Posts

Showing posts from November, 2021
Image
Puma yawatunza vinara kampeni usalama barabarani Ni wanafunzi walioshiriki shindano la michoro NA MWANDISHI WETU WADAU wa usalama barabarani nchini limaetakiwa kuchukua hatua kwa madereva wanaofanya matumizi yasiyo sahihi ya barabara ili kuona kiwango cha ajali barabarani kinapungua. Meya wa Jiji la Zanzibar, Mahmoud Mohammed Mussa, aliyasema hayo alipokua akikabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye zoezi la uchoraji lililoandaliwa kupitia kampeni ya kupunguza ajali za barabarani, hafla iliyofanyika Skuli ya Kiembesamaki ‘A’, Zanzibar. Alisema ni vyema kudhibiti matumizi yasiyo salama kwa madereva wa vyombo vya usafiri barabarani kwa kuona madereva wote wanafuta sheria na taratibu zilizowekwa. Mahmoud alisema hatua hiyo lazima iende sambamba na kufanya udhibiti wa vyombo visivyo fuata utaratibu wa matumizi sahihi ya barabara ili kuepusha ajali zisiso za lazima. Alieleza kuwa kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani kinapaswa kusimamia utekelezaji wa sheria za us