, Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Riziki Pembe Juma, amesema kufanya hivyo kutasaidia kuondoa migogoro ambayo inaongezeka siku hadi siku. Amesema miongoni mwa sheria zinazofanyiwa kazi imebainisha kila kitu ili kuhakikisha haki zinapatikana kwa wahusika wakiwemo wananchi wa hali ya chini, hivyo si vyema kufanya kazi kwa utashi wao binafsi. “Sheria zilizopo zinaelekeza mambo yote yanayotakiwa na yasiyotakiwa kufanyiwa kazi, hivyo sio vyema kufanya kazi kwa utashi binafsi badala yake mfanye kazi kwa mujibu wa sheria zilizopo na sio kuwakandamiza wananchi ambao sisi ndio wanaotutegemea,” amesema Pembe. Ameongeza kuwa ipo haja ya kukaa pamoja kati ya wajumbe wa bodi hiyo na
 https://youtu.be/kWQIDmIAFkQ
Image
WADAU  WATAKA KONGAMANO  KUONDOA HOFU KUTOWEKA KWA AMANI Katika kutekeleza mradi wa kuimarisha amani, uvumivu wa kisiasa na utamaduni wa kupokea tofauti za maoni (peace, tolerance and differences on opinion) unaofadhiliwa na shirika la Internews, Jumatatu Novemba 30, 2020 Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) iliandaa mkutano wa wadau wa amani na uchaguzi uliojadili juu ya namna ya kuendeleza amani baada ya uchaguzi na kufikia maazimio kwamba wadau wote wanapaswa kushirikiana kutafuta suluhu itakayoondoa hofu ya kupotea kwa amani hasa katika kipindi cha uchaguzi. Mwenyekiti wa ZPC Abdalla Mfaume (alieipa mgongo kamera) akiongoza mkutano wa wadau wa amani uliofanyioka katika ukumbi wa kitengo cha uzazi shirikishi Kidongo Chekundu Novemba 30, 2020. Mchungaji wa kanisa Anglican Zanzibar, Father Philip Munguti akichangia mada katika mkutano wa wadau wa amani uliojadili namna ya kuimarisha amani, uvumilivu wa kisiasa na utamaduni wa kupokea maoni tofauti. Mjumbe wa Chama cha Wanahabar