Posts

Showing posts from June, 2021
Image
Simai awataka walimu kutumia huduma za kibenki kujindeleza NA HAROUB HUSSEIN WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya AmaliZanzibar, Simai Mohammed Said, amewataka walimu kuzitumia fursa zinazopatikana katika benki ya NMB ili kurahisisha upatikanaji wa mahitaji yao kwa maendeleo ya haraka. Simai aliyaeleza hayo wakati akifungua semina ya Siku ya Walimu na NMB iliyofanyika katika ukumbi wa Michenzani Mall jijini Zanzibar. Alisema benki ya NMB ina fursa mbali mbali zinazosaidia wafanyakazi katika mahitaji yao ya kila siku hivyo ni vyema walimu wakazitumia fursa hizo kujipatia maendeleo ya haraka. Aidha alisema katika kujali watumishi wa wizara hiyo benki hiyo imeamua kuweka siku maalum ya walimu ikiamini walimu ndio msingi mkuu wa maendeleo katika sekta zote. “Benki hii imeonesha kujali watumishi wetu kwa kuweka siku maalum ya walimu hivyo nakuombeni muwe karibu nayo kwa kuzitumia fursa na huduma zinazopatikana katika benki ya NMB,” alisema Waziri Simai. Alisema katika kurahisisha hudum
Image
Serikali itawapa kipaumbele wajasiriamali wanawake  NA MWANDISHI MAALUM, OMKR Mke wa Makamu wa Kwanza Wa Rais wa Zanzibar,   Zuhra Kassim Ali, (wa pili kushoto), amesema serikali imejipanga kuwahudumia wananchi wote na hasa wajasiriamali wanawake, kwa kutatua kero zao kwa haraka ili kuendelea kuweka mazingira bora ya kutekeleza shughuli zao za kiuchumi.   Zuhra ameyasema hayo katika mahafali ya mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake yaliyoendeshwa kwa njia ya mtandao yaliyofanyika katika ukumbi wa wakfu ya Wangazija Forodhani Jitini, ambayo yalioandaliwa na Taasisi ya Wanawake Wajasiriamali (AWE) kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani. "Serikali inaendelea kusimamia jambo hili kwa karibu ili kuhakikisha wajasiriamali wote wanapata mazingira mazuri kwa ajili ya kufanya shughuli zao za ujasiriamali," alieleza Zuhra. Hivyo Zuhra aliwataka Wanawake hao kuitumia vyema fursa na elimu waliyoipata katika mafunzo hayo ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiuchumi. "Nawao
Image
Wanachama Yanga SC wakubali mabadiliko NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAM WANACHAMA wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es salam wamekubali rasmi kuingia katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji na mabadiliko ya katiba kwenye mkutano mkuu uliofanyika Juni 27, mwaka huu. Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla akiongoza mkutano huo, aliwauliza wanachama kuhusu kuafiki mabadiliko hayo mara baada ya kutambulisha kamati iliyosimamia mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji. Wajumbe 1,170 ambao walijiandikisha katika Mkutano Mkuu uliofanyika katika ukumbi wa DYCC, jijini Dar es Salaam walipitisha mabailiko hayo kwa kura za ndio. Baada ya Dk. Msolla kuwauliza wanachama wanaoafiki mabadiliko hayo na ukumbi mzima ukanyoosha mikono akiwamo, Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi huku baadhi yao wakipiga kelele kuwa wote wanaafiki. Baada ya hatua hiyo, Dk. Msolla aliwakabidhi vyeti wajumbe wa kamati hiyo na kisha akarejea tena kwa wanachama kuwauliza wa
Image
