Posts

Mkakati, mpango kazi kuimarisha mianzi wazinduliwa

Image
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki, amezindua mkakati wa uimarishaji wa miti ya mianzi na kueleza kuwa tafiti zimebaini kuwepo kwa takribani hekta milioni 12.5 zinaweza kuuteshwa miti hiyo nchini ili kuzuia mmomonyoko wa ardhi na kunyonya hewa ukaa. Amesema utafiti huo unaonesha Tanzania inapoteza eneo la misitu yenye ukubwa wa hekta zaidi la 469,000 kila mwaka, hali ambayo sio nzuri na halikubaliki hivyo juhudi za pamoja zinahitajika. Kairuki alieleza hayo jana wakati akizindua mkakati wa kitaifa wa mianzi na mpango kazi wa mkakati huo uliofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii, Dar es salaam. Alisema miti ya mianzi ina nafasi kubwa katika uhifadhi wa mazingira kwa kufyonza hewa ya ukaa (carbondioxide) kwa zaidi ya mara 40, hivyo  zao hilo ni muhimu katika utunzaji wa mazingira na kupunguza  athari za mabadiliko ya Tabianchi. WAZIRI Kairuki akiwa na Katibu Mkuu Abbas, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya  Ardhi, Maliasili na Utal

Ndariananga ahimiza ufanisi taasisi za serikali

Image
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga amesema serikali inahitaji taasisi zake kuongeza ufanisi na tija katika utendaji wake ili kuongeza kasi ya maendeleo katika kukuza uchumi wa watanzania na Taifa kwa ujumla. Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya saba ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji   Wananchi Kiuchumi (NEEC) jijini Dar es salaam na kuitaka bodi hiyo kuwa wabunifu huku wakifanya kazi kwa uadilifu na weledi ili kuchochea ushiriki wa wananchi katika shughuli za kiuchumi nchini. “Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais shupavu Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan imewaamini hivyo ni jukumu lenu sasa kuonesha mchango wenu ikiwa ni pamoja na kusimamia utendaji wa Baraza”, alieleza Naibu Waziri huyo. Aliongeza kuwa; ”Naamini kwa umoja wenu na ushirikiano na Menejimenti ya (NEEC) mtaweza kufanikisha hili na kuleta matokeo chanya katika kukuza uchumi wa Taifa”. Aidha Ummy  amewakumbusha Wajumbe w

Serikali kuandaa mpango wa taifa kukabili madhara ya Elnino

Image
  NA SAIDA ISSA, DODOMA SERIKALI imesema imeendelea kuchukua hatua mbali mbali za kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa ikiwemo Kuandaa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya Elnino kwa kipindi cha mwezi Septemba 2023 mpaka mwezi Juni 2024. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga, Bungeni jijini Dodoma Februari 8, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Mwera, Zahor Mohamed aliyetaka kufahamu kuhusu athari za mvua zilizonyesha Novemba, 2023 na mpango wa serikali kuzuia athari hizo kujirudia. Ummy ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa inaendelea kuzijengea uwezo Kamati za Usimamizi wa Maafa katika mikoa 18 nchini, kufuatilia mwenendo wa majanga, kutoa tahadhari kwa umma kupitia kituo cha oparesheni na mawasiliano ya dharura. “Ili kukabiliana na athari hizi, Serikali imechukua hatua mbali mbali kama vile kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa kupitia

