Posts

Showing posts from August, 2023

Dk. Mwinyi aeleza dhamira CCM kufanya vikao vikuu Z'bar

Image
NA MWANDISHI WETU MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuwa chama hicho kitafanya mkutano mkuu wake taifa ndani ya visiwa vya Zanzibar ilimkutoa fursa kwa wajumbe kushuhudia maendeleo yaliyopatikana. MAKAMU Mwenyekit wa CCM Zanzibar, Dk. Hussein  Ali Mwinyi, akisalimiana na mmoja ya wenyeviti wa CCM wa mikoa waliofika ikulu kumsalimia. Dk. Mwinyi ambaye pia ni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyasema hayo Ikulu Zanzibar alipokua akizungumza na Wenyeviti wa mikoa wa chama hicho kutoka mikoa yote ya Tanzania waliofika kumsalimia. Alisema CCM Zanzibar, itahakikisha inalifanikisha azma hiyo na kuwezesha uptikanaji wa rasilimali zote ikiwemo eneo muafaka la kuhudumia wajumbe wote wa mkutano huo na mikutano mengine ya Halmashauri Kuu taifa ikiwa ni pamoja na kujenga ukumbi mkubwa wa mikutano. Alieleza kuwa uwepo wa ukumbi huo utaiwezesha nchi nzima kuwa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya cham

Samia: Tutaendelea kushirikisha wadau kuwaletea maendeleo

Image
NA MADINA ISSA RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema ataendelea kushirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo benki ya CRDB ambayo imekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali. Akizungumza mara baaada ya kuweka jiwe na msingi soko la jamii la wajasiriamali kilichojengwa na Benki ya CRDB, alisema, benki hiyo imekuwa ikiisaidia serikali ambapo kwa mwaka jana wajasiriamali hao walitoa kilio hicho ambacho CRDB imelichukua hilo. Alisema benki hiyo mara nyingi imekuwa ikiwashika mkono kuona maendeleo ya kusini yaliyoahidiwa yanatimia kwa wakati ambapo ndio lengo la tamasha hilo kupeleka maendeleo katika wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla. Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari mbili kwa uongozi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Dk. Samia, alisema serikali imeamua kujenga vituo hivyo na kupeleka gari hizo na kuwasisitiza uongozi wa jeshi kuzitumia kwa lengo la kusaidia kurahisisha utendaji kazi zao katika suala zima la ulinzi wa raia na mali zao. Alisema, kupat

Hifadhi ya Kitulo yatangazwa kuvutia watalii, wawekezaji

Image
NA MWANDISHI WETU SERIKALI imeendelea kujizatiti kwa   kuitangaza   hifadhi ya Taifa ya Kitulo   ndani na nje ya nchi lengo likiwa ni kuwavutia watalii na wawekezaji kutoka sehemu mbali mbali duniani. Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (pichani), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga aliyetaka kujua mkakati wa serikali wa kuitangaza hifadhi hiyo. Amefafanua kuwa hifadhi hiyo imekuwa ikitangazwa katika matamasha ya Karibu Kusini, Kilifair na Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba na Nanenane na kwa njia ya kidigitali, mitandao ya kijamii, majarida na Safari Channel. Kufuatia hatua hiyo amesema serikali imeanza kuimarisha   miundombinu ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo kufanya ujenzi wa nyumba tatu za malazi ya watalii na pia inatarajia   na kujenga nyumba mbili   na kambi moja   ya kuweka hema katika mwaka huu wa fedha 2023/2024, pamoja na   kukarabati miundombinu ya barabara. Kuhusu utatuzi wa migogoro ya mi

ABSA kuendelea kuchangia kampeni uzazi salama Z'bar

Image
  NA MWANDISHI WETU BENKI ya ABSA Tanzania imeeleza kuwa itaendelea kushirikian na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kustawisha afya za wananchi wa Zanzibar kupitia kampeni na programu mbali mbali. Akizungumza baada ya matembezi ya hiyari na mbio fupi za marathoni (Wogging) zilizoandaliwa na shirika la AMREF Tanzania kwa lengo la kusaidia jamii kupitia sekta ya afya, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Obedi Laiser, alisema wameamua kudhamini tukio hilo kwa kutambua juhudi zinazochukuliwa na serikali kuiimarisha sekta hiyo. “Sisi kama benki tunatambua mchango mkubwa mashirika binafsi kama AMREF mnafanya katika kuleta mabadiliko katika jamii na ndio dhumuni kuu kwetu kutamani kushiriki na kuunga jitihada hizi za kuleta mabadiliko katika afya ya uzazi wa mama na mtoto”, alieleza Mkurugenzi huyo. Aliongeza kuwa dhumuni ya benki hiyo kushiriki kwenye tukio hilo ni kuchangia na utatuzi wa changamoto na vikwazo ambavyo wanawake wajawazito mara nyingi hukumbana nazo wakati wa kujifung

