Posts

Showing posts from April, 2021
Image
Ushirikiano wa vioingozi, wananchi kuimarisha maridhiano NA MWANDISHI WETU WANANCHI wa mkoa wa Kaskazini Unguja, wameeleza kuwa ushirikiano uliopo kati ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar umeimarisha maelewano baina ya wananchi hivyo ipo haja ya kuendelezwa. Wakizungumza na mwandishi nwa habari hizi hivi karibuni, walieleza kuwa hali hiyo inatokana na kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) inayohusisha vyama vya CCM na ACT Wazalendo baada ya uchaguzi mkuu wa oktoba 28 mwaka uliopita. Mkaazi wa shehia ya Bumbwini Mafufuni, Haji Nyange Makame, alieleza kuwa hali hiyo imeongeza kuaminiana miongoni mwa viongozi na wananchi katika shehia yao. “Kabla ya uchaguzi, ilikuwa vigumu kumuona viongozi wa CCM na vyama vyengine wakakaa pamoja katika kazi za kisiasa au kijamii lakini siku hizi huwezi kumjua nani CCM nani ACT kama mgeni nao,” alieleza Nyange. Nae Mwanaacha Hamid Said wa Kilimani Tazari, alieleza kuwa hali ya ushirikianbo imeongezeka na kupongeza utamaduni ulioan
Image
 MAADHIMISHO YA MIAKA 57 YA MUUNGANO Watanzania watakiwa kuulinda, kuutunza, kuuenzi  Makamu wa Rais asema ni tunu na urithi wa taifa NA MWANDISHI WETU, DODOMA IMEELEZWA kuwa Watanzania wana kila sabau ya kuulinda, kuuenzi na kuutunza muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar kwa kuwa ni tunu na urithi wa taifa. Muuungano huo uliotimiza miaka 57 toka ulipoasisiwa Aprili 26, 1964, unatajwa kuwa ni miongoni mwa mambo yaliyoimarisha amani, utulivu na mshikamano miongoni mwa watanzania wa Tanzania bara na Visiwani. Akilifungua kongamano la maadhimisho hayo katika ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Isdor Mpango a lieleza kuwa katika kuimarisha Muungano huo, Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zitahakikisha inamaza changamoto 10 zilizobakia baada ya kufanikiwa kutatua changamoto 15 zilizokuwa zinaukabili muungano huo. Dk. Mpango alisema kuwa serikali mbili hizo zimek
Image
UZINDUZI WA MPANGO WA UWEZESHAJI MADEREVA BODABODA, BAJAJI ULIOFANYIKA KATIKA HOTELI YA UBUNGO PLAZA DAR ES SALAM Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati Benki ya NMB,  Filbert Mponzi, akitoa maelezo juu ya mpango wa uwezeshaji madereva bodaboda na bajaji wakati wa uzinduzi wa mpango huo hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Ubungo Plaza, Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB,  Ruth Zaipuna (kushoto). Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati Benki ya Nmb, Filbert Mponzi. Waziri Jenista Mhagama (katikati) akizungusha bango kuashiria uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji wa mikopo kwa madereva Bajaji na Bodaboda ijulikanayo kwa  ' NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO'.  Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB,  Ruth Zaipuna (wa pili kutoka kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Madereva B
Image
  Wazazi wasiozingatia elimu za watoto wao kukiona NA MWANDISHI WETU MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadidi Rashid, (pichani) amewaagiza masheha wa mkoa huo, kuzidisha mashirikiano na kutoa taarifa za wazazi wasioshughulikia maendeleo ya elimu ya watoto wao. Alieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha kiwango cha ufaulu mkoani humo ambacho kwa muda mrefu kipo chini. Hadidi alitoa agizo hilo skuli ya Ukongoroni wakati akizungumza na wazazi, walezi, walimu na wanafunzi wa skuli hiyo. Alisema imebainika kuwa baadhi ya wazazi wanapuuza upatikanaji wa elimu kwa watoto wao kwa kushirikisha na masuala ya ukataji kuni, kujiingiza katika ajira za watoto ikiwemo za kupara samaki na kupelekea watoto hao kushindwa kuhudhuria skuli kwa wakati, kuwa watoro na kutodurusu masomo yao. Alifahamisha kuwa kutokana na hali hiyo inayofanywa na baadhi ya wazazi kunachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma juhudi za serikali juu ya mikakati iliyojiwekea. Hivyo aliwataka masheha hao kuwa
Image
Udhibiti wa migogoro utaimarisha amani, utulivu NA ASYA HASSAN IMEELEZWA kuwa utashi wa kisiasa na mafunzo ya mara kwa mara juu ya udhibiti wa migogoro utasaidia kuimarisha amani na utulivu nchini. Meneja wa shirika la Search for Common Ground, Hussein Faraji Sengu, alieleza hayo hivi karibuni katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, ofisiani kwake kijangwani, Zanzibar. Sengu alieleza kuwa iwapo makundi mbali mbali ya jamii yatajengewa uwezo, kuna uwezekano wa hali ya amani kuimarika na kuepuka mizozo. Alieleza kuwa ipo mizozo inayoweza kuepukwa kwa wahusika kutambua haki na mipaka yao, hivyo kupitia mradi wa ‘Dumisha amani Zanzibar’, watakutana na makundi mbali mbali wakiwemo wanasiasa ili kuwajengea uwezo wa kutambua vichocheo vinavyoweza kuvuruga amani na utulivu. “Tunaamini hatua hii itawafanya wanasiasa kujitambua na kuwasimamia vyema wanachama wao ili kuepuka migogoro inayotokezea baina yao kabla ya kuwa chanzo cha vurugu,” alieleza Sengu. Alisema mfumo wa vyam
