TAARIFA MAALUM KWA WAANDISHI WA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAOMBI YA WAANDISHI KWA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. HUSSEIN ALI MWINYI Awali ya yote napenda kutumia fursa hii kwa niaba ya Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), kuwajullisha ya kwamba baadhi ya mambo yaliyowasilishwa na waandishi wa habari mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kikao cha tarehe 18/05/2022 yameanza kufanyiwa kazi. Katika kikao hicho cha faragha kilichofanyika katika Ikulu ya Zanzibar, waandishi wa habari walipata fursa ya kuzungumza na Rais mambo mbali mbali yanayohusu mwendendo na hali halisi inayohusiana na tasnia ya habari nchini, hali tunayoamini imeongeza uelewa wa kiongozi huyo wa nchi na wasaidizi wake juu ya mazingira ambayo waandishi wa habari wa Zanzibar wanayofanyia kazi. Pamoja na maelezo ya waandishi ambayo baadhi yao yalipatiwa majibu na kutolewa ufafanuzi wakati wa kikao hicho, pia waa...