Posts

Showing posts from August, 2020
Image
Ayoub ahimiza wazazi, walezi kushirikiana kuinua elimu NA MWANDISHI WETU MKUU wa mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud WAZAZI na walezi wamehimizwa kuzidisha mashirikiano na walimu ili kuimarisa kiwango cha elimu na ufaulu wa watoto wao. MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud, ametoa wito huo wakati wa mahafali ya kwanza ya wananfuzi wa kidatoncha pili wa skuli ya sekondari Ghana iliyopo katika shehia ya Ghana, wilaya ya Kati mkoani humo. Alisema ushirikiano kati ya pande mbili hizo ni nyenzo muhimu katika kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi pamoja na kufanikisha malengo ya walimu ambayo ni kuongeza ufaulu wakati wa mitihani ya taifa. Alisema, kamati ya maendeleo ya elimu ya shehia hiyo imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha inaanza ujenzi wa madarasa mengine mapya ili kusudi kuhamasisha wengine kuchangia ujenzi wa madarasa hayo. Hivyo, aliwataka wananchi kuchangia miradi ya kijamii ikiwemo ujenzi wa madarasa katika skuli hiyo na kuahidi kuwa ata washau