Miradi 93 yasajiliwa siku 100 za Samia NA MWANDISHI MAALUM, OWM WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha siku 100 za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imesajili miradi 93 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.6 itakayozalisha ajira 24,600. Alisema kuwa hatua hiyo inatoa alama kwa wawekezaji wa nje kwamba kwa sasa urasimu katika sekta ya uwekezaji unaendelea kupunguzwa katika maeneo ya usajili wa makampuni pindi muwekezaji anapokusudia kuja kuwekeza nchini. Waziri Mkuu aliyasema hayo Juni 27,2021 alipofungua kongamano la siku 100 za Rais Samia lililofanyika katika kituo cha mikutano ya Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Alisema mbali na miradi hiyo, pia serikali ya Rais Samia amefanya jitihada kubwa ya kuondoa tozo 232 zilizokuwa zinawakwaza wafanyabishara ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao nchini. “…Na haya yote ni katika kuongeza mzunguko wa fedha kwa Watanzania ambao wanashiriki katika
Madiwani watakiwa kuchochea matumizi baraza watumiaji nishati NA MWANAJUMA MMANGA MADIWANI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wametakiwa kuwahamasisha wananchi kulitumia Baraza la Watumiaji wa Huduma za maji na nishati ( CRC)  kueleza matatizo yanayowakabili katika vijiji vyao kupitia sekta hizo. Akitoa mafunzo kwa madiwani hao, Katibu Mtendaji baraza hilo, Hadia Abdulrahman Othman huko Mkokotoni, ali sema lengo la serikali kuunda baraza hilo ni kulinda na kusimamia maslahi ya watumiaji kwa kuhakikisha matatizo yanayowakabili katika sekta za maji, umeme, mafuta na gesi yanapatiwa ufumbuzi.  Aliwataka madiwani  hao kuzingatia taratibu zote za kisheria za uungaji na matumizi sahihi ya  huduma za maji na nishati ili ziwe endelevu na salama kwa wananchi. “Niwaombe sana Madiwani kuhakikisha uungaji wa maji na nishati ya umeme unakuwa kwa mujibu wa sheria na akanuni zilizoekwa na serikali ili kuepusha kupotea kwa mapato ya seriakli sambamba na kuepusha malalamiko yanayojitokeza,” alieleza
Image
Waandishi watakiwa kuelimisha jamii chanjo ya kipindupindu NA KHADIJA KHAMIS, MAELEZO   WAANDISHI wa Habari Zanzibar wametakiwa kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na chanjo ya Kipindupindu ili kujenga uelewa juu ya umuhimu wa chanjo hiyo.   Akifungua mafunzo kwa  waandishi wa habari kuhusu chanjo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar, Dkt. Abdallah Ali Suleiman (pichani), amesema  lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na  dhana potofu zinazotokana na chanjo hiyo   Amesema chanjo hiyo haina madhara kwa binadamu na inatolewa kwa ajili ya kuikinga jamii na maradhi ya mripuko hivyo ameitaka kuondoa shaka hiyo.   Ameeleza kuwa chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa kwa mwezi ujao katika shehia mbali mbali za Unguja na Pemba kwa maeneo ambayo huathirika sana kila unapotokea mripuko wa maradhi hayo.   Nae Afisa Afya ya Jamii, Fauza Mohamed Abdulkadir, amesema chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa kwa watu wen
Image
Watakiwa kuzingatia viwango kwenye kazi za ubunifu, utamaduni NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaaban, amesema serikali kupitia wizara yake inaunga mkono ushiriki wa mashindano yaliyoanzishwa na taasisi ya viwango Zanzibar (ZBS) kwani yataiwezesha Zanzibar kuwa kwenye ramani ya ulimwengu wa viwango. Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi wa shindano la insha inayohusu mchango wa Viwango, Sanaa, Utamaduni na Urithi Jamii katika kukuza uchumi bunifu barani Afrika iliyoandaliwa na shirika la viwango Afrika (ARSO), hafla iliyofanyika katika jengo la ZURA, Maisara Zanzibar. Alisema inaposhiriki katika mashindano na shughuli za mashirika ya kimataifa na kikanda, kwa asilimia kubwa inaweza kufanya vizuri na kuaminiwa hivyo ni imani yake kwamba ZBS itaendelea kuwa wadau wakubwa wa shirikisho hilo la Afrika. Akizungumzia maudhui ya mada ya mashindano hayo, Shaaban alisema, sanaa na ubunifu vina mchango mkubwa katika
