Posts

Showing posts from May, 2021
Image
Majaliwa awawashia moto watendaji wanaodaiwa 'kukwapua' mamilioni NA MWANDISHI WETU, DODOMA WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa (pichani) amewasimamisha kazi mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya watendaji wa wizara ya Fedha na Mipango ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili. Alichukua hatua hiyo katika kikao kazi na waziri wa Fedha na Mipango, Kaibu Mkuu, Manaibu  Katibu Wakuu na Watendaji Waandamizi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.   Mbali ya hatua hiyo, Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kamishna wa Polisi, CP Salum Rashid Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika kwamba tuhuma si za kweli wahusika watarejeshwa kazini.   Majaliwa alizitaja baadhi ya tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, mwaka huu  kupitia vocha 30 ya shilingi milioni 251 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi hiyo maalum n
Image
  Makamu wa Kwanza ataka taasisi za dini zisaidiwe NA MWANDISHI MAALUM, OMKR MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman, amewahimiza waumini wa dini ya Kiislamu na taasisi mbali mbali nchini kuendelea kuzisaidia taasisi za kidini ili waumini waweze kufanya ibada zao katika mazingira yaliyo bora. Akizungumza mara baada ya Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Sogea, wilaya ya Mjini Unguja, Alhaj Othman alisema kushiriki katika kutoa misaada ni wajibu wa kila Muislamu, kwani ni kutekeleza maagizo ya Mwenyezi Mungu na hivyo huzidisha imani. "Waislamu natuweni wenye kujitahidi katika kulitekeleza hili ili tufikie malengo ya kuziimarisha nyumba za Mwenyezi Mungu", alisema Makamu huyo wa Kwanza wa Rais. Kwa sasa, Msikiti huo wa Sogea, ambao upo katika Wilaya ya Mjini Unguja, umezidiwa na idadi kubwa ya waumini hivyo unahitajika kuvunjwa na kuboreshwa zaidi. Kwa upande wake, Alhaj Othman aliahidi kushirikiana na waumini hao katika ujenzi wa msikiti wa mu
Image
Hemed Mgeni Rasmi maadhimisho uhuru wa habari Z’bar NA MWANDISHI WETU MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari kitaifa yatakayofanyika mwishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, Zanzibar. Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo, Dk. Mzuri Issa Ali, (wa pili kulia) alieleza kuwa maadhimisho hayo yatafanyika Jumapili Mei 30, 2021 na zaidi ya watu 250 wakiwemo waandishi wa habari, wadau wa habari na wawakilishi wa taasisi za umma na asasi za kiraia wanatarajiwa kuhudhuria. Alieleza kuwa maadhimisho hayo yataambatana na uwasilishaji wa mapendekezo ya mswada ya sheria mpya ya habari Zanzibar ulioandaliwa na wadau wakiwemo waandishi wa vyombo mbali mbali vya binafsi, serikali na mashirika ya habari. “Mswaada huo ambao umebeba miongozo na maazimio ya habari kikanda, kimataifa na kuzingatia mazingir
Image
DC Kati awataka walimu kumaliza mitaala kuongeza ufaulu NA MWANDISHI WETU MKUU wa Wilaya ya Kati Unguja, Marina Joel Thomas, amewataka walimu wa skuli za sekondari Wilayani humo kuhakikisha wanamaliza mitaala kwa wakati ili wanafunzi wapate muda wa ziada wa kupitia masomo yao. Marina alisema hayo katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa walimu walioleta ufaulu mzuri kwa wanafunzi wa kidato cha pili mwaka 2020 iliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha walimu (TC), Dunga, wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unguja. Alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza fursa kwa wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao ya taifa. “Kumaliza silabasi mapema kutawasaidia wanafunzi kupata muda mzuri wa kuyapitia masomo yao na kuongeza ufaulu katika mitihani yao ya taifa,” alisema Marina. Mbali na hayo Marina alifahamisha kwamba serikali ya wilaya hiyo imekuwa ikifanya jitihada kuona kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kinaongezeka ili kupata wataalamu wa ndani waliobobea katika fani mbali mbali.   Aidha a
Image
TUTATOA USHIRIKIANO KUFANIKISHA MALENGO YA SADC  - HEMED NA KASSIM ABDI, OMPR MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeipa kipau mbele sekta ya uchumi wa buluu unaoelekeza matumizi mazuri na endelevu ya rasilimali ya bahari ili wananchi wake waondokane na umaskini. Mheshimiwa Hemed ameleza hayo wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)  Kampasi ya Utalii Maruhubi. Akizungumizia juu ya Lugha ya Kiswahili Makamu wa Pili wa Rais alilikumbusha Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) kufuatilia maelekezo yaliotolewa na serikali kupitia Kongamano la kiswahili lililofanyika mwaka 2020. Katika kongamano hilo Kwa niaba ya serikali zote mbili Makamu wa Pili wa Rais ameahidi kwamba serikali zitaendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikishwa malengo ya Jumuiya yanafanikiwa. Nae, mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
