Posts

Showing posts from August, 2021
Image
Kunambi ashukuru mchango wa NMB kuimarisha huduma za jamii NA SHADYA SAID, WMA MKUU wa wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi, ameshukuru mchango unaotolewa na sekta binafsi katika maendeleo ya huduma za jamii wilayani humo katika nyanja tofauti. Alieleza hayo wakati akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa mabati 200 na vitanda 30 kwa ajili ya skuli na vituo vya afya wilayani humo kutoka kwa benki ya NMB, hafla iliyofanyika katika skuli ya Msingi Mbuzini. Alisema   msaada wa mabati   unakwenda kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa katika skuli ya Mbuzini   na   skuli ya Mtoni Kigomeni kwani baadhi ya madarasa yamekuwa yakihitaji kuezekwa ili kukamilisha ujenzi wa madarasa ulioanza mwaka 2017. “Kuchelewa kukamilika kwa madarasa haya kumesababisha wananfunzi kusoma nje ya madarasa na vitanda hivi vinakwenda kuongeza maeneo ya kupumzikia na kujifungulia katika vituo vyetu vya afya jambo ambalo ni la kushukuriwa sana,” alisema Kunambi. Aidha aliziomba taasisi nyengine
Image
NMB yaipa Kusini Unguja msaada wa zaidi ya 25m/- NA MWANDISHI WETU MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid ameipongeza benki ya NMB kwa misaada mbali mbali wanayotoa kwa jamii hapa Zanzibar. Alisema wananchi wa maeneo mbali mbali wamekuwa wakilalamikia changamoto za kijamii, ikiwemo sekta ya elimu kukosekana kwa madarasa ya kusomea baadhi ya madarasa kuvujisha hivyo misaada iliyotolewa na benki hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondosha changamoto hizo. Rashid alieleza hayo juzi wakati akipokea vifaa vya kuezekea skuli za mkoa huo na vitanda kwa ajili ya kujifungulia mama wajawazito ili kuwasaidia kwa namna moja ama nyengine. Alisema msaada huo una thamani ya shilingi milioni 25 utatumika kuezekea skuli tatu kwa mkoa huo ikiwemo ya Kizimkazi, Makunduchi na Binguni. “Serikali ya Mapinduzi imekua ikithamini na kutambua misaada inayotolewa na wadau wa maendeleo kama benki ya NMB kwani imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za wananchi wetu,” alieleza
Image
Waandishi andikeni habari zinazoepusha madhara  NA MWAJUMA JUMA WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuepusha madhara kwa watu wengine. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Abdallah Abdulrahman Mfaume, wakati akifungua mkutano wa kukusanya maoni ya kutengeneza kanuni za maadili ya uandishi wa habari na maudhui ya mitandaoni, uliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, uliomo katika jengo la ZURA, Maisara Zanzibar. Amesema katika uandishi na utangazaji wa habari kupitia vyombo habari mbali mbali, kuna haja ya kuzingatiwa kwa ustaarabu na utamaduni wa nchi badala ya kuiingiza usataarabu wa mataifa mengine sambamba na kuzihakikisha habari zinazitolewa. “Kila nchi ina sheria na kanuni zinazosimamia maswala ya habari pamoja na yale masharti ya jumla ya kitaaluma, hivyo si vyema vyombo vyetu vikatumia kanuni za nchi nyengine na ndio maana taasisi zetu kama UTPC (Muungano wa K
Image
  HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS   WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE HAFLA YA   KUSAINI HATI ZA KUONDOA HOJA ZA MUUNGANO ZILIZOPATIWA   UFUMBUZI TAREHE 24 AGOSTI, 2021- ZANZIBAR   Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Waheshimiwa Mawaziri wa SMT na SMZ, Waheshimiwa   Naibu Mawaziri wa SMT na SMZ, Mwanasheria Mkuu wa Serikali – SMT, SMZ Katibu Mkuu Kiongozi - SMT, SMZ Makatibu Wakuu - SMT, SMZ Wanahabari, Mabibi na Mabwana. Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Ndugu Wajumbe,   naomba nianze kwa kufuata mfano wa wenzangu walionitangulia, kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha kukutana hapa tukiwa na afya njema katika siku hii muhimu kwa mustakabali wa Muungano wetu. Ningependa pia kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kunikabidhi kijiti hiki cha kusimamia masuala ya Muungano, akiwa ameacha msingi mzuri wa kuendelea kut