Posts

Showing posts from September, 2022

Programu kuratibu maudhui ya filamu kuanzishwa

Image
NA SAIDA ISSA, DODOMA Na Saida Issa, Dodoma  SERIKALI kupitia kamati ya kutetea haki za wasanii inatarajia kuanzisha programu ya kuratibu uandaaji wa filamu zenye maudhui ya kutangaza utajiri wa nchi katika eneo la utamaduni, historia na jiografia yake. Hayo yalibainishwa jijini hapa jana, na Katibu Mtendaji wa  Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Dk. Kiagho Kilonzo (pichani) wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli za bodi na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu wa fedha. Amesema hadi sasa Kamati ya kutetea Haki za Wasanii imeshapokea malalamiko 30 na kuyashughulikia, huku takribani sh. milioni 300 zilizokuwa zimedhulumiwa zimesharejeshwa kwa wasanii. Alisema lengo la filamu hiyo ni  kujenga mapenzi hasa kwa vijana wa kitanzania kwa nchi yao kwa kuwaongezea ufahamu wa rasilimali waliyonayo. “Programu hii itasaidia kutunza kumbukumbu za kihistoria kwa kuhusisha taarifa za viongozi wetu mbalimbali waliofanya mambo makubwa kama vile Mwl. Julius  Nyere

NMB yaendelea kung'ara benki bora wateja binafsi

Image
NA MWANDISHI WETU BENKI ya NMB imeshinda tuzo ya benki kiongozi wa kuwahudumia wateja binafsi nchini kutokana na ubora wa huduma zake kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha za umma wa walio wengi. NMB ilitunukiwa tuzo hiyo kwenye hafla ya tuzo za Global Banking and Finance (GBAF) zilizofanyika jijini London, Uingereza zilizoanzishwa mwaka 2011 na jarida la Global Banking & Finance Review lenye wasomaji zaidi ya milioni tatu ulimwenguni kote na ambalo shughuli yake kubwa ni kuangazia matukio na maendeleo ya kifedha duniani kwa mwaka wa pili mfululizo,. Akizungumza kwenye hafla ya kuwazawadia washindi wa tuzo za mwaka huu, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema ushindi wa benki hiyo ni kutambuliwa kwa dhamira yake thabiti ya kuwawezesha wateja na kulihudumia kikamilifu taifa kwa ujumla. “Tunawahudumia wateja binafsi wa aina mbalimbali wakiwemo wakulima wadogo, watumishi wa umma, wafanyakazi wa sekta binafsi na wajasiriamali wa kada zote kuanzi

SMZ yaweka sawa taarifa kuhusu Mkurugenzi ZIPA

Image
NA ABOUD MAHMOUD SERIKALI imekanusha taarifa zilizozagaa mitandaoni zinazomuhusu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji na Ukuzaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), Shariff Ali Shariff, kuhusishwa na tuhuma za ujasusi. Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga,  katika Ofisi za Mamlaka hiyo, huko Maruhubi wilaya ya Mjini Unguja, a lisema tuhuma hazina ukweli wowote na zimelenga kumchafulia jina mtendaji huyo  mzalendo kwa nchi yake. Alieleza kwamba tuhuma zinazohusiana na mtendaji huyo kuwa na hati mbili za kusafiria zinaonekana kuwepo kwa watendaji wasio waaminifu wenye kuchezea mifumo ya nyaraka za Serikali. "Kitendo kilichofanywa cha kumchafua mtendaji huyu sio kizuri kwani ni cha uongo hivyo hatutokua tayari kuona watendaji wanaharibiwa majina na naahidi uchunguzi kwa hatua zaidi,"alisema. Aidha Soraga aliwaomba wandishi wa habari kuacha kuyatumia vibaya majukwaa yao na kuendelea kufany

Waliojenga viwanja vya serikali kukiona

Image
NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Rahma Kassim Ali, amewataka watu waliovamia eneo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar liliopo Tunguu, mkoa wa Kusini Unguja na kujenga kinyume cha sheria, kusimamisha ujenzi huo hadi serikali itakapotoa maamuzi. Waziri Rahma alitoa agizo hilo hivi karibuni alipofanya ziara ya kutembelea eneo akiambatana na baadhi ya watendaji wa wizara na ofisi ya mkuu wa mkoa kusini Unguja akiwemo mkuu wa mkoa huo, hadid Rashid hadid. Ziara hizo nio sehemu ya utaratibu aliojiwekea wa kutembelea maeneo ya serikali ambayo baadhi ya wananchi huvamia na kujenga bila ya kua na kibali rasmi cha ujenzi hali inayopelekea kurudisha nyuma. jitihada za kuleta maendeleo nchini. “Kuna baadhi ya wananchi wanapoona maeneo ya wazi huyavamia na kuanza ujenzi bila ya kutambua kuwa maeneo hayo ni ya serikali hivyo wale wote waliovamia eneo hili, kuanzia leo wasitishe mara moja ujenzi huo na atakaekwenda kinyume na agizo hilo hatua za kisheri zitachukuliwadh

