
ZPC, CPS zakubaliana kuimarisha uhusiano, mashirikiano NA MWANDISHI MAALUM KLABU ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) na kampuni ya CPS Lives zimekubaliana kuendelea kushirikiana ili kufanikisha malengo ya taasisi hizo. Makubaliano hayo yamefikiaa katika mazungumzo yaliyofa baina ya uongozi wa ZPC na kampuni hiyo inayojenga mji mpya wa Fumba (Fumba Town Development). Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume aliongoza ujumbe wa klabu yake ulipofanya ziara katika ofisi kampuni hiyo ziliopo ndani ya mji huo unaojengwa Nyamanzi, wilaya ya Magharibi "B'. Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume (alievaa kofia) akiongoza kikao cha majadiliano kati ya ZPC na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya CPS Live Tobias Dietzold. Akizungumzia ziara hiyo, Mfaume alieleza kuwa ililenga kubadilishana mawazo, kumagua maendeleo ya ujenzi wa mji huo na kuimarisha uhusiano. “Kwa muda wa miaka minne sasa ZPC na CPS tumekuwa na mahusiano ya kitaasisi yaliyolenga katika kuimarisha utendaji wa pande zote mbili...