Posts

Showing posts from January, 2022
Image
NMB, Mambo ya kale wakubaliana kuimarisha utalii Zanzibar  NA MWANDISHI WETU WIZARA ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar imetiliana saini makubaliano ya  kuimarisha shughuli za watembeza watalii na benki ya NMB kwa kutoa mafunzo ili kurasimisha shughuli zao waweze kukopesheka. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Fatma Mabrouk Khamis, alitia saini kwa niaba ya wizara hiyo huku Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi  Filbert Mponzi aliiwakilisha benki y a NMB. Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo, Fatma alisema benki makubaliano hayo yamelenga kuinua shughuli za vijana wanaotembeza watalii nchini. Alieleza kuwa mitaani kuna vijana wengi wanaofanya kazi ya kuongoza watalii bila ya ujuzi wa kutosha hivyo kuharibu taswira ya Zanaibar hivyo makakati huo utawasaidia kuimarishawa ujuzi na maarifa yao. “Wapo vijana wanaojihusisha na utalii mfano ‘beach boys’ ambao wanafanya utalii wa mikobani na mara nyingi wanakuwa kero kwa wageni. Kupitia makubaliano haya, tutawapa mafunzo
Image
  Andikeni habari zitakazotatua migogoro – Mfaume KHAMISUU ABDALLAH NA MADINA ISSA WAANDISHI wa habari nchini wameshauriwa kuwa sehemu ya utatuzi wa migogoro ili kuifanya jamii kuwa na mshikamano utakaosaidia kuondoa tofauti hasa za kisiasa na kuharakisha maendeleo ya nchi. Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), Abdalla Abdulrahman Mfaume, alieleza hayo jana wakati akifungua mafunzo ya uandishi wa habari za utatuzi wa migogoro na ujenzi wa amani kwa wanahabari wa vyombo mbali mbali yaliyofanyika katika ukumbi wa Kitengo cha Uzazi Shirikishi, Kidogochekundu Mjini Unguja. Alisema Zanzibar inakabiliwa na migogoro mingi ikiwemo ya ardhi, kijamii, kiuchumi, kidini na kisiasa hivyo ikiachwa bila ya kuripotiwa katika vyombo vya Habari, itashindwa kupatiwa ufumbuzi. Alisema kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa, mara nyingi waandishi wa habari hujikita zaidi katika uandishi wa habari za siasa kipindi cha uchaguzi tu hali inayochangia uwepo wa migogoro hiyo. “Ikiwa tu