Posts

Showing posts from March, 2021
 
Image
Siku ya uhuru wa habari kuadhimishwa kimkakati Zanzibar NA ASYA HASSAN UMOJA wa Taasisi za Waandishi wa Habari Zanzibar, kupitia kamati maalum, unatarajia kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa kutoa tunzo kwa waandishi watakaoandika habari zitakazotoa matokeo chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Farouk Karim, alieleza hayo jana katika mkutano na waandishi wa habari, katika ukumbi wa Idara ya Mawasiliano na Taaluma za Habari ya chuo kikuu cha Zanzibar (SUZA), Kilimani wilaya ya Mjini Unguja. Alisema hatua hiyo itasaidia waandishi kuongezea ujuzi, kujiamini, kujituma na kuongeza ubora katika kazi zao. Alifahamisha kwamba tunzo hizo ambazo zimeegemea katika maeneo makuu matano ambayo ni uandishi wa habari za uchumi wa buluu iliyopewa jina la ‘Dk. Hussein Mwinyi Award’, Uandishi wa Habari za Jinsia (Mama Mariam Mwinyi Award), Uandishi wa Habari za Serikali ya Umoja wa Kitaifa (Maalim Seif Award), Uandishi wa Habari za Rushwa na uwajibikaji
Image
ZPC yaomboleza kifo cha JPM NA MZEE GEORGE WAKATI mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, marehemu Dk. John Magufuli ukifikishwa katika kijiji chao cha Chato mkoani Geita, wananchi na viongozi wa ngazi mbali mbali wamejitokeza kusaini vitabu vya maombolezo vilivyowekwa katika maeneo mbali mbali nchini. Miongoni mwa wananchi na viongozi  waliofanya hivyo jana ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, alieweka saini katika vitabu hivyo vilivyowekwa katika Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui na ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil. Kwa upande wa viongozi wa asasi za kirai, Katibu Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar, Mwinyimvua Nzukwi ambae aliweka saini katika vitabu hivyo Machi 24, 2020  na kueleza kusikitishwa kwao na kifo hicho. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Nzukwi alieleza kuwa kifo cha Dk. Magufuli ni pigo na kwamba kimeacha pengo katika ujenzi wa taifa. Alieleza kuwa Dk. Magufuli licha ya kuwa
Image
Wasaidieni wananchi kufikisha malalamiko uvunjifu haki za binadamu - Awami RAHMA KHAMIS NA ISSA MZEE, MAELEZO Waandishi wa habari Nchini wametakiwa kutoa habari zinazohusu uvunjifu wa haki za binaadamu ili kuwasaidia wananchi kufikisha malalamiko yao sehemu husika ili kukuza ustawi wa jamii nchini.   Akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari katika warsha iliyoandaliwa na Mkufunzi kutoka  Shirika la Waandishi wa Habari wa  Haki za Binaadamu, Sami Awami, (aliesimama) katika Hoteli ya Golden Tulip, Kibweni alisema ipo haja kwa waandishi wa habari kupata mafunzo hayo ili kusaidia upatikananji wa haki za binadamu nchini. Akiwasilisha mada ya haki za bindamu na ugonja wa corona amesema kuibuka kwa maradhi hayo duniani, kumesababisha kutokea kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu kwa baadhi ya raia wa mataifa jambo ambalo limeleta athari kubwa kwa watu wengi hasa wananwake na watoto. Akitoa mfano wa vitendo hivyo, vimejitokeza baada ya kuwekwa karantini iliyowekwa kwa baadhi ya ma
Image