Dk. Mwinyi aipongeza Amref misaada sekta ya afya

Image
NA MWANDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amelipongeza shirika la AMREF Afrika Tanzania kwa kuendeleas kutoa msaada kwa serikali kuimarisha afya ya mama na mtoto kupitia programu ya Uzazi ni Maisha Wogging. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, mama Mariam Mwinyi, Naibu Waziri wa Afya, Khamis Hafidh na Mkurugenzi Mtendaji wa Amref Afrika Tanzania,  Dk. Florence Temu Dk. Mwinyi alitoa pongezi hizo mara baada ya kushiriki matembezi ya hiyari na mbio fupi yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kununulia vifaa tiba vitakavyotumika katika hospitali na vituo vya afya vya maeneo mbali mbali ya Zanzibar ili kupunguza vifo vya Mama na Mtoto Zanzibar Dk. Mwinyi ameeleza kuwa jitihada zinazochukuliwa na wadau wa maendeleo, wahisani na mashirika ya ndani nay a kimataifa yanaongeza uwezo wa serikali katika kuhudumia watu wake hivyo zinapaswa kupongezwa na kuungwa mkono. Alisema licha ya serikali k

ZMBF, Afya Checkers kuimarisha kampeni ‘Afya Bora, Maisha Bora’

Image
NA MWANDISHI WETU TAASISI ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) imeingia makubaliano ya ushirikiano na Afya Checkers ya jijini Dar es salam kwa ajili ya kutoa huduma za afya kupitia kampeni ya ‘Afya Bora, Maisha Bora’ inayoendeshwa na taasisi hiyo kupitia matembezi ya ‘Mariam Mwinyi Walkathon’. OFISA Mtendaji Mkuu wa Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Fatma Fungo (kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Afya Checkers, Dk. Ramona Malikusema, wakisaini makubaliano ya ushirikiano utekelezaji wa kampeni ya ‘Afya Bora Maisha’ katika ofisi za ZMBF, Migombani Zanzibar.   Matembezi hayo ambayo ni mwendelezo wa kampeni ya mama Mariam aliyokua akiifanya kupitia matembezi ya kila mwisho wa mwezi, yanatarajiwa kufanyika Septemba 30, mwaka huu kwa kutanguliwa na kambi ya matibabu itakayofanyika Septemba 28 na 29. Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa ZMBF, Fatma Fungo, alieleza hatua hiyo inalenga kuyaimarisha matembezi hayo na kutoa fursa kwa

NMB, ATCL waja na 'Anga rafiki - Tiketi yako imebima'

Image
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAM BENKI ya NMB na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wamezindua ushirikiano wa kibiashara wa malipo ya tiketi za ndege ujulikanao kama 'Anga Rafiki - Tiketi Yako Imebima'. AFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi wakionesha mfano wa ndege kuashiria uzinduzi wa mfumo wa malipo ya tiketi za ndege kupitia matawi na mawakala wa NMB  hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha wa ATCL, Jamal Kiggundu na kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi. Mfumo huo unaowapa fursa wasafiri watakaotumia ndege za shirika hilo kulipia tiketi kupitia matawi, mawakala na huduma za NMB Mkononi (NMB app) ambazo zitakuwa zimekatiwa bima ya safari. Ushirikiano huo umezinduliwa jana katika Makao Makuu ya NMB jijini Dar es salaam ambapo Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa NMB, Ruth Zaipuna, alieleza kuwa msaf

