Posts

Showing posts from May, 2023

Wanafunzi MCC, MSJ watakiwa kusoma kwa bidii

Image
NA ASYA HASSAN WANAFUNZI wanaosomea fani ya habari katika chuo cha Mwenge Community Center (MCC) na Morogoro School of Journalis (MSJ) wametakiwa kusoma kwa bidii ili kuwa wataalamu wazuri wa fani ya habari wanapomaliza masomo yao. Mwenyekiti wa KLABU ya Waandishi ya Habari Zanzibar (ZPC), Abdallah Abdulrahman Mfaume, alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na wafunzi hao chuoni kwao Amani, ikiwani mwendelezo wa shughuli za maadhimisho ya miaka 30 Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani iliyoadhimishwa Mei 3, mwaka huu. Alisema hatua hiyo itawasaidia kuwa ujasiri katika kutekeleza vyema majukumu ya kuisemea jamii kwaniu tasnia hiyo ni muhimu katika kuchochea maendeleo na ustawi wa jamii. “Leo mpo chuoni lakini mtakapotoka hapa mtakwenda kuitumikia jamii hivyo kuna umuhimu kwenu kujikita katika masomo ili maarfa mnayoyapa mkayatumie kuimarisha ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi”, alieleza Mfaume. Sambamba na hayo aliwataka waandishi wa habari hapa nchini kuacha mihemko wanapo

SMZ, SMT kushirikiana uhifadhi wa misitu

Image
NA SALAMA MOHAMED, WKUMM KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo,  Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Seif Shaaban Mwinyi, amesema serikali zote mbili za Tanzania na taasisi zake zitaendelea kuimarisha mashirikiano ili ziweze kuleta maendeleo nchini.  Akizungumza katika hifadhi ya Msitu Pugu  kanda ya Mashariki wilaya ya Ilala, Dar es salam wakati wa ziara ya kutembelea msitu wa Jane Goodall iliyojumuisha viongozi na watendaji wa Wizara hiyo. Mhifadhi wa msitu wa Jane Goodall uliopo Pugu jijini Dar es salam, Rashid Mustafa (kushoto)  akitoa maelezo kwa viongozi wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar walipotembelea msitu huo wakati wa ziara ya kujifunza inayoongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Seif Shaaban Mwinyi (wa tatu kulia). Amesema dhamira ya ziara hiyo ni kuongeza mashirikiano na kujifunza mazingira yaliopo katika msitu huo ambapo taasisi hiyo imeweza kupiga hatua ya maendeleo katika kuwainua vijana kujifunza mbinu mbali mbali za hifadhi ya misitu. Seif ameel

Serikali yaahidi msukumo uzalishaji mazao ya nyuki

Image
NA MWANDISHI WETU WIZARA ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imeeleza kuwa itaendelea kutoa msukumo kwa wafugaji wa nyuki na wazalishaji wa mazao ya nyuki ili kuimarisha uchumi wao na na tija kwenye kilimo. Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ali Khamis Juma, alipokua akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Nyuki Dulinani yaliyofanyika Kitogani, mkoa wa Kusini Unguja. Alieleza kuwa kutokana na faida zinazopatikana kwenye ufugaji wa nyuki, ipo haja kwa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kuweka mkazo wa kuiimarisha sekta hiyo ili isaidie ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. “Kama mlivyoeleza hapa, nyuki ana faida nyingi kiuchumi na kijamii hivyo wakati wizara mnaendelea na mapitio ya sera ya misitu, mnaweza kutunga kanuni za misitu na nyuki ili kulinda makundi ya nyuki yaliyoanza kupotea”, alieleza Juma. Aidha aliwataka wafugaji hao kufuata maelekezo ya wataalamu sambamba na kulinda uoto wa asili ili kuzalisha bidhaa zitakazotosh

Puma Energy, KIST zasaini makubaliano kukuza ujuzi

Image
NA MWANDISHI WETU KAMPUNI ya  Puma Energy Tanzania imesani makubaliano ya utekelezaji wa programu ya kukuza ujuzi kwa wahitimu wa Taasisi ya Teknolojia Karume (KIST) na Pamoja Zanzibar. Akizindua programu hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Muhamed Mussa, amewataka wahitimu waliopata fursa ya kufanya kazi katka kampuni ya  kuitumia vyema ili kukuza ujuzi na uwezo wao katika kazi. Alitoa wito huo jana wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya progrmu ya kuendeleza ujuzi wa wahitimu wa Taaasisi ya Teknolojia Karume (KIST) na taasisi ya Pamoja Zanzibar kwa upande mmoja na kampuni ya Puma Energy Tanzania iliyofanyika Mbweni mjini unguja. Alieleza kuwa kutokana na mifumo ya elimu na ujuzi iliyopo nchni inazingatia wanafunzi kusoma ili kufaulu mitihani, hivyo mpango huo utawasaidia wahitimu hao kupata ujuzi na uzoefu utakaoimarisha maarifa waliyoyapata chuoni. Lela aliishukuru kampuni ya Puma kwa kuingia makubaliano hayo na taasisi mbili hizo hatua itakayotoa nafasi za ajir

ZBS yanasa nyaya ‘feki’ za umeme

Image
NA MWANDISHI WETU TAASISI ya Viwango Zanzibar (ZBS) imezuia matumizi na usambazaji wa nyaya za umeme (PVC Cable) zenye jina la Kili Cable na namba ya utambulisho TP/EEL/18/2023 baada ya kugundulika kuwa zipo chini ya viwango. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ofisi za taasisi hiyo Maruhubi, Mkurugenzi Mkuu wa ZBS, Yussuph Majid Nassor, ameeleza kuwa mbali ya kuwa chini ya kiwango, pia mtengenezaji amefoji jina la kibiashara la bidhaa hiyo. Majid ameeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa bidhaa hiyo sokoni zilizoingizwa nchini na mfanyabiashara asiyefahamika jambo ambalo ni kinyume na sheria. Amesema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema, ZBS ilichukua sampuli za bidhaa hiyo na kuifanyia uchunguzi wa kimaabara na kugundulika kutokidhi viwango vilivyowekwa.   “Tulipochukua sampuli za waya hizo na kuzipima kwenye mabara zetu, ripoti ya upimaji wa sampuli hizo imenakiliwa kuwa bidhaa hii imefeli   katika kipengele cha ‘sheath’

Ibueni mbinu zitakazowavutia wafadhili - Simbaya

Image
NA MWANDISHI WETU MKURUGENZI Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Keneth Simbaya (pichani kushoto), ameushauri uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kubuni mbinu zitakazoimarisha utendaji na kujitegemea. Simbaya aliyekuwa Zanzibar kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari (WPFD) iliyoadhimishwa kitaifa mjini Zanzibar, alifanya ziara katika ofisi za klabu hiyo Kijangwani na kukutana na viongozi na badhi ya wananchama. Aidha ameeleza kuridhwa na mipango ya Klabu hiyo na kuwataka kuondokana na utegemezi wa mfadili mmoja badala yake kuwa na mikakati itakayowasaidia wanachama wa klabu hiyo kupata maendeleo. Aidha alieleza kuwa muelekeo wa UTPC ni kuzijengea uwezo klabu na viongozi wake ili ziweze kujisimamia kama njia moja ya kuuimarisha muungano huo unaounndwa na vilabu 28 vya waandishi wa habari vya Tanzania bara na Zanzibar. "Lazima mtafute mbinu za kufikia ndoto zenu kama viongozi kukidhi matarajio y