Posts

Showing posts from February, 2023

Simamieni ubora wa bidhaa zinazoingia kuimarisha uzalishaji – Omar

Image
NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban, ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) kufanikisha malengo iliyojiwekea likiwemo la kudhibiti bidhaa zilizo chini ya viwango kuimarisha uzalishaji wa ndani. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo katika ofisi za ZBS Maruhubi, Omar aliwataka wajumbe bodi na uongozi kuhakikisha wanashirkiana kukamilisha majukumu yaliyomo katika mpango kazi wa taasisi ikiwemo ujenzi wa ofisi na maabara katika kisiwa cha Pemba. Aidha aliipongeza bodi hiyo iliyoteuliwa kwa kipindi cha pili kwa kukamilisha ujenzi na upatikanaji wa jengo la ofisi na maabara za kisasa hali iliyoongeza ufanisi wa taasisi kwa wadau wake. “Sitarajii kuona kunakua na mvutano baina ya bodi na ‘management’ (uongozi) bali natarajia mtaendelea kushirikiana kuleta mafanikio zaidi katika siku za usoni,” alieleza Omar. Waziri shaaban akisisitiza jambo Aliwataka wajumbe wa bodi hiyo wanaotoka katika taasisi za serikali na binaf