Posts

Showing posts from November, 2022

TIB yaanika sababu za kuweka riba nafuu mikopo ya kilimo

Image
NA MWANDISHI WETU, MWANZA         BENKI ya Maendeleo Tanzania (TIB) imepongezwa kwa kutoza riba nafuu kwa wakulima na wawekezaji wanaojishughuisha na za uzalishaji, usindikaji mazao na masoko hasa kwa wakopaji wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo hapa nchini.   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Chande (pichani kushoto), wakati alipotembelea banda la benki ya TIB, kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyokua yakifanyika katika viwanja vya Rock City Mall, jijini Mwanza.  Chande alionesha kufurahishwa na huduma za mikopo inayotolewa na benki hiyo kupitia dirisha la kilimo linalowalenga wakulima na wawekezaji wenye miradi ya kilimo na ufugaji.  Akiwa bada la benki hiyo, Chande alijulishwa kuwa riba inayotozwa kupitia kwa mikopo hiyo ni asilimia tano kwa mwaka kwa wakopaji wa moja kwa moja toka benki na asilimia 4 kwa upande wa taasisi zinazokopa kwa ajili ya kukopesha ambapo hutatakiwa kukopesha kwa asilimia isiyozidi asili

TIB yawaita wajasiriamali, wawekezaji kuchangamkia mikopo

Image
NA MWANDISHI WETU, MWANZA        BENKI ya Maendeleo Tanzania (TIB) imeitaka jamii kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na benki hiyo ili kuwekeza katika miradi ya maendeleo kwa ajili kuchagiza ukuaji wa uchumi nchini.  Wito huo umetolewa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki hiyo, Giusy Mbolile (pichani kushoto) kwenye maadhimisho ya 'Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa' yanayoendelea katika viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza.  Mbolile alisema kuwa TIB ina wajibu wa kuwezesha upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu na wa kati kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi nchini, hivyo wawekezaji wenye miradi ya kimkakati wanapaswa kuitumia benki hiyo kufanikisha miradi yao.  “Benki ya Maendeleo (TIB) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa malengo ya kuwezesha upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu na wa kati kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi, hivyo nawasihi wawekezaji wenye miradi ya kimkakati kuitumia ili kufanikisha uwekezaji huo,” alisema Mbolile.  Aliongeza kuwa benki hiyo

TMA kujenga vituo saba vya rada

Image
NA SAIDA ISSA, DODOMA MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 imejipanga kujenga vituo vya rada saba pamoja na vifaa vitakavyosaidia kuangaza nchi masaa 24. Akizungumza na waandishi wa habari   jijini Dodoma, Mkurugenzi Huduma za Utabiri wa TMA, Dk. Hamza Kabelwa, kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022/23 amesema kuwa licha ya kuanzisha miradi hiyo, wataalamu wamepatiwa mafunzo   kwa ajili ya kuendesha rada hizo. “Mafunzo kwa wahandisi na waendesha mitambo kuhusu kuzihudumia na kuzitumia rada hizo yalifanyika kiwandani nchini Marekani. Aidha utengenezaji wa rada mbili za mwisho zitakazofungwa KIA (uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro) na Dodoma ulifikia asilimia 45 ambapo mamlaka ilifungua barua ya dhamana kwa ajili ya malipo ya asilimia 80 ya utengenezaji wa Rada hizo,” amesema Dk. Kabelwa. Alifafanua kwamba kukamilika kwa rada hizi kutakamilisha mtandao wa rada nchini kufikia saba rada amba