Image
SMZ yaipongeza WB kudhamini miradi NA MWINYIMVUA NZUKWI WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali, ameipongeza Benki ya Dunia (WB) kwa misaada na mikopo inayoipatia Zanzibar kwani imechangia kuimarisha ustawi na maendeleo ya jamii. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo kanda ya Afrika, Dk. Taufila Nyamadzabo, ofisini kwake Vuga, alieleza kuwa miradi mbali mbali iliyoidhinishwa na benki hiyo hivi karibuni itachochea kasi ya maendeleo ya Zanzibar na watu wake. Alieleza kwamba ili kufikia malengo iliyojiwekea, Zanzibar inapaswa kutumia kikamilifu fursa zinazotolewa na washirika wa maendeleo jambo ambalo alimuahidi mkurugenzi huyo kulisimamia kikamilifu. “Miradi iliyoidhinishwa na Benki ya Dunia ina sura mbili, yaani msaada na mikopo nafuu, hivyo ili tufanikiwe lazima tuwe na usimamizi bora ili tija ipatikane,” alieleza Jamal. Akiitaja miradi iliyoidhinishwa na WB ambayo ilikuwa ni sehemu ya mazungum
Image
  Bodaboda zaongeza ajali barabarani Z'bar NA MADINA ISSA KAMISHNA wa Polisi Zanzibar, (CP) Mohammed Haji Hassan (pichani) amesema ajali za barabarani zinazohusisha pikipiki za biashara (bodaboda) zimeongezeka katika kipindi cha mwezi Januari hadi Mei mwaka huu. Ameeleza kuwa hali hiyo imesababisha majeruhi na vifo kutokana na waendesha bodaboda wengi kutofuata sheria na kanuni za usalama barabarani. Akizungumza katika mkutano na waendesha bodaboda wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali ya Unguja huko katika kiwanja cha Kijangwani Mjini Unguja Kamishna huyo alieleza hali hiyo haipaswi kuachwa. Alisema lengo la mkutano na wafanyabiashara hao ni kujadili namna ya kupunguza ajali za barabarani na kuepusha vitendo vya kihalifu ambapo kwa sasa vimeshika kasi. Alisema katika kipindi hicho jumla ya ajali 93 zimetokea kati ya hizo ajali 34 zimesababishwa na usafiri wa bodaboda huku vifo vilikuwa 41 ambapa kati ya hivyo vilivyosababishwa na bodaboda ni 25. Akizungumza idadi
SMZ yavutiwa na nia ya BOSCH kuwekeza Z'bar NA MWINYIMVUA NZUKWI SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imeeleza utayari wake kushirikiana na kampuni ya BOSCH Groups ya Ujerumani kuwekeza katika nyanja mbali mbali za uchumi nchini. Wakizungumza kando ya mkutano wa utambulisho na Rais wa kampuni hiyo kanda ya Afrika, Dk. Markus Thill, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaban, walieleza kuwa serikali ipo tayari kuisaidia kampuni hiyo kufikia malengo. Walieleza kwamba, ili kuimarisha kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya uwekezaji nchini, serikali imeona vyema kuweka mazingira yatakayohamasisha uwekezaji. "Ujio wa BOSCH nchini utavutia wawekezaji wengine kufikiria kuja na kuwekeza nchini wakiamini kwamba watapata huduma stahiki kutokana na uzoefu wake katika uwekezaji ndani na nje ya Afrika," alieleza Soraga. Aliongeza kuwa mbali ya kutenga maeneo maalum ya uw
Image
Hemed aongoza mazishi marehemu ajali ya basi Shinyanga NA KASSIM ABDI, OMPR Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amewaongoza waaumini na wananchi wa Zanzibar katika mazishi Wahda Yussuf, mmoja ya marehemu aliyefariki katika ajali ya basi iliyotokea mkoani Shinyanga usiku wa kumakia Juni 2, mwaka huu. Hemed alieambatana na viongozi pamoja na watendaji wa serikali, walishiriki katika sala ya maiti iliyosaliwa Masjid Fatma, Kwahani ambapo maziko ya Wahida yalifanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe, wilaya ya Magharibi ‘B’, Unguja. Makamu wa Pili wa Rais ambae juzi usiku alikuwa miongoni mwa viongozi na wananchi waliopokea miili ya marehemu hao katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, alifanya hivyo kutekeleza ahadi ya serikali iliytoitoa katika Baraza la Wawakilishishi kwamba itasimamia na kugharamia mazishi ya marehemu hao. Pamoja na wahida, marehemu wengine waliozikwa jana katika maeneo mbali mbali ya Unguja ni Rehema Haji Juma, aliye
