Posts

Showing posts from December, 2023

Wanahabari wanawake wapewa mbinu kukwepa udhalilishaji mitandaoni

Image
NA AMINA MCHEZO WAANDISHI wa habari wanawake wananafasi na mchango mkubwa katika kuielimisha jamii kupitia mitandao ya kijamii kukizingatiwa usalama wao . Akifungua mafunzo ya siku mbili  kwa waandishi wa habari wanawake Zanzibar, Mkufunzi na mwanahabari mkongwe kutoka nchini Kenya,  Cecilian Maundu (pichani), amesema wanahabari wanawake wamekuwa wakipitia wakati mgumu wakiwasilisha kazi zao za kimtandao ukilinganisha na wanahabari wa kiume. Amesema hali hiyo huwawia vigumu baadhi ya waandishi kuendelea na kazi yao na wengine kuathirika kisaikolojia kutokana na baadhi ya wafuasi wa kimtandao kuwatolea maneno ya kashfa pasi na wao kuridhia. Maundu amesema hali hiyo inaweza ikaondoka au kusaidiwa endapo kutakuwa na ushirikiano wa pamoja kati ya waandishi na taasisi za kihabar ili kuunda kikosi kazi ambacho kitamlinda mwandishi pale tu anapopata kadhia ya kimtandao. "Zanzibar mnapaswa kutumia taasisi hizi kama ZPC, TAMWA, MCT na nyengine ili pale kuona mnashambulia Kwa pamo

Zaipuna awapa msukumo vijana kuikabili changamoto za karne ya 21

Image
NA MWANDISHI WETU AFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri vijana nchini kunoa ujuzi wao wa karne ya 21 ili kufanikiwa katika soko la kisasa la ajira lenye ushindani. Akizungumza katika mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne wa skuli za sekondari za Feza yaliyofanyika jijini Dar es salam mwishoni mwa wiki, Zaipuna alisema ujuzi wa Karne ya 21 ni pamoja na kufikiri kwa kina, ubunifu, ushirikiano, mawasiliano, tekinolojia ya habari, uongozi, na stadi za maisha. “Mkiwa na ujuzi huu, nina hakika kabisa kwamba mtafaulu katika shughuli zenu za maisha iwe mnataka kuajiriwa au kujiajiri. Mtawavutia waajiri na wawekezaji na kwa moyo wa kuendelea kujifunza, mtaimarika siku hadi siku na kujiongezea thamani,” Zaipuna alisema. Aliongeza, “Kwa miaka mingi, nimekuwa sehemu ya Shule za Feza na ninathamini sana msisitizo ambao shule inaweka katika elimu ya maisha na maendeleo, ushirikiano na jamii na ukuzaji wa stadi za uongozi, sifa ambazo naamini zitakuwa na athiri chanya

SERIKALI YA DK. SAMIA IMEKUZA USAWA WA KIJINSIA - MAJALIWA

Image
NA MWANDISHI MAALUM WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha awamu hii ya uongozi kwa kutekeleza mikakati na sera zinazolenga kuondoa ubaguzi na kukuza usawa wa kijinsia.  Ametoa kauli hiyo Jumapili, Desemba 3, 2023 wakati akizungumza na maelfu ya wananchi waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya tatu ya kumbukumbu ya kumuenzi mwanasiasa mkongwe, Bibi Titi Mohammed yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ujamaa, Ikwiriri, wilayani Rufiji, mkoani Pwani.  Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alisema: “Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali, asasi za kiraia na jumuiya ya kimataifa, bado kuna changamoto nyingi katika kufikia usawa wa kijinsia. Ukweli huo unatoa msukumo muhimu wa kuendeleza na kuimarisha juhudi zetu katika kushughulikia masuala ya usawa wa kijinsia”, amesema. Akitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita, Waziri Mkuu amesema ya kwanza ni kuongeza idadi ya wanawake