Kamati TASAF yatakiwa kuzitembelea kaya za wanufaika

Image
NA MWANDISHI WETU, DODOMA WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameitaka Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuwa na utamaduni wa kuwatembelea walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. Hatua hiyo imetajwa itawasaidia kubaini na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa mpango huo ambao serikali inautekeleza kwa lengo la kuimarisha maisha ya kaya maskini nchini. Jenista alitoa maelekezo hayo jijini Dodoma, wakati akizindua Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF iliyoteuliwa hivi karibuni mara baada ya kamati iliyopita kumaliza muda wake.    Aliwahimiza wajumbe wa kamati hiyo, kuhakikisha wanazungumza na viongozi, waratibu na walengwa katika maeneo yote ambayo mpango unatekelezwa ili kufikia lengo la serikali la kuzikwamua kaya maskini kutoka katika lindi la umaskini. “Mwenyekiti na wajumbe wa kamati hii, tembeleeni maeneo ambayo mpango wa TASAF unatekelezwa ili mjir

JMKF, PIT zawanoa wasichana kufikia ndoto zao

Image
DAR ES SALAM WASICHANA 40 kutoka skuli na vyuo mbali mbali wapepatiwa mafunzo ya ujasiriamali na stadi za maisha ili kuwawezesha kujikomboa kimaisha. Mafunzo hayo yaliyopewa jina la ‘Wasichana Washika Hatamu’ yaliandaliwa na taasisi za Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) kwa kushirikiana na shirika la Plan International Tanzania (PIT), yalifanyika kwa siku mbili katika hoteli ya Regency Park jijini Dar es salaam.   Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa JMKF, Vanessa Anyoti, alieleza kwamba imekuwa jukwaa muhimu katika kutambua haki za msichana na changamoto kubwa anazopambana nazo duniani.   Alieleza kwamba kwa sasa kuna wito wa kuchukuliwa kwa hatua za makusudi, kuleta mageuzi  ya kijamii na kisiasa ili kuondoa vizuizi vya ubaguzi na chuki vinavyoendelea kurudisha nyuma maendeleo ya wasichana.   “Tanzania inaungana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kukuza ufahamu wa jamii juu ya masuala yanayowakabili wasichana na kuwapatia f

Euro 10.1M kuimarisha usalama wa chakula Tanzania

Image
Na Saida Issa,DODOMA SERIKALI imezindua mradi wa miaka mitatu na miezi sita wa uboreshaji huduma za afya ya mimea Tanzania utakaogharibu kiasi cha EURO milioni 10.1 ikiwa ni hatua za kuimarisha usalama wa chakula nchini. Hayo yalibainishwa Jijini Dodoma na Naibu waziri wa Kilimo Antony Mavunde,wakati  akizungumza katika uzinduzi huo. Alisema Februari 16, 2021, serikali ya kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliingia mkataba wa kutekeleza mradi wa Kuimarisha Afya ya Mimea na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU). Mradi huu wa miaka mitatu na miezi sita unafadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Mfuko wake wa Maendeleoa (EDF), Shirika la Umoja w a Mataifa la Kilimo na Chakula (FAO) na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “Aidha, FAO ni wasimamizi wa mradi na utekelezaji hufanywa na serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viutilifu (TPHPA) iliyo chini ya Wizara ya Kilimo”alisema Mavunde. Alisema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa bajeti ya jumla EURO Mil

NMB, Bunge SC hapatoshi 'Kivumbi na Jasho' season II

Image
NA MWANDISHI WETU, DODOMA MSIMU wa pili wa Bonanza la ‘NMB Kivumbi na Jasho,’linalokutanisha timu za michezo za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya NMB, linafanyika Jumamosi Septemba 17, 2022 jijini Dodoma. Bonanza hilo linafanyika baada ya Septemba 16, mwaka huu benki hiyo kukabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa timu ya Bunge SC. Akizungumza wakati akipokea msaada wa vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Bunge SC, Tarimba Abbas, alieleza kuwa bonanza hilo linalenga kujenga na kuimarisha mahusiano mema baina ya bunge na NMB. Aidha Tarimba aliahidi kulitumia bonanza hilo kama kama ilivyofanya msimu uliopita kuzipa makali timu za bunge zinazojiandaa na mashimdano ya mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA 2022). "Tunatambua na kuthamini malengo ya bonanza hili, lakini tuwe wazi kwamba kwetu ni zaidi ya hapo. Mwaka jana lilitupa kipimo sahihi kuelekea EALA 2021, ambako tuliibuka washindi wa jumla katika michezo nane tuliyoshi

