Posts

Showing posts from November, 2023

Wadau TIB watakiwa kuimarisha mashirikiano

Image
NA MWANDISHI WETU  WADAU wa Benki ya Maendeleo nchini (TIB) wametakiwa kuimarisha mashirikiano ili kuongeza mchango wa benki hiyo katika maendeleo ya taifa. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila (kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo TIB, Agapiti Kobello (wapili kushoto) wakati alipowasili kufungua Mkutano wa Wadau wa Benki ya Maendeleo (TIB) Kanda ya Dar es Salaam uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam. Wengine ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TIB, Juma Hassan Reli (watatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Lilian Mbassy (wapili kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miradi, Zuwena Hemed (kulia).   Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila wakati akifungua mkutano wa majadiliano uliowakutanisha watendaji na wadau wa benki hiyo wa kanda ya Dar es salaam ulioangalia majukumu na mafanikio ya benki hiyo katika kuchangia maendeleo nchini. Mkutano hu

Vodacom yawapa uhakika wa matibabu mama, watoto wachanga

Image
NA MWANDISHI WETU KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom imetoa zawadi ya bima kubwa ya afya kwa mama 100 na watoto wachanga 100 waliozaliwa na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Mnazimmoja, Zanzibar. Mama (mzazi)   Maryam Yohana Daniel (aliyeketi) akipokea bima kubwa ya afya kwa niaba ya wenzake wakati wa hafla ya ugawaji wa bima hizo kwa mama wazazi na watoto katika hospitali ya Mnazimmoja. Hatua hiyo ni sehamu ya kampeni ya kampuni hiyo ya kueneza upendo katika msimu wa sikukuu ambapo k ina mama waliojifungua kuanzia Novemba 9, mwaka huu katika hospitali hiyo watapatiwa bima ya ‘Voda Bima’. Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi bima hizo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Annette Kanora (wa tatu kushoto), alisema hatua hiyo ni muendelezo wa mpango wa kampuni hiyo kuwashukuru wateja wake na kusaidia kupunguza changamoto zinazoikabili jamii.   Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Annette Kanora (wa tatu kushoto) pamoja na wa

Enezeni elimu kupunguza uharibifu wa misitu – Shamata

Image
NA SALAMA MOHAMMED, WKUMM WAZIRI wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame Khamis, ameitaka Idara ya Misitu kuandaa mafunzo maalum kwa wanajamii, Taasisi za Serikali na Zisizo za kiserikali (NGO's) ili kupunguza uharibifu wa misitu. Ameeleza hayo shehia ya Bwejuu katika eneo la hifadhi ya Msitu wa Jamii Tongole, wilaya ya Kusini Unguja wakati alipokua akizindua zoezi la Upandaji wa miti asili kwenye msitu huo. Shamata amesema kuna baadhi ya watu wana mwamko mdogo wa kutunza misitu asili na hivyo kusababisha matatizo yakiwemo ya mabadiliko ya tabia nchi hivyo wakipatiwa elimu itawasaidia kuondokana na uharibifu huo.   Aidha amefahamisha kuwa lengo la hatua hiyo ni kudhibiti uharibifu wa msitu na uvamizi unaofanywa na watu kwa kufyeka miti kuandaa mashamba ya shughuli za kilimo, ujenzi na ujenzi wa makaazi usiozingatia taratibu na sheria za nchi.   "Nataka kuwakumbusha kwamba msitu huu umehifadhiwa na jamii chini ya sheria ya misitu namba 10 ya mwaka 1996

Mama Mariam ahimiza lishe bora, mazoezi kujikinga na maradhi

Image
NA MWANDISHI MAALUM, LONDON MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) mama Mariam Mwinyi, amesisitiza umuhimu kwa jamii kubadili mtindo wa maisha kwa kuzingatia lishe bora, sambamba na kufanya mazoezi. MKE wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Mariam Mwinyi akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa afya za maradhi yasiyoambukiza (NCDs), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Marlborough House nchini Uingereza. Mama Mariam alitoa wito huo wakati wa uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa afya za maradhi yasiyoambukiza (NCDs) unaolenga kutekelezwa katika nchi 56 wanachama wa Jumuiya ya Madola katika ukumbi wa Marlborough House, Uingereza. Alieleza kuwa ili kukabiliana na maradhi yasiyo ya kuambukiza kama ya saratani, ugonjwa ya moyo, shinikizo la damu na mengineyo hususani kwa vijana, kuna hitajika jamii kuhakikisha inapata lish

