Wanahabari waombwa kuhamasisha chanjo ya UVIKO 19
NA ASYA HASSAN MENEJA Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kutokana Wizara ya Afya Zanzibar, Bakar Hamad Magarawa, amesema vyombo vya habari vina wajibu wa kuendelea kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya ya UVIKO - 19. Alisema hayo alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano wa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya hali halisi ya maradhi hayo na upatikanaji wa chanjo yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kwa kushirikiana na Internews. Alisema lengo la serikali hadi kufika Disemba mwaka huu asilimia 70 ya wananchi wawe tayari wamechanjwa lakini hadi sasa waliochanjwa ni asilimia 35, hali inayoonesha kwamba kuna kundi kubwa halijahamasika kupata kinga hiyo. Sambamba na hayo alifahamisha kwamba licha ya serikali na waandishi wa habari kufanya kazi kubwa ya kuihamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuchanja bado jamii haijaona umuhimu huo. Alisema kwa sasa vipo vituo zaidi ya 120 vinavyotoa chanjo hizo katika maeneo mbalimbali, hivyo aliiomba jamii ikavitumia ipasa...