Shekimweri TAKUKURU aiipa njia kukabili rushwa

Image
NA SAIDA ISSA,DODOMA TAASISI ya Kuzuia na Kuapambana na rushwa Tanzania (TAKUKURU), imeshauriwa kuwajengea uelewa watumishi wa umma hasa katika maeneo ya manunuzi ili miradi inayofanyika iendane na thamani halisi ya fedha kudhibiti vitendo vya rushwa. Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri, alipotembelea maonesho ya ya maadhimisho ya Miaka 20 ya kuanzishwa kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora yanayoendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete ambapo Taasisi mbalimbali za msaada wa sheria zinashiriki. “Lazima tukiri kwamba kuna changamoto kwenye mapambano dhidi ya rushwa, kitu cha kwanza kumlea samaki akiwa mchanga kwani mnafanya kazi nzuri na kwenye wilaya tumeandaa  midahalo  kushindanisha shule kwenye kupinga masuala ya rushwa kwa njia ya mdahalo,” alieleza Shekimweri. Alieleza kuwa hatua hiyo imelenga kujenga uelewa wa wanafunzi na kujenga tabia ya ya kuchukia vitendo vya rushwa wakiwa wadogo ili wawe raia wema siku za baa

Mbunge ataka vijana kutambua nafasi zao kwenye maendeleo

Image
NA SAIDA ISSA, DODOMA MBUNGE wa Viti Maalum, Nusrat Hanje, amesema katika kuhakikisha mchango wa vijana unaonekana kwenye maendeleo ya taifa vijana wanatakiwa kutambua nafasi yao na nguvu ya ushawishi waliyonayo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ‘Vijana Makini’, jijini Dodoma alisema serikali ina wajibu wa kutengeneza mbinu wezeshi kwa kuwafanya vijana wanajibika kwa kua kundi hilo lina idadi kubwa ya watu nchini. "Vijana ni sehemu kubwa katika nchi yetu, nikiwa Mbunge kijana naishauri serikali yetu kuwatengenezea mbinu wezeshi vijana hawa ambao ndio taifa la kesho,” alieleza Mbunge huyo. Aliongeza kuwa iwapo serikali itaweka misingi imara na thabiti kwa vijana wa leo hapo baadae hakutakuwa na changamoto katika taifa kwani watakua imewekeza katika eneo salama. Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi, Uratibu na Uwezeshaji kiuchumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Eliakim Mtawa alisema mara nyingi vijana ndio wenye tatizo kwani wan

Othman aongoza mazishi ya mke wa mwandishi habari Zanzibar

Image
NA MWANDISHI MAALUM, ZPC MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  Alhaj  Othman Masoud Othman, Septemba 12, 2022 alijumuika na wananchi na viongozi mbali mbali katika maziko ya mke wa Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima na mwanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), Talib Ussi Hamad, bi. Hafsa Said Salum. Maziko ya bi. Hafsa aliyekua mtumishi wa Baraza la Manispaa Mjini, yalifanyika katika makaburi ya Kianga baada ya kusaliwa katika msikiti wa Weles, mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Akizungumzia msiba huo uliotokea Septemba 11, mwaka huu, Mwenyekiti wa ZPC, Abdallah Abdulrahman Mfaume, alitoa pole kwa wafiwa na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu na kumuombea dua marehemu apumzike kwa amani. Aidha aliwataka wanachama wa Klabu hiyo na waandishi wa habari Zanzibar kuendeleza umoja na mshikamano kama waliouonesha katika msiba huo kwa kuwa hupunguza machungu na kuongeza faraja kwa wafiwa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala Pema, Amin. Picha

Dk. Mwinyi kuongoza wadau sekta ya maji kujadili changamoto, mafanikio

Image
NA MWANDISHI WETU WADAU wa sekta ya maji wa ndani na nje ya Zanzibar wanatarajiwa kukutana Septemba 14 na 15, mwaka huu katika Kongamano la    Kimataifa la Maji Zanzibar. Kongamano hilo linalotarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, litafanyika katika hoteli ya Goldern Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar . Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Maisara, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Shaibu Hassan Kaduara, alisema wadau wa sekta ya maji wapatao 2,000 kutoa ndani na nje ya nchi wakiwemo, watafiti, watunga sera na watendaji wa wizara na idara za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano na Zanzibar watashiriki. Alieleza kongamano hilo ni sehemu ya kuunganisha Juhudi za Utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Uwekezaji katika sekta ya maji Zanzibar (ZanWIP) wa miaka mitano unaoanza 2022 hadi 2027 uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi. Alisema, hatua hiyo ni utamb