Dimwa azionesha fursa za kilimo jumuiya CCM

Image
NA mWANDISHI WETU NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Mohammed Said Mohammed ‘Dimwa’, amezishajihisha jumuiya za CCM kuyatumia mashamba ya chama hicho kulima kilimo cha kisasa ili kujipatia ajira. Dk. Dimwa alieleza hayo mara baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho ya wakulima nane nane huko katika viwanja vya Dole Kizimbani, wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja. Alisema CCM ina mashamba makubwa na moja katika malengo yake ni kuwekekeza katika kilimo hivvo ni fursa sasa kwa vijana na jumuiya zote za chama ambao wanataka kujiunga na kilimo kuyatumia sasa mashamba hayo. “CCM ina mashamba mengi yakiwemo ya Kilombero, Kiwengwa na Bumbwini lakini la kilimo hasa ni hili la Kilombero na tuna heka nyingi waende kwenye maonesho kupata elimu ili waweze kuyatumia na wajiajiri kama inavyoelekezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ili kuepuka kukaa bila ya kazi maalum,” alisema. Aidha alisema, chama kimeshazungumza na benki

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Image
NA MWANAISHA SHARIA, MOROGORO WAANDISHI wa habari wametakiwa kuendelea kuibua changamoto mbali mbali zinazowakabili wanawake ili wapate fursa za maendeleo zinazojitokeza nchini. Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya alipokua akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za usawa wa kijinsia yaliyofanyika hoteli ya Flomi, mjini Morogoro. Amesema wandishi wa habari wana nguvu ya kufikisha ujumbe kwa jamii hivyo wana jukumu la kuhakikisha wanatoa elimu ya usawa wa kijinsia ili kutatua changamoto zilizopo. "Waandishi wa habari mtakapoibua kero za wanawake na kuzisemea mtaleta mabadiliko kwa wanawake hao lakini pia jamii nzima kwani kupitia kwao ukatili na ukandamizaji wanawake na watoto wa kike utaondoka”, alieleza Simbaya. Aidha Mkurugenzi huyo amewataka waandishi waliopatiwa mafunzo hayo kutumia vizuri elimu hiyo kwa kuandika habari na kuanda vipindi kuhusu usawa wa kijinsia ili kuleta mabadil

TADB yawaonesha fursa wakulima, wavuvi

Image
NA MWANDISHI WETU MKURUGENZI Idara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula, Hamad Masoud Ali (wa kwanza kulia), amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wakulima hapa nchini kutumia fursa mbali mbali zikiwemo za mikopo ili kuongeza uzalishaji wa mazao. Mkurugenzi huyo alieleza hayo, kwenye hafla ya ufunguzi wa semina iliyowashirikisha wakulima, wafugaji na wavuvi, hafla iliyofanyika katika viwanja vya maonesho ya kilimo vilivyopo Dole. Alisema ili wakulima, wafugaji na wavuvi wapige hatua, lazima wawe na uhakika wa mtaji, ambapo suala hilo hivi sasa limerahisishwa kwani upo uwezekano wa kuchukua mikopo kwenye taasisi za kifedha. Alieleza kuwa wakulima wengi wa Zanzibar wamejikita kwenye kilimo cha kujikimu kutokana na kutokuwa na mtaji, hivyo uwepo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, utawasaidia kuondokana na changamoto wa mitaji. Alifahamisha kuwa suala jengine muhimu litakalowafanya wakulima, wafugaji na wavuvi wapige hatua na kupata tija zaidi ni kuhakikisha wanakuwa na elimu ya kutosha kwa s

ZMBF yawapelekea 'Tumaini Kits' wanafunzi wa kike

Image
NA MWANDISHI WETU MKE wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni muasisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, ameeleza kuwa taula za kike zinazotolewa na taasisi hiyo kwa wanafunzi wa kike zinawaweka kwenye mazingira salama. Ameeleza hayo wakati wa hafla ya ugawaji wa taula za kike za Tumaini (Tumaini Kits) kwa wanafunzi wa skuli ya Kijini, iliyopo wilaya ya Kaskazini ‘A’, mkoa wa Kaskazini Unguja. Mwenyekiti huyo alisema msichana anapotumia taula hizo huwa kwenye mazingira salama na kwamba muda wote humuwezesha kuhudhuria masomo yake bila ya kukatisha masomo kutokana na kuwa kwenye hedhi. Mwenyekiti wa ZMBF mama Mariam Mwinyi akihutubia wakati wa h afla ya ugawaji wa taula za kike za Tumaini (Tumaini Kits) kwa wanafunzi. Aidha alifahamisha kuwa taula za Tumaini kits zinazotolewa na ZMBF zina faida kwa wasichana na wanawake ikiwemo faida za kuwa salama kwa afya ya uzazi. Alieleza kuwa zinaweza kutumika zaidi ya miaka mitatu na