Posts

Showing posts from September, 2023

ZBS yachangia kambi ya matibabu ya ZMBF

Image
NA MWANDISHI WETU TAASISI ya Viwango Zanzibar (ZBS) imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali ili kuimarisha ustawi wa jamii na uchumi kupitia njia mbali mbali. Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Yusuph Majid Nassor, alieleza hayo jana wakati akikabidhi msaada wa vifaa vya uchunguzi na matibabu kwa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) kwa ajili ya kambi ya uchunguzi wa afya na matibabua itakayofanyika kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba 2, mwaka huu. Yusuph alieleza kuwa hatua hiyo inaangukia katika moja ya maeneo yanayosaidiwa na taasisi yake kupitia mpango wa kusaidia jamii na wadau wake ikiwemo taasisi hiyo ambayo ni miongoni mwa wateja wake. “Kila mwaka huwa tunatoa sehemu ya mapato tunayokusanya kwa jamii na tumelkua tukipeleka msaada kwa wizara ya afya na kwa mwaka huu tunaelekeza sehemu ya mapato hayo katika tukio hili kuiunga mkono ZMBF lakini pia wizara ya afya”, alieleza Yussuph. Hata hivyo aliahidi kuwa taasisi yake itaendelea kusaidia shughuli

Uislam unakubali uzazi wa mpango

Image
NA MWAANDISHI MAALUM KWA muda mrefu, suala la uzazi wa mpango limekuwa na mjadala mrefu katika jamii na vyombo vya habarijuu ya kama jee ni sawa au linapingana na maelekezo ya dini ya Kiislamu? Maelezo yamekuwa mengi na yenye aina tafauti ya maelezo, lakini ukweli na uhakika ni kwamba dini ya Kiislamu haina pingamizi juu ya uzazi wa mpango kwa vile linasaidia mzazi na mtoto kuwa na afya bora. Sheikh Khamis Abdulhamid Mjumbe wa Baraza la Maulamaa Zanzibar, Sheikh Khamis Abdulhamid, amesema dini ya Kiislamu haijakataza  uzazi wa mpango ambao hauna na madhara kwa pande zote mbili. “Wakati Quran inashushwa Masahaba waliwahi kusema Quran haikutukataza kutumia njia ya mshindo (kumwanga maji ya uzazi nje) ili kupanga uzazi“, Sheikh Khamis alisemaa. Hata hivyo, aliongeza ni muhmu kwa wanawaume kujitahidi kufuatilia na kujipanga kupata elimu ili ndoa zao ziwe na furaha kwa kuweka utaratibu maalum wa kupata watoto. “Ikiwa mtu atasema ukikataa kuzaa nimekuacha basi hakika hio ni talaka ila hi

Dk. Mwinyi awapongeza madaktari wa China

Image
NA MWANDISHI MAALUM RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Serikali ya China kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Tanzania ikiwemo Zanzibar kwenye masuala mbali mbali ya maendeleo. Dk. Mwinyi ametoa shukurani hizo Ikulu, Zanzibar alipowakabidhi vyeti na medali timu ya madaktari 32 kutoka China waliohudumu kwenye hospitali za Zanzibar kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuwaaga baada ya kumaliza muda wao nchini. Rais Dk. Mwinyi amesema, Zanzibar imenufaika na fursa nyingi kutoka China kupitia sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo Afya hususan kupokea timu za madaktari bingwa wanaofika nchini kubadilishana uzoefu na wazawa hali aliyoieleza imeimarisha uhusiano mwema uliopo baina yao pamoja na kujifunza uzoefu wa masuala mbalimbali ya afya. Dk. Mwinyi alieleza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendeleza maeneo mengi ya afya kwa kujenga hospitali zenye vifaa tiba vya kisasa, kuboresha miundombinu na kuongeza hospitali za wilaya na mikoa pa

