Posts

Showing posts from June, 2022

'Andikeni habari zitakazochochea maendeleo '

Image
NA MWANDISHI WETU WANAHABARI nchini wametakiwa kubadilika na kuandika habari zitakazochochea maendeleo ya nchi na watu wake. Wito huo Umetolewa na Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Hassan Khatib Hassan, (wa katitaki pichani) alipokua akifungua mafunzo ya waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kwa kushirikiana na shirika la Internews Tanzania, yaliyofanyika katika ukumbi wa Uhuru, Kariakoo Zanzibar. Alieleza kuwa vyombo vya habari ni muhimu kwani vinaweza kuandika habari zenye kuibua hamasa ya wananchi kufikia dhamira ya serikali na kufichua maovu dhidi ya maendeleo ya nchi na watu wake. Hassan aliongeza kuwa wananchi walio wengi wanasikiliza na kufuatilia vyombo vya habari wakiamini kuwa watapata taarifa za ukweli na zinazozingatia weledi na sio taarifa za kubuni ama kughushi.   “Iwapo mtajikita zaidi kutaka kuwafurahisha wasomaji na wasikilizaji au watazamaji basi tunaweza kufika pahala tukapoteza m

Semina ya Makatibu Wakuu na Wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii Baraza la Wawakilishi

Image
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Jabir Bakari akitoa salamu za mamlaka hiyo kabla ya ufunguzi wa semina ya Makatibu Wakuu na Wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi kuhusu dhana ya wasambazaji maudhui katika utangazaji iliyofanyika katika hoteli ya Madinatul Bahar iliyopo Mbweni Unguja. Seminahiyo imeandaliwa na Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) na kudhaminiwa na TCRA. WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Rahma Kassim Ali, akifungua semina kwa Makatibu Wakuu na Wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi kuhusu dhana ya wasambazaji maudhui katika utangazaji iliyofanyika katika hoteli ya Madinatul Bahar iliyopo Mbweni Unguja. Semina hiyo imeandaliwa na Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) na kudhaminiwa na TCRA.  MWENYEKITI wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi, Mohammed Ahmada Salum, akitoa neno la shukrani katika semina kwa Makatibu Wakuu na Wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawa

Wanufaika TASAF wataja mafanikio

Image
NWANDISHI WETU, PEMBA WANUFAIKA wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF), kisiwani Pemba wamesema miradi waliyoibua imewakomboa kiuchumi na kumudu gharama za kusomesha watoto wao skuli. Walisema miradi mingi waliyoianzisha kutokana na ruzuku wanazopokea kupitia mpango huo , imewatoa kutoka katika dimbwi la umasikini na sasa wana uhakika wa kupata kipato cha kujikimu kimaisha. Mmoja ya wanufaika hao, Bahati Vuai Haji wa kijiji cha Kwareni Vitongoji, mkoa wa Kaskazini Pemba alieazisha biashara ya mgahawa wa chakula, alisema kuwa kabla ya kuwezeshwa na TASAF hali yake kiuchumi ilikuwa ngumu. Alisema baada ya kupitia ruzuku hiyo aliweka akiba na kuanzisha biashara ya bagia na kujiunga katika vikundi vya kuweka na kukopa hatimaye kuazisha mgahawa wa chakula (Mamantilie) ambapo kwa sasa ndio kazi inayoendesha familia yake ya watoto watano.  “Nashukuru hivi sasa napata fedha familia yangu inapata huduma ya chakula na nyengine maan

Daraja la TASAF lapunguza utoro wa wanafunzi Mjini Wingwi

Image
NA MWANDISHI WETU, PEMBA WANANCHI wa vijiji vya Chupwe, Sebudawa na Mjini Wingwi wameleeza kuwa ujenzi wa daraja linalounganisha vijiji hivyo umepunguza utoro wa wanafunzi na upatikanaji wa huduma nyengine za jamii. Akizungumza na waandishi wa habari waliofika ktika shehia ya  Mjini Wingi, wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba , Mwalimu dhamana wa skuli hiyo, Juma Khamis Kombo, alisema kabla ya kujengwa kwa daraja hilo, utoro wa wanafunzi ulikua mkubwa. Alisema baada ya kukamilika kwa daraja hilo lililojengwa kupitia miradi ya jamii ulioibuliwa na wananchi wa shehia hiyo, mahudhurio ya wanafunzi yameimarika. “Awali wanafunzi walikuwa wanashindwa kufika skuli kikawaida kutokana na kushindwa kuvuka kutoka katika makaazi yao na kwenda skuli hasa katika msimu za mvua,” alieleza mwalimu huyo. Aliongeza kuwa awali wananchi walipanga magogo ili kuvuka kutoka eneo moja kwenda jengine kwa ajili ya shughuli za kijamii wakiwemo wanafunzi ambao walikuwa wakianguka na madaftari yao

NMB yakabidhi gawio la 30.7b/- serikalini

Image
NA MWANDISHI WETU, DODOMA MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, ameyataka mashirika ambayo serikali ina hisa kuhakikisha yanatoa gawio la serikali pamoja na taasisi zinazotakiwa kutoa asilimia 15 ya mapato ghafi kwa mujibu wa sheria zifanye hivyo kwa wakati. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa hafla ya kupokea gawio la shilingi bilioni 30.7 kutoka kwa benki ya NMB iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Juni 15 2022. Alisema mashirika yanayotegemea ruzuku kutoka mfuko mkuu wa serikali yanapaswa kuwa na   mikakati madhubuti inayotekelezeka ili kupunguza utegemezi kwa serikali na kumuagiza   Msajili wa Hazina kuhakikisha   wakuu wa taasisi hizo wanatekeleza maagizo hayo. Dk. Mpango alieleza kuwa, serikali itaendelea kuweka mazingira endelevu ya biashara kwa sekta ya fedha nchini na kuipongeza benki ya NMB kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii sambamba na kusaidia ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa kuimarisha mifumo ya ukusany