Image
  Sakata la kupigwa mwandishi Z'bar: SMZ yaahidi kuchukua hatua kwa waliohusika Wadau wasema ni mwanzo mzuri, waahidi kuendelea kufanya kazi nayo NAMWANDISHI WETU SIKU moja baada ya kutokea tukio la udhalilishaji wa mwanahabari Jesse Mikofu wa gazeti la Mwananchi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imeahidi kuwachukulia hatua askari wanne wa Kikosi cha Valantia Zanzibar (KVZ) wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo. Jesse alishambuliwa na askari hao waliokuwa wakiwaondoa wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) katika eneo la  Darajani, mjini Unguja, akiwa anatekeleza majukumu yake ya uandishi wa habari. Akizungumza mkutano wa pamoja wa Waandishi wa habari, ulioitishwa kwa pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tabia Maulid Mwita na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Ali Mohammed, kwa ajili ya kutoa tamko la serikali, uliofanyika  katika ofisi za Wizara ya Habari, Migombani.   Masoud, alisema s
Image
  SUK tunda la maridhiano linalopaswa kuenziwa • Vyombo habari, NGOs zatajwa kuchangia uimara wake NA ASYA HASSAN KUWEPO kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ya Zanzibar inayoundwa na vyama vya CCM na ACT Wazalendo, kunatajwa kuwa ni matokeo ya maridhiano ya kisiasa yaliyolenga kutatua mgogoro wa kisiasa wa muda mrefu ulioikumba Zanzibar. Mgogoro huo unatajwa kusababisha mifarakano ya kijamii na kuzorotesha maendeleo ya kijamii sambamba na kudhoofisha maswala ya amani na utulivu hasa baada ya kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania. Mfumo huo uliorudishwa mwaka 1992, ulianza kuonesha dalili za misuguano na mifarakano katika jamii hata kabla ya uchaguzi wa kwanza wa mwaka 1995 ambao ulikuwa na ushindani mkali kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF). Yapo mambo mengi yaliyoashiria uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi huo na hata katika chaguzi nyengi zilizofuata kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambao ndipo chimbuko la maridhiano ya kisiasa Zanzibar lilit
Image
Mbunge Welezo akemea udhalilisahaji watu wenye ulemavu NA MWANDISHI WETU WAZAZI na walezi wenye watoto wenye ulemavu, wameombwa kutowaficha kwani kufanya hivyo ni sehemu ya udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za binadamu. Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Welezo, Unguja katika hafla ya kukabidhi viti mwendo (wheel chair) kwa watu wenye ulemavu wa jimbo hilo iliyofanyika katika tawi la CCM Mwendapole, shehia ya Welezo wilaya ya Magharibi ‘A’. Alieleza kuwa kushirikishwa kwa watu wenye mahitaji maalum katika shuguli za kijamii ni miongoni mwa haki za binadamu hivyo ipo haja ya elimu iendelee kutolewa. “Watu wenye ulemavu na wenye mahitaji maalum ni sehemu ya jamii, hivyo tuwatoeni na kuwapeleka skuli ili kupata elimu lakini pia tuwashirikishe katika mambo mengine ya kijamii,” alisema Maulid. Aidha aliwapongeza wananchi wa jimbo hilo kwa mashirikiano wanayoyatoa kwa viongozi wa jimbo hilo jambo linalopelekea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa ufanisi. “Tuendelee kush
Image
  Dk. Mwinyi ahimiza upendo, kuhurumiana NA MWANDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kuhurumiana ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wanyonge wakiwemo wajane, mayatima na mafakiri. Alhaj Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo wakati alipokuwa akiwasalimia Waumini wa dini ya Kiislamu huko katika Masjid Tawba maarufu Jongeyani uliopo Malindi kwa Tausi, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi mara baada ya kumaliza Sala ya Ijumaa. Katika salamu zake hizo, Alhaj Dk. Mwinyi alisema kwamba kila mmoja kwa nafasi yake ni vyema akaona haja ya kuyasaidia makundi hayo katika jamii ili na wao waweze kuitekeleza ibada ya funga ya Ramadhani ipasavyo. Alhaj Dk. Mwinyi alitoa wito kwa wafanyabiashara wote kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kuhurumiana hivyo, mfanyabiashara anatakiwa kupata faida ya kiasi na sio kupata faida mara mbili kwani hilo si jambo la busara. Kutokana na hilo, Rais Dk.
