Posts

Showing posts from July, 2022

Msando awataka waandishi kutete haki za binadamu

Image
NA MADINA ISSA MKUU wa wilaya ya Morogoro, Albert Msando, amewataka wanahabari nchini kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi zikiwemo za utetezi wa haki za binadamu ili kuongeza tija katika kutoa habari kwa wananchi. Aliyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wanahabari yanayohusu namna bora ya kutoa habari yaliyoratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), yanayofanyika mkoani Morogoro. “Mwandishi wa habari mzuri ni yule anayetoa taarifa zinazozingatia ukweli, usahihi na kutopendelea ili jamii inufaike na wenye mamlaka wachukue hatua zinazostahiki,” alieleza Msando. Aidha aliwataka wanahabari kujitahidi kuwa watetezi wa haki za binadamu bila ya ushabiki au kuegemea upande mmoja ili kuepukana na changamoto mbali mbali zinazoweza kuwatokea. “Tujitahidini sana kuishi katika utetetezi wa haki za binaadamu na tusimameni katika ukweli na haki na wala tusiwe chanzo cha machafuko badala yake tuache habari ifike kama ilivyo ili wananchi

Simbaya Mkurugenzi mpya UTPC

Image
MUUNGANO wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umepata Mkurugenzi Mtendaji mpya kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Mkurugenzi wake, Aboubakar Karsan. Taarifa iliyotolewa na Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo (katikati pichani) kupitia mtandao wake wa Twitter imemtaja Mkurugenzi huyo kuwa ni Keneth Simbaya ambaye aliwahi kuiongoza taasisi hiyo siku za nyuma. “Nikiwa Rais wa UTPC nina furaha kutangaza kuwa Union of Tanzania Press Clubs, (Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania) UTPC, imepata Mkurugenzi Mtendaji mpya Ndg. Kenneth Simbaya (kulia kwangu), amechukua nafasi ya Abubakar Karsan (kushoto kwangu) ambaye amestaafu,” alieleza Nsokolo katika taarifa yake hiyo iliyoambatana na picha akiwa na watendaji wawili hao. Kwa niaba ya uongozi na wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), inampongeza Ndg. Simbaya kwa kuaminiwa na bodi ya wakurugenzi ya UTPC kushika wadhifa huo lakini pia Ndg. Karsan kwa utumishi wake uliotukuka kwa taasisi hiyo inayowaunganish

Hakuna habari yenye thamani zaidi ya maisha - Mussa

Image
NA MWANDISHI WETU WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuzingatia usalama wao wanapokua katika kazi za kutafuta na kutoa habari. Akifungua mafunzo ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari, Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya muungano wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Yussuf Mussa, alisema mafunzo hayo yatawajengea uwezo waandishi kujitambua na kujua thamani yao katika utendaji wa kazi zao. Alisema waandishi wa habari wana jukumu la kuwapasha wananchi habari lakini sayansi na teknolojia inawaweka wanahabari katika hatari licha ya kurahisisha kazi zao, hivyo ipo haja ya kujua jinsi ya kujilinda. Awali Ofisa Programu, Machapisho, Utafiti na Mafunzo kutoka UTPC, Victor Maleko, alieleza kuwa suala la usalama na ulinzi wa waandishi ni muhimu hivyo ni vyema wakazingatia wanachofundishwa. Aidha alisema UTPC inatekeleza mradi wa miaka miwili unaolenga kuzijengea uwezo taasisi za kihabari nchini, ambapo moja ya shughuli zake ni kutoa mafunzo kwa wanachama wa klabu kuhusu uli