Posts

Showing posts from January, 2021
Image
  Dk. Mwinyi ateta na CDF Mabeyo ikulu Zanzibar R AJAB MKASABA, IKULU ZANZIBAR RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuendelea na kazi kubwa ya kuimarisha amani na kuilinda mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, aliyefika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kumpongeza. Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limeendelea kufanya kazi kubwa ya kulinda amani nchini na kutoa pongezi maalum kwa kuisimamia amani hiyo hasa katika kipindi cha uchaguzi Mkuu uliopita. Alisema kuwa wananchi wa Tanzania wanajivunia hatua hiyo ya Jeshi lao katika kuhakikisha wanakuwa salama wao pamoja na mali zao wakati wote na kumuhakikishia Jeneral Mabeyo kwamba Zanzibar iko salama. Rais Dk. Mwin
Image
Dk. Mwinyi awaagiza Makatibu Wakuu kusimamia mapato, matumizi NA MWAMDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Makatibu wa Wakuu wa wizara za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kusimamia uwajibikaji, ongezeko la mapato na kuondoa urasimu kwenye wizara zao. Dk. Mwinyi ametoa maagizo hayo kwenye hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni wakiwemo makatibu wakuu, manaibu makatibu wakuu, Mwenyekiti, Wajumbe kamisheni ya utumishi na mkuu wa wilaya ya Magharib ‘A’ Alisema Makatibu Wakuu ndio wasimamizi wakuu wa utendaji kwenye wizara, hivyo wakasimamie uwajibikaji, utoaji huduma bora kwa wananchi, wakasimamie mapato na kuondosha urasimu. Alisema inashanga hadi leo zipo baadhi ya wizara maduhuli ya serikali yanakusanywa kwa fedha tasilimu, wakati ikizingatiwa tekolojia hiyo imepitwa na wakati na kwamba fedha za serikali zinatakiwa zikusanywe kwa njia ya mtandao.   "Nataka mkahakikishe fedha na maduhuli ya serika
Image
  Wizara yajipanga kuongeza ufanisi awamu ya pili TASAF NA MWANDISHI WETU SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itahakikisha utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa kunusuru kaya maskini unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) unaangalia mahitaji ya walengwa na wanaostahiki kupatiwa huduma zikiwemo za fedha taslimu. Hatua hiyo imeelezwa itawezekana kwa kuwashirikisha wakaazi wa vijijini na shehia husika ili kupatikana kwa walengwa wanaokusudiwa kuingia katika mpamgo huo. Waziri   wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Utatibu na Baraza la Wawakilishi, Dk. Khalid Salum Mohamed, alieleza hayo wakati akizungumza na wajumbe wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Serikali katika ukumbi wa wizara hiyo Vuga, mjini Zanzibar. Alisema utekelezaji huo unalenga kuimarisha maisha ya kaya maskini kupitia mradi huo yanatimia na watendaji wanaosimamia jukumu hilo wanatimiza    masharti na vigezo vilivyowekwa katika kuzifikia kaya hizo. Alisema, en
Image
Soraga awataka wajasiriamali kujengeana uwezo kibiashara NA MWAMDISHI WETU WAJASIRIAMALI wadogo wadogo na wafanyabiashara wametakiwa kutumia matamasha ya kibiashara kujengeana uwezo, umoja na kupeana taarifa zitakazoimarisha biashara nchini. WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga ambae pia ni Kaimu waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda, alieleza hayo alipokuwa akifunga tamsha la saba la biashara katika viwanja vya Maisara Suleiman, mjini Unguja. Alisema iwapo wadau wa biashara wataendelea kuunga mkono matamasha hayo, mipango ya serikali kuwawezesha kutangaza biashara zao utafanikiwa na kuleta tija kwa jamii nzima. Alieleza wizara yake ina mpango wa kuweka tamasha hilo mara mbili kwa mwaka ili kutanua wigo kwa wajasiriamali, wafanyabiashara na taasisi za umma pamoja na binafsi kutangaza biashara na huduma wanazozitoa kwa jamii. Alisema kuwa wizara imefarajika na kupata matumaini makubwa kuona wanaendelea kushiriki katika maonyes
Image
  Makamu wa Pili ataka mikakati kukuza kiswahili   NA OTHMAN KHAMIS, OMPR MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema watanzania wanatakiwa kuongeza mikakati ya itakayohakikisha lugha ya kiswahili inaongeza watumiaji kwenye ghafla za rasmi za kimataifa. Alieleza hayo jijini Dodoma katika ukumbi wa Hazina alipokuwa akifunga maadhimisho ya siku ya kiswahili, ambapo alisema inapaswa iwepo mikakati ya kuhakikisha lugha hiyo kubwa barani Afrika inapaa kimataifa. Hemed alisema kiswahili ni bidhaa inayouzika kwenye soko la kimataifa na kuipatia manufaa makubwa nchi, hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa lugha hiyo imeanza rasmi kutumika katika mikutano inayoandaliwa na taasisi za kimataifa. Alisema hadhi iliyofikia lugha hiyo hivi sasa imefungua milango kwa wataalamu wa kiswahili kufaidika kutokana na fursa zinazopatikana kwenye maeneo ya ukalimani, tafsiri, uandishi wa vitabu, uhariri na ufundishaji kwa wageni. Alisema watanzania wenye uwezo wana fursa ya kushir
Image
