Posts

Showing posts from December, 2021
Image
Hai yatumia fedha za UVIKO 19 kujenga madarasa 43 NA MWANDISHI WETU, HAI MPANGO wa maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO - 19, umefanikisha ujenzi wa vyumba 43 vya madarasa katika skuli ya sekondari uliogharimu shilingi milioni 860 katika wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro. Mkuu wa wilaya hiyo Hai, Juma Irando (pichani) aliyasema hayo hivi karibuni katika taarifa yake kwa Kamati ya Siasa mkoa wa Kilimanjaro iliyongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Patrick Boisafi walipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na mapambano dhidi ya UVIKO – 19 wananchi 28,877,019 wamepatiwa chanjo ya ugonjwa huo. Irando alisema ujenzi wa madarasa hayo utakamilika kabla ya Disemba 31 mwaka huu na wanafunzi 3,950 wakiwemo wasichana 2,050 na wavulana 1,900 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa kipindi cha Januari mwakani wataanza masomo yao kama serikali ilivyoagiza. Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa huo,   Patrick Boisafi, alimpongeza Rais Samia
Image
  Kairuki ahimiza biashara kati ya Tanzania, China NA MWANDISHI WETU WAFANYABIASHARA wa Tanzania wametakiwa kutumia fursa za uwekezaji nchini china ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi mbili hizo. Wito huo umetolewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mberwa Kairuki (pichani) mara baada ya ziara ya kutembelea viwanda na kampuni za zinazofanya biashara baina ya nchi mbili hizo hivi karibuni. Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Tanzania nchini humo ilieleza kuwa Balozi Kairuki amewataka wafanyabiashara hao kufanya hivyo kuunga mkono azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuifungua nchi. Aidha Balozi Kairuki alieleza kuwa kufanya hivyo pia kutaimarisha mahusiano kati ya mataifa hayo na kuongeza biashara kati yao kama moja ya nyenzo zao. Katika hatua nyengine Kairuki amewataka watanzania wanaofanya biashara ya bidhaa kutoka nchi hiyo kuhakikisha wanafanya manunuzi ya bidhaa zao kabla ya kuanza kwa maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina yanayoanzia Januari 25, ya kila mwaka.
Image
  UZINDUZI WA RIPOTI YA UTAFITI WA VYOMBO VYA HABARI NA URIPOTI WA UCHAGUZI MKUU 2020, DISEMBA 22, 2021 ZANZIBAR KATIBU Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Suleiman Abdallah Salim (kulia), akikata utepe kuzindua ripoti ya utafiti wa vyombo vya habari na uripoti wa uchaguzi mkuu wa 2020, uliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein uliomo katika jengo la ZURA, Zanzibar. KATIBU Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Suleiman Abdullah Salim (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa vyombo vya habari na uripoti wa uchaguzi mkuu wa 2020, Dk. Darius Mukiza, wakionesha ripoti hiyo baada ya kuzinduliwa katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein uliomo katika jengo la ZURA, Zanzibar. Mtafiti Kiongozi, Abadallah Katunzi akitoa maelezo juu ya matokeo ya utafiti vyombo vya habari na uripoti wa uchaguzi mkuu wa 2020 uliofanywa na Shule kuu ya uandishi wa habari ya Chuo Kikuu cha Dar es salam (SJMC) wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo kwa wandishi wa habari na viongo
Image
Dk. Mwinyi kufungua mkutano wa wataalamu kudhibiti ‘ufisadi’ NA MWANDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (pichani), anatarajiwa kufungua mkutano na mafunzo ya wataalamu wa kudhibiti rushwa na ufisadi nchini Tanzania utakaofanyika baadae wiki hii. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Wataalamu wa Kudhibiti rushwa na uhujumu uchumi tawi la Tanzania (ACFE), Msomi Maira, alieleza kuwa mkutano huo utaanza Disemba 13 - 15, mwaka huu katika hoteli ya Madinatul Bahr, Mbweni. Mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha wataalamu na watendaji wanaohusika na masuala ya udhibiti wa vitendo hivyo vyenye athari za kiuchumi na kijamii. Msomi aliongeza kuwa lengo la kufanyika kwa mkutano huo sambamba na mafunzo ni kujenga uelewa ili kuongeza idadi ya wataalamu hao lakini pia ufanisi wa taasisi zinazosimamia udhibiti wa ufisadi. “Wazungumzaji wakuu katika mkutano huo ni pamoja na Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serika
Image
ZATUC yahimiza wafanyakazi kutambua sheria za kazi, ajira NA MWANDISHI WETU SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC), imesema kuna umuhimu kwa wafanyakazi kujua sheria za kazi ili ziweze kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kuwaongoza pale wanapotaka kudai haki zao. Katibu Mkuu wa chama hicho, Khamis Mwinyi Mohammed (pichani), alisema hayo alipokuwa akizungumza na gazeti hili katika kikao cha kujadili haki za wafanyakazi na utekelezaji wake kilichoandaliwa na Shirika la msaada la kimataifa la Actionaid katika ukumbi Kitengo cha kudhibiti Malaria, Mwanakwerekwe. Alisema asilimia kubwa ya wafanyakazi hawajui sheria hizo jambo ambalo husababisha kuleta mkanganyiko mkubwa baina yao na waajiri pale kunapobidi kudai baadhi ya haki zao. “Wafanyakazi wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upataji wa haki zao, kwani asilimia kubwa wanashindwa kutofautisha haki za msingi na nyenginezo jambo ambalo husababisha kuleta malalamiko ndani ya taasisi mbalimba