Posts

Showing posts from June, 2026

Programu kuimarisha elimu Chaani yazinduliwa

Image
Waziri  Lela asema  itaongeza hamasa ya kujifunza  NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohamed Mussa, amesema programu ya kuimarisha elimu katika jimbo la Chaani itapunguza changamoto zinazowakabili wazazi na walezi katika kugharamia mahitaji ya wanafunzi, hususani gharama za kambi za masomo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Chaani Masingini, alisema Serikali ya awamu ya nane inaendelea kuitanguliza sekta ya elimu kwa kuimarisha miundombinu, kuongeza vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia katika ngazi zote. WAZIRI Lela,  Mbunge na Mwakilishi wa jimbo la Chaani wakikabidhi moja ya makoksi ya karatasi kwa mmoja ya walimu wakuu skuli za jimbo kwa ajili ya mitihani ya kujiandaa na mitihani ya taifa  ya wanafunzi wa skuli zao. Alisema dhamira hiyo inaonekana kupitia ongezeko la bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, ambapo kwa ...

Uwazi matumizi ya bahari nyenzo muhimu kulinda uchumi wa Afrika – Tony Long

Image
NA MWANDISHI WETU MKURUGENZI Mtendaji wa Global Fishing Watch, Tony Long (pichani) amesema uwazi katika shughuli za baharini ni msingi muhimu wa kulinda rasilimali za bahari, kuimarisha uchumi wa Afrika na kuhakikisha usalama wa chakula kwa mamilioni ya wananchi wanaotegemea sekta ya uvuvi. Long alisema kwa karne nyingi jamii za pwani ya mashariki mwa Afrika zimeitumia Bahari ya Hindi kama chanzo cha biashara, ajira na maendeleo, huku akieleza kuwa umuhimu wa bahari unaendelea kuongezeka wakati ambapo uchumi wa buluu unatajwa kuwa miongoni mwa nguzo kuu za maendeleo ya bara. Alisema sekta za uvuvi na ufugaji wa samaki huchangia takribani dola bilioni 24 za Marekani kila mwaka katika uchumi wa Afrika, wakati thamani ya uchumi wa buluu wa bara hilo ikikadiriwa kufikia dola bilioni 300. Hata hivyo, Long alisema ukuaji huo unakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na kukosekana kwa uwazi katika shughuli nyingi za uvuvi wa baharini. Akinukuu matokeo ya utafiti wa mwaka 2024 uliofanywa na Gl...

Absa Tanzania yahamasisha wajasiriamali kutumia huduma za kifedha

Image
NA MWANDISHI WETU BENKI ya Absa Tanzania imeendelea kuhamasisha wanawake wajasiriamali kutumia huduma rasmi za kifedha ili kuimarisha biashara zao na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Hatua hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia huduma zinazolenga kuongeza ujuzi wa usimamizi wa fedha, upatikanaji wa mitaji na matumizi ya teknolojia katika biashara. Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani jijini Dar es Salaam, ambayo Absa ilikuwa miongoni mwa wadau waliodhamini, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa benki hiyo, Victor Nchimbi, alisema benki hiyo inatambua mchango mkubwa wa wajasiriamali katika kukuza uchumi. MKUU wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Victor Nchimbi, akizungumza na wajasiriamali kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo zinazowalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani ambapo Absa ilikuwa moja ya taasisi zilizojitokeza kudh...