  SMZ itaendelea kuwatunza wazee - Dk. Mwinyi NA R AJAB MKASABA, IKULU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema serikali ya awamu ya nane itaendelea kutunga sera, sheria na kubuni mipango yenye lengo la kuimarisha ustawi wa wazee.   Dk. Mwinyi alieleza hayo jana wakati akifungua semina ya mapitio ya utekelezaji wa mradi wa uwajibikaji na utimilifu kwa wazee (AFFORD II) kwa kipindi cha mwaka 2020 na mpango wa mwaka 2021, iliyofanyika katika hoteli ya Verde.   Alisema kuwa serikali itazingatia mahitaji ya wazee katika ujenzi wa miundombinu, maakazi, pamoja na sekta ya afya na kwamba itaendelea kuimarisha ushirikiano ili jitihada za kuwatunza wazee zinapata ufanisi. Alifahamisha kuwa ipo sheria ya masuala ya Wazee Namba 2 ya mwaka 2020 ambayo imeweka utaratibu wa upatikanaji wa haki na huduma za ustawi kwa wazee, ikiwemo urasimishaji wa mpango wa Pensheni jamii.   Aliongeza kuwa hatua inayofuata ni kuhakikisha uundwaji wa kanuni za
Image
Maofisa Idara Maalum SMZ wasimamishwa kupisha uchunguzi NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Mohammed Ali amewasimamisha kazi baadhi ya maofisa waandamizi katika vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Vuga, waziri huyo alisema msingi wa kuwasimamisha kazi maofisa hao unatokana na ripoti ya Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), kuonesha kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma pamoja na kutowajibika. WAZIRI Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa Idara Maalumu za SMZ, Masoud Ali Mohamed, akionesha ripoti za Ukaguzi wa miradi ya Serikali, uliofanywa na (ZAECA) kwa Vikosi vya KMKM, JKU na ZIMAMOTO, mbele ya waandishi wa habari  . Massoud alisema kwa mamlaka aliyokasimiwa na dhamana ya kisheria amemsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar, Gora Haji Gora juu ya kadhia mbali mbali zinazomkabili. Masoud alisema kadhia
Image
  Waziri ataja mikakati kukuza uchumi wa bluu NA MWANDISHI WETU WIZARA ya Uchumi wa Bluu na Maendeleo ya imeeleza kuwa inaandaa mikatati mahsusi kukabiliana na changamoto ya uchache wa wataalamu kuzihudumia sekta zilizomo katika wizara hiyo. Waziri wa wizara hiyo Abdalla Hussein Kombo, alisema hivi karibuni wakati akifungua kongamano lililoshirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo katika viwanja vya Maisara.   Alisema tatizo hilo linazikabili nchi nyingi zinazopakana na bahari, hivyo kuna haja ya kuwekwa mikakati itakayomarisha uchumi kupitia sekta mbali mbali ikiwemo ya uvuvi. Alisema ili kufikia azma ya Zanzibar kunufaika na uchumi wa buluu, lazima sekta hiyo isimamiwe vyema na kuwekwa mkazo katika vipaumbele vya serikali ya awamu ya nane. "Dhana ya uchumi wa bluu ni mtambuka na inahitaji ushiriki wa kila mmoja wetu, ninawaomba tuendelee kuimarisha mashirikiano baina ya serikali na sekta binafsi sambamba na wadau wengine wa maendelo," alieleza Kombo. Aliongeza
Image
Kagere aiongoza Simba ikiiadhibu Chipukizi Mapinduzi Cup NA MWANDISHI WETU WAWAKILISHI wa Tanzania katika ligi ya mabingwa Afrika Simba SC imeanza michuano ya kombe la mapinduzi kwa ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya chipukizi FC Katika mchezo uliopigwa jana majira ya saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Amaan zanzibar, simba ilikutana na ushindani mkali katika kipindi cha kwanza huku wachezaji nwake wakipoteza nafasi nyingi za kufunga. Ikichezesha sehemu kubwa ya wachezaji wa kikosi cha pili, Simba ilijikuta ikipachikwa bao katika dakia ya 35 lililofungwa na Faki Mwalimu Sharif na kuongeza hamasa ya wachezaji wa hiyo yenye makao makuu yake kisiwani Pemba. Mchezo huo uliohudhuriwa pia na Makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad aliekuwa mgeni rasmi, Simba ilisawazisha bao hilo katika dakika ya 44 kupitia kwa mshambuliaji Medie Kagere kwa njia ya kichwa na kuongeza kasi ya mchezo huku timu hizo zikishambuliana kwa zamu na kupelekea kumaliza dakika 45 za kwana timu hizo zikiwa 1
Image
Maalim Seif: Viongozi tendeni haki kwa wote NA MWANDISHI WETU MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amewata viongozi kutenda haki kwa Wazanzibar wote bila ya kujali tofouti zao. Alisema kama wananchi na viongozi wao watashirikiana itakuwa chachu ya kusukuma mbele gurudumu la maedeleo miongoni mwa Wazanzibari. Maalim Seif alisema hayo katika msikiti wa Jumuiya ya Waarabu, Rahaleo Unguja, alipoungana na waumini wa dini ya Kiislam kkatika swala ya Ijumaa. Aliwataka viongozi waliochaguliwa na walioteuliwa kupiga vita ubaguzi wa aina yoyote katika kuwahudumia wananchi. “Tukifanyakazi kwa pamoja nakuhakikishieni maendeleo ni rahisi sana,” alisema Malim Seif. Sambamba na hilo amewataka waumini dini ya Kiislam kuiombea dua Zanzibar ili umoja uliopo udumu. Akizugmzia kuhusu ajira uwepo wa utulivu ni muhimu kwa ushiriiana an sekta binafsi kuondoa changamoto ajira Viwani Zanzibar. “Kama tukuvutana tutachelewa kupata maedeleo lakini sisi Wazanzibar tumeli