ZPC, CPS zakubaliana kuimarisha uhusiano, mashirikiano

NA MWANDISHI MAALUM

KLABU ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) na kampuni ya CPS Lives zimekubaliana kuendelea kushirikiana ili kufanikisha malengo ya taasisi hizo.

Makubaliano hayo yamefikiaa katika mazungumzo yaliyofa baina ya uongozi wa ZPC na kampuni hiyo inayojenga mji mpya wa Fumba (Fumba Town Development).

Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume aliongoza ujumbe wa klabu yake ulipofanya ziara katika ofisi kampuni hiyo ziliopo ndani ya mji huo unaojengwa Nyamanzi, wilaya ya Magharibi "B'.

Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume (alievaa kofia) akiongoza kikao cha majadiliano kati ya ZPC na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya CPS Live Tobias Dietzold.

Akizungumzia ziara hiyo, Mfaume alieleza kuwa ililenga kubadilishana mawazo, kumagua maendeleo ya ujenzi wa mji huo na kuimarisha uhusiano.

“Kwa muda wa miaka minne sasa ZPC na CPS tumekuwa na mahusiano ya kitaasisi yaliyolenga katika kuimarisha utendaji wa pande zote mbili na ndio maana tuliona umuhimu wa kuja kuwatembelea kushuhudia mafanikio yaliyofikiwa,” alieleza.

Alisema ZPC ikiwa ni taasisi mwamvuli ya waandishi wa habari inapaswa kuwa na mahusiano mema na wadau wake wakiwemo kutoka sekta binafsi ili kuharakisha maendeleo ya tasnia ya habari, taasisi hizo na jamii kwa ujumla.

Akizungumza  Mtendaji Mkuu wa CPS Live Tobias Dietzold alielezea kufurahishwa kwake jinsi taasisi hiyo ya kihabari inavyofuatilia maendeleo ya mradi huo unaohusika na ujenzi wa mji mpya wa maendeleo wa Fumba.


Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CPS Lives Tobias Dietzold (kulia) akizungumza na viongozi wa ZPC. Wengine ni Mratibu wa ZPC Mgeni Hamad (kulia) na Mweka Hazina Halima Thuweni.

“Siku zote ZPC (klabu ya waandishi wa habari Zanzibar) imekuwa daraja muhimu kwa jamii ya watu ambao hawafiki huku kila mara. Na sisi tunaahidi tutaendelea kushirikiana na waandishi wa habari kupitia ZPC,” alieleza.

Ziara hiyo ya kawaida ilihusisha viongozi wa klabu hiyo ambao walipata nafasi ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo unaohusisha ujenzi wa nyumba za makaazi huku baadhi yao zikiwa zimeshahamiwa.





 


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango