Posts

Showing posts from October, 2021
Image
  HAFLA YA UZINDUZI WA RASMI MWONGOZO WA MASHAURI KWA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAWAKE KATIKA PICHA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia, uliofanyika Oktoba 28, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Kitabu cha Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia. Uzinduzi huo umefanyika Oktoba, 28 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, wa pili kushoto Mwakilishi mkazi wa UN Women hapa nchini bibi.  Hodan Addou, kulia Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello. Baadhi ya wanachama wa chama cha majaji na mahakimu wanawake (TAWJA) na w
Image
UN kusaidia utatuzi changamoto mifumo ya afya NA MWANDISHI WETU UMOJA wa Mataifa (UN) Tanzania umeeleza kuridhishwa na ushirikiano uliopo baina ya serikali za Tanzania katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii. Hayo yameelezwa na watendaji masjhirika ya umoja huo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Umoja wa Mataifa Kinazini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shughuli za maadhimisho ya miaka 76 toka kuasisiwa kwake. Walieleza kuwa mashirika ya umoha huo, yanakusudia kushirikiana na serikali kuimarisha mifumo ya afya ili kuhamasisha jamii kuondokana na maradhi mbali mbali ukiwemo wa UVIKO 19. Akizungumza hatua hizo, Dk. Vendelin Simon kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha ifikapo 2030 jamii inakuwa salama dhidi ya magonjwa yakiwemo ya kuambukizia  “Kupitia maadhimisho haya tutajiikita zaidi katika kuimarisha mazingira ya usafi katika maeneo ya fukwe na kuyafikia makundi ya wanajamii wakiwemo wanafu
Image
Tanzania inatambua kazi zinazofanywa na UN – Dk. Tax NA SAIDA ISSA, DODOMA JAMHURI  ya Muungano wa Tanzania imesema inatambua kazi kubwa inayofanywa na Umoja wa Mataifa (UN) ikiwemo ya kuimarisha umoja, mshikamano na ustawi wa jamii. Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa jijini Dodoma, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax, alisema kuwa siku hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa. Alieleza kuwa maadhimisho hayo yanayofanyika kila mwaka yanalenga kutambua kazi zinazofanywa na umoja huo katika mataifa mbali mbali ulimwenguni ikiwemo Tanzania. "Katika kipindi cha miaka 76 Umoja wa Mataifa umejitanabaisha kuwa ni taasisi muhimu kimataifa kutokana na mchango mkubwa katika masuala mabli mbali ya kimaendeleo, kijamii na amani ulimwenguni," alisema Waziri huyo. Alieleza kuwa katika kipindi hiki dunia ikiwa inapambana na mlipuko wa UVIKO 19, ambao umesababisha changamoto nyingi na kuathiri dunia nzima katika sekta mbali mbali ikiw
Image
Samia awaapisha mawaziri, wajumbe NEC LAwataka kuzingatia weledi, uwajibikaji NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAM RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewaapisha viongozi mbali mbali aliowateua hivi karibuni na kuwataka kuzingatia weledi katika utekelezaji wa majukumu yao. Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ikulu ya Dar es salam, Rais Samia amewaapisha viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na viongozi walioteuliwa kushika nafasi katika wizara ya habari na kuwaomba watekeleze majukumu yao kwa ufanisi. Alisema uteuzi viongozi hao utaleta uwajibikaji mzuri hasa katika   sekta ya habari kwa vile hivi sasa inakwenda kwenye mabadiko ya kukuza matumizi ya teknologia. Aidha aliwataka viongozi hao kuzingatia uwajibikaji na kusimamia utendaji kwenye maeneo yao ya kazi ili Tanzania ipige hatua za maendeleo kwa kasi zaidi. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Makamu wa Rais Dk. Isdori Mpango alisema imeonekana somo la aina ya uongozi anaoutaka Rais Sa
Image
TASAF yaidhinishiwa 5.5b/- kukabili athari za UVIKO 19 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM MKURUGENZI Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF), Ladislaus Mwamanga, amesema mfuko huo umeidhinishiwa shilingi bilioni 5.5 kati ya fedha zilizotolewa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Shirika la Fedha Kimataifa (IMF). Mwamanga alieleza kuwa TASAF itazitumia fedha hizo kuondoa athari za kiuchumi zilizochochewa na mripuko wa UVIKO 19 kwa kaya 40,740 za walengwa wa TASAF, wenye uwezo wa kufanya kazi katika miradi ya jamii wanaoishi Mjini. Alieleza hayo jana katika ofisi za jijini hapa, wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ofisi za mfuko huo kuhusiana na Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO -19 kwa mpango wa kunusuru kaya za walengwa wa TASAF. Alisema kupitia hizo kaya za walengwa wenye uwezo wa kufanya kazi wanaoishi katika maeneo ya mjini, watafanya kazi katika miradi ya jamii na kulipwa ujira wa wastani wa shilingi
Image
Wazazi wekezeni kwenye elimu za watoto wenu - Mbunge NA MWANDISHI WETU MBUNGE wa Jimbo la Dimani, Mustapha Mwinyi Kondo, amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi wa skuli ya Msingi Kisauni kuwekeza zaidi katika elimu za watoto wao badala ya mambo mengine yasiyo na tija kwa maisha yao ya sasa na baadae. Mustapha alieleza hayo wakati wa sherehe za kuwaaga walimu wa waliostaafu na kuwapongeza wanafunzi waliofaulu michipuo katika mitihani yao ya taifa ya darasa la sita mwaka 2020. Katika sherehe hizo zilizofanyika katika skuli hiyo iliyopo wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja, Mbunge huyo alieleza kufanya hivyo pia kutachangia maendeleo ya skuli hiyo wakati msaada unapohitajika ili watoto wao kufanya vizuri katika masomo yao. Alisema licha ya serikali kutoa elimu bila ya malipo lakini wazazi wanapaswa kuchangia baadhi ya misaada ya kielimu inapohitajika pale uongozi wa skuli unapowataka wazazi na walezi kutoa misaada yao katika kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili Shule hiyo. Al
Image
Wanahabari watakiwa kuzingatia usalama wao wakiwa kazini NA KHAMISUU ABDALLAH MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Mussa Yussuf, amewataka waandishi wa habari kujiunga na jumuiya za waandishi ili kuzungumzia changamoto zinazowahusu na kuzipatia ufumbuzi. Mussa ambae pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma alitoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya ulinzi na usalama kwa wanahabari yaliyofanyika jjini Dodoma. Alisema ikiwa wanabari watajiunga na jumuiya hizo, changamoto nyingi zinazowakabili wandishi wa habari na taaluma ya uandishi wa habari zitapatiwa ufumbuzi na kuleta mabadiliko katika utekelezaji wa majukumu yao. Hata hivyo alikemea tabia ya makundi ndani ya jumuiya hizo na kueleza kuwa ni adui anaeharibu jumuiya zao kutofikia malengo waliyojiwekea. “Tunapokutana lazima tuzungumze madhaifu yetu kwani moja ya vitu vinavyoharibu jumuiya nyingi za wanahabari ni makundi na yamejigawa zaidi kimas