Posts

Showing posts from April, 2023

Dk. Mwinyi aongoza viongozi, wananchi kumuombea mzee Karume

Image
  NA MWANDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi jana amewaongoza wananchi wa Zanzibar, katika dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume aliyefariki dunia Aprili 7 mwaka 1972. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu mzee karume. Dua hiyo iliyoanza majira ya saa 3:00 asubuhi ilifanyika katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali kutoka serikali zote mbili na viongozi wa chama cha Mapinduzi. Mara baada ya kumalizika kwa kisomo cha dua, Dk.   Mwinyi alianza kuweka shada ya maua katika kaburi la mzee Karume, akifuatiwa Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, mabalozi na Ali Abeid Amani Karume akiwakilisha familia.   MTOTO wa marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu mzee kar