Dk. Samia awaonya wanasiasa katiba mpya

Image
Asema   si mali ya wanasiasa, a wataka kutolazimisha upatikanaji wake NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM RAIS wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema katiba si mali ya vyama vya siasa, bali ni ya watanzania wote, hivyo marekebisho yanayohitaji kufanyika lazima kufanyike tafakari kubwa. Dk. Samia alieleza hayo jana katika ukumbi wa kituo cha mikutano cha Julius Nyerere, Dar es Salaam wakati akifungua mkutano maalum wa siku tatu wa baraza la vyama vya siasa na wadau wa demokrasia.  Alitumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuacha jukumu la kujimilikisha katiba, kwani si mali yao na kutumia fursa hiyo kuvitaka vyama vikatoe maoni ya katiba. Alisema maoni yaliyopo kila upande, wamependekeza marekebisho ya katiba kwa upande wa bara na Zanzibar, lakini mchakato wa marekebisho ya katiba si mali ya vyama vya siasa na hivyo wanasiasa waache kuwaburuza wananchi. “Mchakato wa katiba si mali ya vyama vya siasa, katiba ni ya watanzania, awe

Tutaendelea kuzipatia ufumbuzi changamoto za wananchi – Ayoub

Image
NA MADINA ISSA MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema ataendelea kushirikiana na watendaji wanaosimamia sekta mbali mbali ili wananchi wa mkoa huo waendele kupata maendeleo. MKUU wa mkoa wa Kaskazini Unguja,Ayoub Mohammed Mahmoud (wa pili kushoto) akimsikiliza sheha wa shehia ya Mangapwani wakati wa kikao cha kusikiliza changamoto za wananchi wa mkoa huo. Akizungumza na wananchi katika kikao cha kusikiliza changamoto kwa wananchi wa kijiji cha Bumbwini, wilaya ya Kaskazini ‘B, alisema baadhi ya changamoto zimekuwa zikipatiwa ufumbuzi ili wananchi wafaidike na huduma. Alisema serikali ya awamu ya nane imekuwa na lengo la kufikisha huduma muhimu kwa wananchi wake, hivyo aliwahakikishia wananchi kuendelea kushirikiana nao ili kuona huduma hizo zinawafikia kwa wakati. Akizungumzia suala la wananchi kuendelea kunufaika na rasilimali zilizopo ndani ya mkoa huo, aliwataka wananchi wa Shehia hiyo kusubiri kwa muda wa wiki mbili kutatua changamoto zilizopeleke

Utafiti kuimarisha zao la mwani unahitajika - Mama Mariam

Image
NA MWANDISHI WETU MWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, ametoa rai ya kufanyiwa utafiti wa zao la mwani ili kulitambulisha zaidi duniani. MKE wa Rais wa Zanzibar mama Mariam Mwinyi (kulia), akimsikiliza rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA), Dk. Agnes Kalibata, mazungumzo hayo yaliyofanyika jana katika ukumbi mdogo wa jengo la mikutano la kimataifa la Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Mama Mariam alitoa rai hiyo alipozungumza kwenye mkutano wa kimataifa unaojadili mfumo wa chakula kwenye mada ya nafasi ya mwanamke kwenye sekta ya kilimo na chakula, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa la Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Alisema Zanzibar ni nchi inayoongoza barani Afrika kwenye uzalishaji mwani na inakamata asilimia tatu ya pato la taifa baada ya utalii unaochangia asilimia 30 ya pato la taifa na kilimo cha karafuu. Alisema, asilimia 70 ya dunia ni bahari na 30 ni ardhi hiyo alisema

KCFZ yasaidia kambi za wanafunzi Fujoni

Image
NA MWANDISHI WETU TAASISI na mashirika ya ndani na nje ya nchi zimetakiwa kutoa misaada kwa wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya taifa ili kurahisisha juhudi za walimu za kuhakikisha wanafunzi wanapata matokeo mazuri. MENEJA wa taasisi ya Korea Culture Foundation for  Zanzibar (KCFZ), Jenipher Barnaba Marcus akizungumza na wanafunzi waliopo katika kambi ya masomo skuli ya Fujoni wakati walipofika kutoa msaada wa chakula na vyandarua kwa wanafunzi wa skuli hiyo. Wito huo umetolewa na Mwalimu Mkuu skuli ya Fujoni, wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, Abdu Maulid Fidia, alisema hayo skulini hapo mara baada ya kupokea msaada wa mchele na vyandarua vilivyotolewa na taasisi ya utamaduni ya Korea (Korea Calture of Zanzibar - KCFZ). Alisema wanafunzi wanaojiandaa na mitihani kwa kukaa kambi wana mahitaji mengi yakiwemo ya vyakula hivyo kujitokeza kwa wadau hao kutasaidia upatikanaji wa mahitaji kwa wanafunzi. Aidha alisema baadhi ya wanafunzi wameshindwa kukaa kambi kutokana na kutomudu gharama za