Image
Tuwafunzwe watoto wetu kuyapenda, kuyatunza mazingira - DC Msaraka NA SALUM VUAI MKUU wa Wilaya ya Mjini, Rashid Simai Msaraka, jana alizindua wiki ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, huku akiihimiza jamii kuwajengea watoto mapenzi na muamko wa kupanda na kutunza miti. Maadhimisho ya siku hiyo yanayofikia kilele chake tarehe 5 Juni, yanafanyika kwa harakati mbalimbali zinazohusisha uhifadhi wa mazingira ya nchi kavu na baharini. Katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye bustani ya Botanic iliyopo Migombani Wilaya ya Mjini, Msaraka aliongoza wananchi mbalimbali na wadau wa mazingira, katika shughuli ya kupanda miti kwa lengo la kulistawisha eneo hilo. Akizungumza na wananchi wakiwemo wanafunzi wa skuli ya msingi Migombani, Mkuu huyo wa Wilaya alisema ni muhimu wazazi na walezi kuwarithisha watoto utamaduni wa kuyapenda mazingira kwa kujumuika nao katika upandaji miti mbalimbali ikiwemo ya matunda na kivuli. Alisema miti ni rasilimali inayopaswa kuendelezwa kutokana na
Image
  Wizara ya habari kuwaendeleza watendaji wake  Yapongeza utendaji wa vyombo vya habari MWANDISHI WETU WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imeeleza kuwa mwaka wa fedha 2021/2022, itaimarisha mazingira ya utendaji kazi kwa wafanyakazi wake ikiwemo utoaji wa vitendea kazi na stahiki zao kwa mujibu wa sheria. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa wizara hiyo, Tabia Maulid Mwita (pichani), wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi katika Baraza la Wawakilishi Chukwani, Juni 2, 2021. Alisema mpango huo utaenda sambamba na kuwaendeleza wafanyakazi hao kwa kuwapatia mafunzo ili kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa lengo la kuongeza ufanisi na bidii ya kazi. Aidha alisema wizara katika mwaka huo pia imejipangia maeneo muhimu ya utekelezaji, ikiwemo kuimarisha miundombinu ya habari kwa ajili ya uzalishaji wa vipindi, ununuzi wa maudhui, ufatiliaji wa habari, ununuz wa mitambo ya uchapaji. Waziri Tabia alieleza kuwa kipaumbele chengine ilichojiw
Image
Wananchi Kaskazini Unguja wapongeza GNU NA KHAMISUU ABDALLAH WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wamepongeza hatua ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi kutekeleza katiba na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) iliyoimarisha umoja wa Wazanzibari. Wananchi hao walitoa pongezi hizo katika mkutano ulioandaliwa na Rais Mwinyi kwa ajili ya kuwashukuru kwa kumchagua kwa asilimia 100 ya kura katika uchaguzi uliofanyika 2020 katika ukumbi wa Ofisi ya chama hicho Mkoa wa Kaskazini Unguja Mahonda. Walisema katika miaka ya nyuma hasa mkoa huo uliweka matabaka baina ya vyama na vyama mtu na mtu jambo ambalo lilikuwa halileti taswira njema hasa kwa dini ya kislaamu. Aidha walisema kitendo alichokifanya Rais kimeonesha imani kubwa kwa wananchi wa Zanzibar katika kuona wanakuwa wamoja kwani hakuna jambo jema kama kuwaunganisha watu waliogombana. “Watu wa Kaskazini tunakupongeza kwa dhati kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwani hivi sasa s