Posts

Showing posts from March, 2022
Image
GeSCI kuzindua mpango kuimarisha elimu Tanzania NA MWANDISHI MAALUM MPANGO kutathmini utungaji na utekelezaji wa sera za elimu nchini Tanzania unatarajiwa kuzinduliwa Machi 24, 2022 katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Zanzibar. Taarifa iliyotolewa na taasisi ya Global e-Schools and Communities Initiative (GeSCI), ameeleza kuwa mpango huo unaotekelezwa na chuo kikuu cha Makerere, Uganda na Kituo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Notre Dame, umelenga kufanya tafiti, tathmini na kutafsiri sera za ufundishaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa hiyo imeeleza kuwa kupitia mpango wa Tathmini ya Kurekebisha sera za kufundishia (ADAPT), utafiti unafanyika ili kufikia malengo ya kutoa mafunzo kitaifa na kikanda ili kuimarisha maamuzi ya kitaifa yanayotokana na takwimu. Katika uzinduzi huo, miongoni mwa wageni watakaohudhuria na kuwasilisha taarifa na mada ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tanzania Bara Prof. Eliamini Sedoyeka, Katibu Mkuu Wizara ya
Image
KILELE SIKU YA VIWANGO AFRIKA Uzalishaji, usafirishaji bidhaa uzingatie viwango kulinda afya NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban, ameeleza kuwa katika kushajihisha ukuaji wa biashara, uzalishaji, uagiziaji na usafirishaji bidhaa unapaswa kuzingatia viwango na ubora vilivyowekwa. Alieleza hayo jana katika hotuba iliyoso mwa kwa niaba yake na Katibu Mtendaji wa Baraza la Leseni Zanzibar, Rashid Ali Salim, katika kilele cha maadhimisho ya siku ya viwango Afrika iliyoadhimishwa ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein katika jengo la mamlaka ya udhibiti wa maji na nishati Zanzibar (ZURA). Alieleza kuwa bidhaa zenye viwango, zinazokubalika katika biashara za kimataifa kwani zina uhakika wa kulinda afya za watumiaji na mazingira. Alieleza kuwa utumiaji wa bidhaa zilizo chini ya kiwango hupelekea athari nyingi zikiwemo za kimazingira na kuzagaa ovyo kwa takataka zinazotokana na bidhaa hizo. Aidha aliwakumbusha viongozi na watendaji wa Taasisi ya Viw
Image
  SMZ kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI NA SABIHA KHAMIS, MAELEZO WAZIRI wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui amesema wizara hiyo inakusudia kuimarisha maabara na kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa sekta ya afya, ili wafikie lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi. Akizungumza na ugeni kutoka Shirika la misaada la Marekani  ofisini kwake Mnazi Mmoja, alisema kuimarisha maabara na kuwapatia mafunzo wafanyakazi kutasaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI. Alisema wafanyakazi watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufanya utafiti ili kuongeza kiwango cha utoaji huduma na kuimarisha sekta ya afya nchini, hasa katika kukabiliana na ugonjwa huo. “Katika kuwajenga kuimarisha huduma za afya kwa wananchi ni kuwajengea uwezo wafanyakazi wa kufanya utafiti ambao utasaidia kutoa huduma bora kwa jamii”, alisema Mazrui. Alifahamisha kuwa kupitia shirika hilo wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na UKIMWI nchini, hivyo aliomba kuwepo na ushirikiano   wa   kutosha ili kutokomeza j
Image
  DK. MWINYI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI KWARARA KIDUTANI RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, machi 21, 2022 ameweka jiwe la msingi mradi wa uhuishaji na uimarishaji wa mfumo wa usambazaji maji Zanzibar, huko Kwarara Kidutani, ikiwa ni shamrashamra za wiki ya maji duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 22 ya kila mwaka. Akizungumza katika hafla hiyo ali sema upatikanaji wa huduma za maji safi na salama katika maeneo yote ya Zanzibar ni miongoni mwa vipaumbele vya serikali anayoiongoza. Aidha alisema jitihada zinazochukuliwa na serikali ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2020 - 2025, mipango mikuu ya maendeleo na ahadi alizozitoa wakati wa  kampeni.   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiondoa kitambaa kuweka jiwe la msingi mradi wa uhuishaji na uimarishaji wa mfumo wa usambazaji maji Zanzibar huko Kwarara Kidutani, wilaya ya Magharibi ‘B’ Un
Image
 RAIS SAMIA APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Profesa Rwekaza Mukandala Ikulu Jijini Dar es Salaam Machi 21, 2022. RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wajumbe wa Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa mara baada ya kupokea taarifa yao Ikulu Jijini Dar es Salaam Machi 21, 2022.   BAADHI ya Wajumbe wa Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kupokea Taarifa yao Ikulu Jijini Dar es Salaam Machi 21, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi cha kuratibu Ma
Image
Watendaji OMKR wakiwa kuongeza ubunifu NA RAYA HAMAD, OMKR WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dkt. Saada Mkuya Salum (katikati), amewataka Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar kuendelea kuwa wabunifu ili kwenda sambamba na maono ya Serikali ya awamu ya nane ya kutimiza matarajio ya kuwatumikia vyema wananchi. Dkt. Mkuya ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya ofisi baina yake na Waziri mpya wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Harous Said Suleiman kufuatia mabadiliko ya baraza la Mapinduzi   yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi hivi karibuni. Amesema kwamba wananchi wanamatarajio makubwa ya Serikali ya awamu ya nane katika utekelezaji wa sera na mipango mbali mbali ya maendeleo na kwamba ni vyema wafanyakazi kujitahidi kwenda sambamba na matarajio hayo. Hata hivyo, Dkt Saada amewakumbusha watendaji hao pia kujitahidi kuenda na muda kwa kuzingatia   wakati katika utekelezaji wa shughuli za k