letter head

TAARIFA MAALUM KWA WANACHAMA WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR - ZPC

NDUGU WANACHAMA,

Kwa niaba ya Kamati Tendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar [ZPC] ninawajulisha kuwa Kamati ilikutana Julai 7, 2020 katika ofisi zake Kijangwani na kujadili mambo mbali mbali na kufikia maamuzi yafuatavyo:-

1.   Mkutano Mkuu wa Wanachama wa ZPC ufanyike Agosti 8, 2020 kama ilivyopendekezwa katika vikao vilivyotangulia. Kutokana na uamuzi huo, taarifa rasmi inatolewa kwa Wanachama kama inavyoelekezwa na katiba ya Klabu kifungu cha 16(d) kinachotaka taarifa ya Mkutano Mkuu wa ZPC itolewe mwezi mmoja kabla ya siku ya Mkutano. Agenda za Mkutano huo zitatangazwa baadae pamoja na taratibu za uchaguzi wa viongozi Klabu ambao ni moja ya agenda za Mkutano huo.

2. Kamati Tendaji imeteua Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi itakayoratibu, kusimamia na kuendesha uchaguzi wa viongozi wa Klabu inayoundwa na Wajumbe kutoka asasi za kiraia. Majina ya Wajumbe wa Kamati hiyo yatatangazwa baada ya kukamilika kwa tatatibu za uteuzi wao,

3. Kuandaa kanuni za uchaguzi wa klabu ambazo zitatumika katika Mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa ZPC,

4.   Kupokea na kujadili taarifa ya maandalizi ya Mkutano Mkuu na kupendekeza mambo ya kufanyika ili kukamilisha maandalizi na kufanikisha Mkutano kwa kiwango cha juu,

5.   Kupitia na kuidhinisha maombi ya wanachama ambao walikuwa hawajakamilisha taratibu wakati wa kikao kilichopita na kupitia orodha ya Wanachama wa ZPC.

Aidha Kamati inawashukuru Wanachama na wadau mbaki mbali wa Klabu kwa ushirikiano wanaoutoa na kuwataka kuendelea kufanya hivyo hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya Mkutano Mkuu ili kutekeleza kwa ufanisi matakwa ya katiba ya Klabu.

Imetolewa na:-

Mwinyimvua A. Nzukwi,

Kaimu Katibu Mkuu - ZPC,

Kwa niaba ya Kamati Tendaji - ZPC

Julai 8,2020.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango