Posts

Showing posts from August, 2022

Wanahabari waombwa kuhamasisha chanjo ya UVIKO 19

Image
NA ASYA HASSAN MENEJA Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kutokana Wizara ya Afya Zanzibar, Bakar Hamad Magarawa, amesema vyombo vya habari vina wajibu wa kuendelea kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya ya UVIKO - 19. Alisema hayo alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano wa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya hali halisi ya maradhi hayo na upatikanaji wa chanjo yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kwa kushirikiana na Internews. Alisema lengo la serikali hadi kufika Disemba mwaka huu asilimia 70 ya wananchi wawe tayari wamechanjwa lakini hadi sasa waliochanjwa ni asilimia 35, hali inayoonesha kwamba kuna kundi kubwa halijahamasika kupata kinga hiyo. Sambamba na hayo alifahamisha kwamba licha ya serikali na waandishi wa habari kufanya kazi kubwa ya kuihamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuchanja bado jamii haijaona umuhimu huo. Alisema kwa sasa vipo vituo zaidi ya 120 vinavyotoa chanjo hizo katika maeneo mbalimbali, hivyo aliiomba jamii ikavitumia ipasa

Mwenyekiti CCM awazawadia watoto waliozaliwa siku ya sensa

Image
NA  MWANDISHI WETU MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa Mjini (Kichama), Talib Ali Talib, ameitaka jamii kujenga tabia ya kutembelea wagonjwa wakati wa matukio maalum ya kitaifa ili kuimarisha imani na mappenzi miongoni mwao. Talib alieleza hayo alipotembelea wodi za wazazi za hospitali ya Mnazimmoja na Mwembeladu, mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na kukabidhi zawadi mbali mbali kuwapongeza wazazi hao na kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makaazi lililoanza jana. Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Talib alisema alisema pamoja na kuhamasisha ushiriki wa makundi yote kwenye sensa, ametoa zawadi hizo kushereheka siku yake ya kuzaliwa pamoja na watoto hao. Alisema watoto waliozaliwa katika siku hiyo watakuwa na historia kubwa nchini na kwamba watalikumbuka zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya nchi na ustawi wa watu wake. “Hawa ni miongoni mwa watanzania walioingia kwenye hisabu kupitia sensa hii hivyo bila shaka watakuwa na kumbukumbu isiyosahaulika kama ilivyo kwa watu w

Mhandisi Zena ahimiza ushiriki wa vijana katika maendeleo

Image
NA MWANDISHI WETU KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, amewahimiza vijana kushiri utekelezaji mradi wa ‘Kijana imara’ ili kutatua changamoto zinazowakabili. Akifungua mdahalo wa ‘Kijana Imara Transformative’, ulioandaliwa na Shirika la Kiona Youth Coordinates (KYCo) katika hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar, alisema mradi huo utasaidia kubadili mitazamo ya watu juu ya masuala ya vijana. Alisema vijana ni kundi kubwa katika jamii hivyo kuna umuhimu wa kuunganisha mawazo na nguvu zao ili kuepuka kupeleka nguvu zao katika mambo yasiyo na tija. “Kwa kuzingatia kuwa vijana ni kundi kubwa hivyo kama hatutakuwa na njia nzuri ya kutumia nguvu kwa kweli wataipeleka mahali ambapo sio sahihi na matokeo yake tunaweza kuharibikiwa,” alieleza. Akizungumza katika mdahalo huo uliohudhuriwa na vijana zaidi ya 250 kutoka taasisi mbali mbali za vijana na mabaraza ya vijana, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatm