Posts

Showing posts from July, 2021
Image
  Waandishi wahimizwa kuepusha migogoro NA ASYA HASSAN WAANDISHI wa habari wametakiwa kujikita katika uandishi wa habari zenye mnasaba wa kuleta amani katika jamii kwa lengo la kuepusha migogoro inayoweza kusababisha vuruga ndani ya jamii. Hayo yalisemwa na Meneja Mkaazi wa shirika la Search for Common Ground, Hussein Sengu, alipokwa katika mafunzo ya usuluhishi na ujenzi wa amani yaliyowashirikisha waandishi wa habari kupitia mradi wa dumisha amani unaosimamiwa na shirika hilo. Aliseama waandishi wa habari ni watu watakao weza kuifanya jamii kuwa na Amani ama kuisababisha kuingia matatani hivyo ni vyema kuzitumia kalamu na midomo yao kwa uweledi na ufanisi ili kuona Amani iliyopo inazidi kuimarika. Meneja huyo alisema lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya namna ya kuripoti habari zenye mlengo wa kuleta amani katika jamii na sio kuongeza tofauti ziliyopo ndani ya maeneo yao. Sambamba na hayo alisema jamii imekuwa ikikabiliwa na matatizo tofauti
Image
Waandishi watakiwa kuwasilisha kazi zenye ubunifu EJAZ NA KHAMISUU ABDALLAH KAMATI inayosimamia tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Zanzibar imeeleza haja ya waandishi kuzingatia ubunifu na weledi katika kazi wanazoziwashilisha katika mashindano. Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo inayoundwa na taasisi za habari Zanzibar, wakati wakitangaza msimu wa pili wa tuzo hizo kwa mwaka 2021/ 2022 kwa waandishi wa Zanzibar katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Kikwajuni Zanzibar. Alieleza kuwa ili kazi iweze kushinda, kuna haja ya mwandishi kufanya kazi ya ziada na kwamba upo umuhimu wa kuzingatia misingi ya taaluma na matokeo ya kazi ya mwandishi. “Tunawashukuru wote walioshiriki na walioshinda katika msimu mwa kwanza na tunapoelekea msimu wa pili ipo haja ya kujiandaa na kujipanga kikamilifu ili kazi yako hata kama haikushinda basi iwe na matokeo,” alisema Dk. Mzuri ambae pia ni mkurugenzi wa T
Image
Mkulima ashinda gari la 169m/- promosheni ya NMB NA MWANDISHI WETU, MOROGORO MKAAZI wa Kinole, wilaya ya Morogoro vijijini, Abdallah Mohammed (50), ameshinda promosheni ya ‘Bonge la Mpango’ na kukabidhiwa zawadi ya gari yenye thamani ya shilingi millioni 169. Promosheni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na benki ya NMB, ilimalizika rasmi Jumatano wiki hii ambapo Mohammed alikabidhiwa gari hiyo Toyota Fortuner katika hafla ya makabidhiano yaliyofanjika katika soko kuu la Chifu Kingalu karibu na tawi la NMB la Wami mjini Morogoro juzi. Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi hiyo, Kaimu Ofisa Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani wa benki hiyo, Benedicto Baragomwa, alisema promosheni hiyo ililenga kubadilisha maisha ya watanzania ambapo zawadi mbali mbali zilikabidhiwa kwa wateja 120 walioshinda katika promosheni hiyo. Baragomwa alieleza kuwa mbali ya gari na fedha taslimu, zawadi nyingine zilizokabidhiwa ni pikipiki za magurudumu matatu aina ya LIFAN na gari ndogo aina ya TATA Ace. “NMB ilifanya
Image
  Majaliwa aipongeza NMB kutekeleza mpango wa Ushirika Afya   NA MWANDISHI WETU, TABORA WAKULIMA nchini wametakiwa kutumia mpango wa Ushirika Afya ili kujihakikishia usalama wa afya zao wakati wa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara. Wito huo umetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa, alipokuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Ushirika na kuitaja hatua hiyo kuwa ni mafanikio makubwa katika vita dhidi ya umaskini na maradhi. Alisema makubaliano yaliyofikiwa kati ya benki hiyo na vyama hivyo vya ushirika, yanathibitisha kuanza rasmi kutolewa kwa huduma baada ya wanachama wake kukabidhiwa kadi za NHIF kwenye kilele Jumamosi iliyopita. Aidha Waziri Mkuu alizishukuru taasisi za fedha kwa mchango inaoutoa kuviimarisha vyama vya ushirika na kuvifanya kuwa nguzo muhimu ya uchumi wa taifa. Katika hafla hiyo, Majaliwa alikabidhi kwa wakulima wa tumbaku Kulwa Mfaume, Saleh Mpemba na Athanas Semeduke kadi