NBC kushirikiana na taasisi SMZ kukusanya mapato, kuimarisha huduma

Image
NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum (pichani), amesema mashirikiano kati ya benki ya taifa ya biashara (NBC) na taasisi za Serikali kwenye matumizi ya mifumo ya kidigitali yataongeza ufanisi kwa taasisi za serikali hususani katika ukusanyaji wa mapato. Dk. Mkuya ameeleza hayo wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano kati ya benki hiyo na taasisi sita za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege Zanzibar. Alieleza kuwa hatua hiyo pia itachochea upatikanaji wa huduma bora kwa wateja na kuondoa urasimu unaochochea vitendo vya upotevu wa mapato lakini pia kukuza uwekezaji nchini. Aliongeza kuwa mashirikiano baina ya benki hiyo na taasisi hizo yatachochea matumizi ya mifumo ya kifedha katika jamii jambo litakaloongeza nguvu ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Aidha alieleza kuwa serikali inakamilisha maandalizi ya sheria ya serikali mtandao ili

Msaada wa kisheria unahitajika kuwaokoa watoto wanaokinzana na sheria

Image
NA AMINA MCHEZO MSAADA wa watoto kisheria, kisera na kimipango ni uwanja mpana huku ikionekana sheria iliopo Sasa ya mtoto sheria namba 6 ya mwaka 2011 inamapungufu hivyo wizara ya Màendeleo ya jamií, jinsia, wazee na watoto Zanzibar inafanya juhudi kuhakikisha sheria hiyo inapitiwa upya. Sheria hiyo Kwa Sasa inaonekana bado haitoi ulinzi Bora Kwa mtoto hivyo Kwa Sasa wadau na taasisi za usimamizi wa mtoto wamekuwa wakiisindikiza tume ya marekebisho ya sheria ili kuwe na sheria mpya. "Kwa Sasa tumeshatoka kwenye hatua nyingi za ukusanyaji wa maoni ya wadau na Sasa nadhani tupo katika hatua ya kuishirikisha tume ya marekebisho ya sheria ili tuone kwamba tunapata baraka za mwisho na kunipeleka mbele ili tuwe na sheria mpya ili mambo yawe mazur Kwa watoto" Amesema mkuu wa wa Division   ya hifadhi ya mtoto kupitia idara ya ustawi wa jamii na wazee. WASAIDIZI wa Sheria (Paralegal) wakiwa katika moja ya mikutano ya kujengewa uwezo ili watoe huduma bora wa wateja wao. Mtoto an

Nsokolo ahimiza ulinzi wa waandishi, vyombo vya habari

Image
NA KHAMISHUU ABDALLAH RAIS wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), DeogratIus Nsokolo, amewasisitiza waandishi wa habari kuuelimisha umma juu ya umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na nafasi ya waandishi katika jamii. Nsokolo alitoa rai hiyo wakati akifungua mdahalo kuadhimisha siku ya kimataifa ya Kukomesha Uhalifu dhidi ya Waandishi wa Habari uliofanyika wa njia ya mtandao jana, ulioshirikisha waandishi wa habari, viongozi wa klabu za wanahabari, UTPC na wadau wengine. Alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza ufahamu kwa jamii jinsi vyombo vya habari vinavyochangia kujenga jamii yenye habari na taarifa sahihi na uelewa utakaoujenga mazingira bora kwa wanahabari kufanya kazi zao bila ya vitisho na vikwazo. Aidha alisema pia hatua hiyo inaweza kuzuia misimamo ya upande mmoja na kupotosha habari kwa kuuelimisha umma jinsi waandishi wanavyochunguza na kuripoti masuala yanayowahusu na vitendo visivyo na maadili. Aliongeza kuwa ili kujenga taifa lenye umoja, m