Image
  Dk. Mwinyi ahimiza tahfifu ya bei za futari, bidhaa Ramadhani R AJAB MKASABA, IKULU ZANZIBAR SERIKALI imeahidi kuchukua hatua kali kwa mfanyabiashara yoyote atakaebainika kupandisha bei za bidhaa au huduma kwa utashi ama tamaa bila ya kuwepo sababu ya msingi kwani tayari imeshatoa bei elekezi za bidhaa muhimu za chakula. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema hayo leo katika risala yake aliyoitoa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ya kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa mwaka 2021 sawa na mwaka 1442 Hijria. Alhaj Dk. Mwinyi alieleza kwamba ni vyema wananchi wenye kipato cha chini wakafikiriwa hasa katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo mahitaji ya familia yanaongezeka. Alisisitiza kwamba kwa msingi huo huo, wafanyabiashara wa bidhaa zote zikiwemo za nguo ni vyema wakazingatia uwezo wa wananchi kwani kuwakatia nguo watoto katika kipindi hichi kwa ajili ya Sikukuu ni sehemu ya utamaduni wa wananchi wote wa Zanz
Image
Wanahabari wahimizwa ‘kuilea’ SUK NA MWAJUMA JUMA MKURUGENZI wa Chama Cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) ofisi ya Zanzibar, Dk. Mzuri Issa amesema kunahitajika nguvu ya pamoja ili kuimarisha maridhiano ya kisiasa yaliyoasisi Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar. Akizungumza katika mafunzo ya Waandishi wa habari juu ya umuhimu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alisema waandishi wa habari wanapaswa kuchukua jukumu lao na kuhakikisha lengo la kuanzishwa kwake linafanikiwa. Alisema kwenye taifa, ustawi na umoja wa wananchi ni nguvu kubwa katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana. Hivyo alieleza kuwa waandishi wa habari wana wajibu wa kuacha ushabiki wa siasa bali wajuwe kwamba wao ndio wanaopaswa kupaza sauti zao ili jamii izidi kujenga matumaini na serikali hiyo. Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo, Mkufunzi wa Waandishi kutoka Internews, Ali Haji Mwadini, alisema pamoja na waandishi kufanya kazi katika mazingira magumu, bado wanajukumu la kuifahamisha j
Image
Ayoub ahimiza upatikanaji wa habari sahihi NA MWAJUMA JUMA MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud, ameeleza kuwa upatikanaji kwa habari sahihi na kwa wakati ni jambo la lazima hivyo wanahabari wanapaswa kwenda na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano. Ayuob aliyasema hayo alipokutana na wajumbe wa Kamati Tendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), waliyofika ofisini kwake kujitambulisha huko ofsini kwake Mkokotoni mkoani humo. Alisema kutokana na mabadiliko ya teknolojia, jamii imekuwa ikipata habari nyingi ambazo baadhi yao sio sahihi na kupelekea athari kwa jamii na ikiwemo migogoro na machafuko ya kijamii. “Kwa tulipofikia, swala la kupatikana kwa habari sahihi ni jambo la lazima kwani zinapokosekana habari sahihi hutolewa sizizo sahihi na zinapoifikia jamii athari yake inakuwa kubwa na tunaweza kupelekea nchi ikaingia kwenye migogoro ikiwemo ya kivita”, alisema. Hivyo alisema uwepo wa Klabu ya Waandishi wa Habari ni faraja kw