Image
Dk. Mwinyi aahidi hatua kali waliohusika ripoti ya CAG NA MWANDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa wale wote waliohusika na kasoro zilitolewa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kasoro hizo zisije kurudiwa tena. Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo mara baada ya kukabidhiwa Ripoti za Hesabu za Serikali kwa mwaka 2019 -2020, huko katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, hafla ambayo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa fedha nyingi za Serikali zinapotea kwa kiasi kikubwa na iwapo hali hiyo itaendelea maendeleo hayatoweza kupatikana katika kuijenga nchi.   Alisema kuwa   lengo na madhumuni ya kupokea ripoti hiyo hadharani ni katika suala zima la kuhimiza uwajibikaji na utawala bora kwani ni lazima Serikali iwe wazi na kujulikana changamoto ndipo itakapowezekana kukabiliana na matatizo kama
Image
DC Kunambi awaalika wananchi kukimbiza mwenge NA SHADYA MOHAMED MKUU wa wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Kunambi amesema miradi mitano yenye thamani ya shilingi milioni 619,480 inatarajiwa kupitiwa na mwenge wa uhuru katika Wilaya hiyo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizo, Kunambi aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa uhifadhi wa mazingira na miti asili uliopo katika shehia ya Kitundu. Miradi mingine ni ya shamba darasa na bwawa la ufugaji wa samaki, kukagua huduma utoaji wa za afya ya kijiji, kuangalia darasa la TEHAMA na kituo cha kurekebisha taibia za watumiaji wa dawa za kulevya (Sober House). “Maandalizi kwa ajili ya kuupokea mwenge wa uhuru ndani ya wilaya yetu yanaendelea vyema na ninawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi ili zoezi la kuukimbiza mwenge lifanyike kwa ufanisi mkubwa,” alieleza Kunambi. Mwenge wa uhuru ulioanza mbio zake Mei 17, 2021 katika mkoa wa Kusini Unguja, utaanza mbio zake katika mkoa wa Mjini Magharibi kupitia wilaya ya Magharibi ‘A’
Image
 DK. MWINYI ATEMBELEA ENEO LA UWEKEZAJI BANDARI YA  KISASA MANGAPWANI RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akisalimiana na baadhi ya viongozi alipowasili katika eneo linalotarajiwa kujengwa kwa bandari ya kisasa Mwangapwani wilaya ya Kaskazibi 'B'. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza CEO wa Kampuni ya United Petroleum Collins Chemngorem  (alieshika kipaza sauti) . Wa kwanza kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud na kati kati ni Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Rahma Kassim Ali. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Makame Machano Haji akitowa maelezo ya eneo  la Ujenzi wa Bandari ya Kisasa Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini 'B' Unguja wakati wa ziara hiyo. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwin
Image
Dk. Mwinyi ahimiza waumini kufanya hijja mapema NA MWANDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi, amewataka waumini wa dini ya kiislamu kujipanga na kufanya ibada ya Hijja mapema badala ya kusubiri hadi baada ya kustaafu. Aidha aliieleza kuwa serikali inaendelea na mikakati ya kuanzisha mfuko wa Hijja ili kuwafanya waumini wengi kutekeleza ibada hiyo ambayo ni nguzo ya tano ya Uislamu. Dk. Mwinyi, aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia katika baraza la Eid el Fitri katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajuni Mjini Unguja, baada ya waumini wa dini ya kiislamu kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Alisema Mahujaji wa Zanzibar wanapaswa kujiandaa mapema kuteleza ibada hiyo, badala ya kusubiri hadi mtu anapostaafu na ameitaka Kamisheni ya wakfu na Mali ya Amana, kukamilisha mapendekezo yaliotolewa ili kufanikisha mfuko wa Hijja Zanzibar. Alisema ili kutekelelza vyema ibada hiyo na kuuendeleza mbele uislamu serikali
Image