Dk. Mwinyi awataka wananchi kuwa watulivu kifo cha JPM NA MWANDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Watanzania kuwa watulivu kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, Dk. Mwinyi pia alituma salamu za rambirambi kuwataka kuwa na moyo wa subira Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Mjane wa marehemu Mama Janeth Magufuli, familia yake na wananchi Tanzania. Alisema kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wananchi wote wa Zanzibar anatoa salamu hizo na kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. “Huu ni msiba mzito sana kwangu na kwa taifa letu la Tanzania, hivyo nakuombeni tuwe na subira na tuwe watulivu,” alieleza Dk. Mwinyi katika taarifa yake. Dk. Magufuli alifariki jioni ya Machi, 17 mwaka huu kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena
Image
Zanzibar     yaadhimisha s iku ya ustawi kimataifa kwa mara ya kwanza  Maafisa ustawi, wadau watakiwa kuzingatia maadili NA KHAMISUU ABDALLAH SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imesema inathamini juhudi na mchango unaotolewa na maofisa ustawi wa jamii katika kusaidia jamii iliyowazunguka.     Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Ali Mohammed, katika hotuba yake ya kilele cha maadhimisho ya ustawi duniani iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi, katika ukumbi wa shekh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Machi 16 mwaka huu. Maadhimisho hayo yanayofanyika kila Jumanne ya tatu ya mwezi wa tatu, Masoud alisema serikali  itaendelea kuwashika mkono na kutambua mchango wa Maafisa ustawi wa jamii kwani ni watu muhimu katika jamii. Alisisitiza kwamba serikali imelenga kuimarisha ustawi wa wananchi wa Zanzibar kama yalivyokuwa madhumuni ya mapinduzi ya Zanzibar. Alibainisha kuw
Image
  TASAF kujenga wodi ya akina mama, maabara zahanati ya Mkambarani NA JAMES MWANAMYOTO, MOROGORO NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, (pichani) ameiahidi Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, kwamba kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) serikali itajenga wodi ya kuwahudumia akina mama wajawazito na maabara katika zahanati ya kijiji cha Mkambarani ili wananchi hao wapate huduma bora za afya. Ndejembi ametoa ahadi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya kamati hiyo iliyoelekeza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kujenga jengo la kina mama kwa ajili ya kuwapatia huduma stahiki, ikiwa ni pamoja na kujenga maabara itakayotoa huduma bora na vipimo wananchi wa Mkambarani. Amesema, kutokana na maelekezo yaliyotolewa na kamati ofisi yake itajenga wodi ya akina mama ili kuwe na faragha wakati wa kuwahudumia akina mama wajawazito. Kuhusu maelekezo ya ujenzi wa maabara, Ndejembi ameihakikis
Image
Msi sambaze habari zilizothibitishwa - Mfaume NA MWANDISHI MAALUM WATUMIAJI wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari nchini wametakiwa kutosambaza habari zisizothibitishwa ili kuepuka kuingia katika migogoro ya kisheria. Mjumbe wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abdallah Abdulrahman Mfaume, (pichani aliesimama) alitoa wito huo wakati akifungua mkutano wa majadiliano iliyowakutanisha wadau mbali mbali wa habadi na jumuiya za kiraia zinazohusika na maendeleo ya vijana Zanzibar. Alisema maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani yameongeza wigo wa utoaji na usambaji wa habari na taarifa hivyo ipo haja ya kuchukuliwa kwa hatua za tahadhari ili kuepusha madhara kwa jamii. Alisema kazi ya usambazaji na utoaji wa habari nchini unasimamiwa na sheria, kanuni na muongozo hivyo kuna umuhimu wa kuzingatiwa wwledi katika dhana ya uandishi wa habari. "Upashanaji wa habari katika nchi yeyote unasimamiwa na sheria na kanuni na sio kila mtu anaweza kuifanya
Image
