Posts

Showing posts from December, 2022

JUWAZA kuhamasisha upatikanaji haki za wazee

Image
NA MWANDISHI WETU JUMUIYA ya Wastasfu na Wazee Zanzibar (JUWAZA) imesema itaendelea kuhamasisha upatikanaji wa stahiki za wazee zikiwemo za kiafya  ili kupata haki zao na afya zao zinaimarika. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake Migombani, Katibu wa jumuiya hiyo, Salama Kondo Ahmed, alisema jumuiya imekuwa ikitekeleza kazi zake kwa mashirikiano na serikali pamoja na taasisi binafsi katika kuhakikisha inafikia malengo yake. Alisema kuwa idadi ya watu wenye umri wa miaka 80 na kuendela inakadiriwa kukua kwa mara tatu zaidi baina ya mwaka 2022 na 2050 na kufikia milioni 426 ulimwenguni hivyo nchi zinahitaji kujiandaa na kuandaa mazingira ya kukidhi mahitaji ya wazee. Kondo alisema, JUWAZA ina mikakati mbali mbali ya kuimarisha ustawi wa wazee na wastaafu itakayotekelezwa kwa ushirikiano na serikali na taasisi binafsi “Miongoni mwa mambo ambayo tumeweza kuyasimamia ni pamoja na kufanya utetezi na kupelekea kuuanzishwa kwa mpango wa pensheni jamii kwa wazee wote t

MATUKIO MBALI MBALI YALIYOAMBATANA NA MKUTANO MKUU MAALUM WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR - ZPC

Image
Mkutano mkuu maalum wa ZPC ulifanyika Disemba 26, 2022 katika ukumbi wa Uhuru ZSSF Kariakoo Zanzibar Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, akihutubia kuufungua mkutano  Wanachama wakifuatilia maelezo na hotuba zilizokua zikitolewa Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, mara baada ya kuufungua mkutano mkuu malum.  Katibu Mkuu wa ZPC, Mwinyimvua Nzukwi (kushoto) akitoa maelezo kabla ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, kuokea na kugawa zawadi za vitabu vya kanuni za usambazaji maudhui mitandaoni kwa waandishi wa habari na wawakilishi wa taasisi za kihabari waliohudhuria Wanachama wakifuatilia maelezo na hotuba zilizokua zikitolewa Wanachama wakifuatilia maelezo na hotuba zilizokua zikitolewa Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, ripoti ya madhila kwa w

Tabia kuvalia njuga changamoto za waandishi wa habari

Image
  NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Mauld Mwita, ameahidi kuvalia njuga changamoto zinazowakabili waandishi wa habari wa vyombo vya binafsi ili wanufaike na kazi wanazozifanya kwenye vyombo hivyo. Ameeleza hayo Disemba 26, 2022 wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa Klabu ya waandishi wa habari Zanzibar (ZPC), uliofanyika katika ukumbi wa Uhuru uliopo katika viwanja vya kufurahishia watoto Kariakoo Zanzibar. Ameeleza kuwa anatambua changamoto zinazowakabili waandishi na watendaji wa vyombo vya habari hasa vya binafsi hivyo atafanya ziara za kushitukiza ili kujionea na kuona hatua za kuchukua kustawisha hali za wafanyakazi wa vyombo hivyo. Swala la wafanyakazi wa vyombo binafsi kutokua na mikataba nalifahamu lakini pia nafahamu mambo mengi ndio maana nmepanga kufanya ziara za kushitukiza ili nikajionee mwenyewe na nitachukua hatua kwa kushirikiana na taasisi au wizara nyengine,” amesema Tabia. Waziri Tabia akifungua mkutano  Aidha wa