  Dk. Mwinyi asema Tanzania inataka dunia yenye amani NA R AJAB MKASABA, IKULU JAMHURI ya Muungano wa  Tanzania, ikiwemo Zanzibar,  zinashirikiana na mataifa mbali mbali katika kudumisha amani, kutafuta suluhu ya migogoro, kuimarisha usalama na maendeleo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alieleza hayo katika hotuba yake wakati alipoungana na viongozi kadhaa duniani kwa njia ya mtandao kujadili njia za kuimarisha umoja na mshikamano ambapo mada kuu ilikuwa ni “Kuimarisha umoja na kudumisha amani katika rasi ya Korea. Mjadala huo ambao umefanyika kwa njia ya mtandao kutokana na uwepo wa maradhi ya corona, ambapo Dk. Mwinyi aliimpongeza Dk. Hak Jan Han mwanzilishi wa taasisi ya “Universal Peace Federeration” kwa kumpa fursa ya kuungana na viongozi wengine katika mjadala huo. Katika mjadala huo ambapo miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa ni kuwataka   viongozi wa dunia   siyo tu   kuzungumiza matatizo ya kuzuka kwa maradhi ya COVID 19, bali
Image
Wanahabari watakiwa kuibua changamoto za jamii NA ASYA HASSAN WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kusimamia wajibu wao wa kuibua changamoto zinazowakabili wananchi ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka. Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa kaskazini Unguja, Makame Haji Machano, alipokuwa akifumngua mkutano wa wadau kuadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Ayoub Mohammed Mahmoud. Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za mkoa huo Mkokotoni, wilaya ya Kaskazini 'A', Unguja uliandaliwa na klabu ya waandishi wa habari Zanzibar (ZPC) na kuhudhuriwa na wanachama wa klabu hiyo, viongozi wa asasi za kiraia, taasisi za umma na biashara. Makame alieleza kuwa waandishi wa habari na vyombo vya habari ndio mdomo wa jamii hivyo wakitekeleza vyema majukumu yao, watawasaidia viongozi kujua mahitaji ya wananchi na kuwatimizia kwa wakati. Alifahamisha kwamba watu wote ikiwa viongozi au raia wa kawaida wanahaki ya kupata haba
Image
Othman akutana na balozi wa Uingereza, Mwakilishi UNICEF NA MWANDISHI WETU MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imekubali kufanya kazi na Serikali ya Uingereza katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kidunia, likiwemo suala la dawa za kulevya kwa lengo la kuendelea kuilinda Zanzibar na watu wake. Othman amesema hayo alipofanya mazungumzo na Msaidizi Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Rick Shearn, wakati Balozi huyo alipofika kwa ajili ya kujitambulisha kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ofisini kwake Migombani, mjini Unguja. Balozi Shearn ameonesha azma ya serikali ya Uingereza kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye masuala kadhaa, likiwemo hilo la kupambana na uhalifu unaovuuka mipaka ya mataifa. Alisema bado kuna mambo yanaendelea kuiumiza dunia hasa suala la madawa ya kulevya na ufichwaji wa fedha za kihalifu. “Serikali imekubaliana kupitia vyombo mbalimbali vinavyohusika na usi
Image
SIKU YA UHURU WA HABARI DUNIANI Wadau wataka uhuru zaidi NA MUHAMMED KHAMIS, TAMWA WAKATI dunia  ikiadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, imelezwa kuwa   ipo haja kwa mamlaka mbali mbali   kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari   na uhuru wa kupata habari kwani  ni haki ya kikatiba. Hayo yamalezwa katika mkutano wa kujadili rasimu ya sheria ya habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) uliopo Maisara mjini Unguja.  Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari wanawake TAMWA-Zanzibar, Dk. Mzuri Issa Ali, alisema upatikanaji wa habari unachochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi, hivyo kuna kila sababu wananchi na wanahabri kupewa uhuru wao wa kufanya kazi bila ya kubugudhiwa. Mkurugenzi huyo aliwataka wanahabari kujikita zaidi katika kujiongezea elimu kwani ndio itakayowasaidia na kuwafanya kuwa wapambanuzi na mambo sambamba na kuepuka changamoto. Katika hatua nyengine aligusia pia suala la
Image
 
Image
Sadaka zinaimarisha amani, upendo kwenye jamii – Sheikh Kahalid NA MWANDISHI WETU OFISI ya Mufti wa Zanzibar imeeleza kuridhishwa kwake na sadaka zinazotolewa kwa watu wenye mahitaji maalum na watoto yatima, kwani inasaidia kuimarisha amani, upendo na kupunguza ukali wa maisha miongoni mwa jamii. Katibu wa ofisi hiyo Sheikh Khalid Ali Mfaume, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa vyakula vya futari iliyotolewa na taasisi ya Shura Muslim Charitable Organization katika ofisi za jumuiya hiyo, Kilimahewa, mjini Zanzibar. Alisema Mweyezi Mungu aliyataja makundi ya mayatima, wajane na watu wasiojiweza kuwa miongoni mwa yanaopaswa kusaidiwa hivyo jumuiya hiyo imefanya jambo jema linalopaswa kuigwa na kila mwenye uwezo. “Tumehimizwa na Allah (S.W) kuwashika mkono mayatima, masikini na wale wenye mahitaji maalum kwani kufanya hivyo sio kunawapunguzia ugumu wa maisha tu, bali huongeza upendo na kujenga amani katika jamii,” alisema Sheikh Mfaume. Alisema