UNDP kushirikiana na   SMZ  kuendeleza miradi ya uchumi NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali (pichani), amefanya mazungumzo na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la   Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Christine Musisi na kujadiliana namna shirika hilo litakavyosaidia miradi ya maendeleo ya kukuza uchumi wa Zanzibar. Mazungumzo hayo yamefanyika jana, katika Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ zilizopo katika ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, jijini Dar es Salaam.   Jamal alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibari itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo wa ndani na nje ikiwemo UNDP, kusaidia uwajibikaji na utendaji kazi wa serikali kwa ufanisi kama alivyoagiza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar wa   awamu ya nane Dk. Hussein Ali Mwinyi. Alisema Zanzibar imejipanga katika kuimarisha uwajibikaji na utendaji kazi kwa wafanyakazi wake ili kuhakikisha nchi inafikia malengo yaliyowek
Image
  Waziri ataka wanawake kuinua sekta ya utalii NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale, Lela Mohammed Mussa, amewataka wanawake kuungana kuitetea jinsia yao na kuachana na mila za kuamini kuwa kufanya kazi katika sekta ya utalii kwa wanawake ni kinyume na utamaduni. Akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Machi 8, mwaka huu iliyoandaliwa na hoteli ya Park Hyatt, ikiwa na lengo la kuwahamasisha wanawake kuunga mkono katika shughuli mbali mbali zikiwemo za kisiasa na kijamii. Alisema jamii ya Wazanzibari imekuwa ikitawaliwa na dhana mbaya kuhusiana na sekta hiyo kiutalii lakini jamii hiyo ya wanawake inajitambua na imeonekana kufanya vizuri katika ajira mbali mbali bila ya kuharibu mila, silka, desturi na tamaduni zao. Aidha alisema utafiti uliofanyika duniani unaonesha kuwa dhamana nyingi walizopewa wanawake kuzifanyia kazi wamekuwa wakifanya vizuri zaidi kuliko wanaume. Hivyo, alisema kuwa hakuna haja ya kuendelea kuvunjana moyo na ba
Image
  Soraga ahimiza mafunzo kwa watendaji kuongeza ufanisi  NA SHARIFA MAULID, WNARKUU WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga, ametilia mkazo suala la kupatiwa mafunzo wafanyakazi ili kuwajengea uwezo wa utakaoimarisha utendaji katika maeneo yao. Ameeleza hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Idara ya Utumishi na Uwendeshaji ya wizara hiyo juu ya utekelezaji wa majukumu   yao katika ukumbi wa wizara yake Mwanakwerekwe, wilaya ya Magharib ‘B’. Alisema katika utekelezaji wake, Wakurugenzi wa idara hiyo waangalie mahitaji na sio kupewa mtu mmoja kila inapotokea nafasi za mafunzo ili kuondosha manung’uniko miongoni mwa wafanyakazi. Soraga aliwataka viongozi na wafanyakazi kufuata taratibu za kazi, muongozo   wa sheria za kazi na maagizo yanayotolewa na serikali kwa lengo la kuweka mustakabali mzuri utaopelekea ufanisi wa majukumu   ya kila mmoja na maendeleo ya wananchi kwa ujumla. Hivyo aliutaka uongozi wa Idara hiyo kuhakikisha wafany
Image
  Ayoub ataja vipaumbele Kaskazini Unguja, apiga marufuku ‘vigodoro’ MWASHUNGI TAHIR, MAELEZO  MKUU wa Mkoa Kaskazini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud, ameeleza kuwa serikali ya huo umelenga kukuza sekta ya utalii kwa kuvitangaza na kuviendeleza vivutio vya utalii vilivyomo mkoani humo. Ayoub alieleza hayo ofisini kwake Mkokotoni, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia utekelezaji wa kazi za serikali ya mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Alieleza kuwa mkoa huo una vivutio vingi na maeneo ya mahoteli na mikahawa mikubwa, fukwe zinazovutia na maeneo ya kihistoria ambayo wageni na wenyeji wanapasa kuyajua. Aliongeza kuwa pamoja na kuimarisha sekta hiyo, katika kipindi cha miaka mitano pia mkazo zaidi utawekwa katika ukuzaji wa sekta zinazokuza ustawi wa jamii zikiwemo za kilimo, mifugo, maji safi na salama, elimu, afya, miundombinu ya barabara na michezo. “Pia kwa kuzingatia mipango ya serikali kuu, serikali ya mkoa itaendelea kuhamasisha ujenzi wa v