Wanahabari watambua mchango wa Senyamule Geita

Image
Na MWANDISHI WETU, DODOMA CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita (GPC), kimempongeza Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, kwa mabadilko ya utendaji na maendeleo aliyoyafanya alipokua mkuu wa mkoa huo. Mwenyekiti GPC Renatus Masuguliko ametoa pongezi hizo jana (Disemba 19, 2022) ofisini kwa Mkuu wa mkoa huyo alipofika kwa lengo la kukabidhi hati ya pongezi kwa niaba ya wanachama wa klabu hiyo.   Masuguliko ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kutambua mchango wa Senyamule alioutoa kwa wananchi wa mkoa wa Geita na chama hicho katika kipindi alichokua Mkuu wa mkoa huo kwa takriban mwaka mmoja kabla ya kuhamishiwa mkoa Dodoma. Akiambatana na Katibu wa klabu hiyo, Novatus Lyaruu, mwenyekiti Masuguliko amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja ambao Senyamule akiwa mkoani Geita, alifanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika sekta zote na kumpongeza kwa kusimamia kwa vitendo kaulimbiu aliyoianzisha ya ‘Geita ya dhahabu, Utajiri wa heshima’. “Mheshimiwa Senyamule ulipokuja na hii ka

Utulivu watawala upigaji kura Amani

Image
NA MWANDISHI WETU MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Jacobs Mwambegele, amesema uchaguzi mdogo wa jimbo la Amani uliofanyika jana, umefanyika katika mazingira ya amani na kwamba tume yake imetimiza wajibu. Akizungumza mara baada ya kukagua vituo mbali mbali kuangalia zoezi hilo linavyofanyika, Mwenyekiti huyo alisema vituo vyote vya kupiga kura vimefunguliwa kwa wakati na wapigara kura wamepata vifaa vyote. Alisema vituo 23 vilivyotumika katika zoezi hilo kwa shehia nne vilifunguliwa saa 1:00 asubuhi na vilifungwa majira ya saa 10:00, ikiwa ni kuashiria kumalizika kwa zoezi la kumchagua mbunge mpya wa jimbo hilo. Alisema katika vituo hivyo, mawakala wa vyama vya siasa, walipewa fursa kamili ya kutekeleza majukumu yao kwenye vyumba vya kupigia kura, huku wananchi nao wakijitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi hilo.   Alisema hadi muda wa mchana wa jana, hakukua na malalamiko yaliyofikishwa katika tume hiyo na kwamba tume ilikuwa tayari muda wote kupokea chang

Marekebisho sheria huduma za habari Januari

Image
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye (mwandishi), amewahakikishia wanahabari kuwa kikao kijacho cha bunge kitapeleka marekebisho ya sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016. Alieleza hayo wakati akifungua kongamano la maendeleo ya sekta ya habari mwaka 2022, lenye kauli mbiu ‘habari kwa maendeleo endelevu’, lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam Alisema katika bunge litakaloanza Januari mwakani, wizara hiyo inatarajia kupeleka marekebisho ya sheria hiyo ili ifanyiwe marekebisho katika baadhi ya vifungu, hali ambayo itakuza uhuru wa habari. Nape alieleza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, itashirikiana na vyombo vya habari na kwamba itawezesha kuweka mazingira mazuri na kuondosha vikwazo kwa wanahabri. Nape aliwashauri wadau wa habari waone ipo haja ya kuzioanisha sheria ya habari na sheria ya u

Changamoto sekta ya habari kupatiwa ufumbuzi

Image
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAM SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza kuwa itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wadau wa habari katika kuhakikisha changamoto zinazowakabili zikiwemo sheria zisizo rafiki zinatatuliwa. Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alieleza hayo hivi karibuni alipokua akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), uliofanyika jijini Dar es salaam. Alisema serikali itafanya kazi na waandishi kwa sababu inatambua mchango wa UTPC katika kunyanyua uwezo wa waandishi wa habari hapa nchini, kuwezesha ofisi za waandishi wa habari mikoani kufanya kazi, kuchochea maendeleo mikoani na kupasha habari wananchi waweze kupata uelewa ili kufanya uamuzi sahihi “Niko tayari kufanya kazi na UTPC wakati wa shida na raha ninachowaomba msiniangushe mniunge mkono na mimi nitawaunga mkono waswahili wanasema imani huzaa imani, mimi nina imani kubwa na UTPC na ninapenda sana umoja huu kwa sababu ninatambua hapa nilipo