Jumuiya ya madola kuwakutanisha mawaziri wa sheria Z’bar

Image
NA MWANDISHI MAALUM TANZANIA inatarajai kuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa sheria wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola, utakaofanyika visiwani Zanzibar kuanzia Machi 4 hadi mwaka huu. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Pindi Chana, alieleza hayo jana katika ukumbi wa Idara ya Habari wa Bungeni jijini Dodoma, ambapo alisema maandalizi ya mkutano huo wa kimataifa yanaendelea. Alisema katika mkutano huo, Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya sheria kutoka nchi na mataifa 56 wakiambatana na maofisa waandamizi pamoja na wageni takriban 300 kutoka nchi za jumuiya ya Madola wanatarajiwa kuhudhuria. Dk. Chana alisema mkutano huo utajadili mifumo ya kisasa ya uvumbuzi wa kiteknolojia na mambo ya kijidijitali yanavyoweza kusaidia kuongeza ufanisi kwenye tasnia ya sheria na utoaji haki.   “Katika mkutano huo Tanzania tunawania tuzo mbili moja ni usajili wa watoto chini ya miaka mitano na nyingine ni utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Mama Samia legal aid camp

Dk. Khalid ashajihisha mashirikiano kufikia uchumi wa kidigitali

Image
NA MWANDISHI WETU WADAU wa sekta ya mawasiliano na mitandao nchini wametakiwa kuimarisha ushirikiano na mamlaka za serikali ili azma ya mageuzi ya kidigitali ifikiwe. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed, (pichani), ametoa wito huo katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania na kampuni ya usambazaji wa maudhui ya Zanzibar Cable Television (ZCTV) iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Zanzibar. Dk. Khalid alieleza kuwa serikali zote mbili za Tanzania, zimewekeza miundombinu na mazingira rahisi ya kuwezesha taasisi na kampuni za mawasiliano kutekeleza majukumu yao kwa faida. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed, (katikati),  akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa masirikiano ya kibiashara kati ya Airtel Money na ZCTV. Aliongeza kuwa hatua hiyo inalenga kuleta unafuu wa gharama za mawasiliano kwa wananchi lakini pia kurahi

Kazi 529 za kuwania tunzo za umahiri wa takwimu

Image
NA MWANDISHI MAALUM JUMLA ya kazi 529 za waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari zimewasilishwa kwa ajili ya kuwania tuzo za umahiri za uandishi wa habari za takwimu za wanawake na uongozi. Kwa mujibu taaraifa kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake ofisi ya zanzibar (TAMWA ZNZ), imeeleza kuwa kazi hizo ni pamoja na vipindi vya redio, televisheni, makala za magazeti na zile kutoka katika mitandao ya kijamii zilizoandikwa na kurushwa katika vyombo vyao kuanzia mwezi Janauari hadi Disemba 31, 2023. Taarifa hiyo iliyosainiwa na mkurugenzi wa chama hicho Dk. Mzuri Issa, ilifafanua kuwa kazi hizo zinaonesha ni jinsi gani waandishi walivyokuwa na muamko wa kuandika habari za uongozi kwa wanawake. Mkurugenzi huyo alisema kasi hizo zinashajihisha wanawake na vijana wakike kujiamini zaidi na kuwa na matumaini ya kupata nafasi mbali mbali za uongozi lakini pia zinaielimisha jamii kuhusu umuhimu wa wanawake katika uongozi. Dk. Mzuri alisema lengo la tuzo hizo ni kuhi

AfDB kuendelea kukuza uchumi wa Tanzania

Image
NA BENNY MWAIPAJA, DODOMA WAZIRI wa Fedha, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba, amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia Nishati, Dk. Kevin Kariuki na kuishukuru benki hiyo kwa kufadhili miradi 29 ya kitaifa na kikanda, yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 3.84 Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia Nishati, Dk. Kevin Kariuki walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma. Mazungumzo baina ya wawili hao yamefanyika jijini Dodoma ambapo Dk. Nchemba amesema kuwa AfDB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo huku katika miradi hiyo, miradi 26 ni ya kitaifa na mitatu ni ya kikanda iliyopo katika sekta za miundombinu ya barabara, nishati, maji na kilimo.  Amesema kuwa zaidi ya asilimia 13.6 ya fedha hizo zimeelekezwa katika uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme kupitia miradi mitano ambapo mitatu kati ya hiyo ni ya kitaifa na mingine miwil