Image
Vijana watakiwa kutumia vyema mitandao ya kijamii NA MADINA ISSA MKURUGENZI Mtendaji wa Jumuiya wa Jukwaa la Vijana Zanzibar Zanzibar Youth Forum (ZYF), Maulid Suleiman, (pichani aliesimama) amewataka vijana nchini kutumia mitandao ya kijamii ipasavyo, ili kuepusha kuleta athari kwa mbalimbali kwa jamii. Maulid alitoa wito huo jana wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana kupitia mradi wa kukuza ushiriki wa asasi za kiraia katika sheria na uhuru wa msingi wa vyombo vya habari, yaliyofanyika katika ukumbi wa kitengo cha kudhibiti malaria Mwanakwerekwe Mjini Unguja. Alisema vijana wengi wanatumia vibaya mitandao hiyo na kusababisha migogoro ndani ya jamii. Alisema ni vyema kwa vijana hao kutumia mitandao hiyo kwa kutoa taarifa sahihi ambazo zitaleta mafanikio nchini na kufikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kuelimisha jamii hasa wanaotumia mitandao ya kijamii. Aidha alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuwajengea uwezo taasisi zisizo za kiserikali na ushiriki na utetez
Image
Dk. Mkuya ahimiza uwajibikaji taasisi zilizo wizarani kwake RAYA HAMAD, OMKR WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum,   amewataka watendaji na wafanyakazi wa Tume ya Kuratibu na Udhubiti wa Dawa za Kulevya, kuongeza juhudi zamapambano dhidi ya wanaoingiza, kuuza na kusambaza kwa maslahi ya Zanzibar Dk. Saada ameeleza hayo alipokutana na uongozi na wafanyakazi wa tume hiyo na kuwasisitiza kuwa waadilifu na waaminifu kwa vile ya matumizi ya dawa za kulevya ni kero katika jamii na mtandao wake ni mkubwa Ameeleza kuwa katika kusimamia vyema utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo Dk.   Saada, amewataka kuzidisha mashirikiano na taasisi mbalimbali wanazofanya kazi kwa ukaribu ikiwemo Uwanja wa ndege, Bandarini,   kikanda, kitaifa na kimataifa na kusambaratisha mitandao wa wahalifu Pia amewakumbusha kuwa hivi sasa fursa nyingi za maendeleo zinapatikana zikiwemo utalii ujenzi wa miundo mbinu ambazo zimekuwa zikiibua fursa mbali mbali za kiuc
Image
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Samia ataka wadau kutathmini mafanikio yaliyofikiwa Asema agenda ya usawa wa jinsia inahitaji mashirikiano Aipongeza FAWE kuchochea kasi ya maendeleo ya elimu NA MWANDISHI WETU MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka wadau wa masuala ya jinsia nchini kuitumia siku ya kimataifa ya wanawake duniani kufanya tathmini na kuweka mikakati ya kusukuma mbele agenda ya maendeleo ya jinsia badala ya kulalamika. Ameeleza kuwa kufanya hivyo kutachochea kasi ya mendeleo ya wanawake duniani kwani siku hiyo inatoa fursa kwa serikali, taasisi zisizo za serikali na wadau kupima utekelezaji wa harakati za kumjengea uwezo na kumkomboa Mwanamke na mtoto wa kike. Makamu wa Rais alieleza hayo juzi usiku katika harambee iliyoandaliwa na Jumuiya ya kuwawezesha wanawake Zanzibar (FAWE) ikiwa ni sehemu ya madhimisho ya siku ya wanawake duniani inayofikia kilelele chake leo, iliyofanyika hoteli ya Serena mjini Unguja. Alisema ili kuhak