Mhandisi Zena ahimiza ushiriki wa vijana katika maendeleo

NA MWANDISHI WETU

KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, amewahimiza vijana kushiri utekelezaji mradi wa ‘Kijana imara’ ili kutatua changamoto zinazowakabili.

Akifungua mdahalo wa ‘Kijana Imara Transformative’, ulioandaliwa na Shirika la Kiona Youth Coordinates (KYCo) katika hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar, alisema mradi huo utasaidia kubadili mitazamo ya watu juu ya masuala ya vijana.

Alisema vijana ni kundi kubwa katika jamii hivyo kuna umuhimu wa kuunganisha mawazo na nguvu zao ili kuepuka kupeleka nguvu zao katika mambo yasiyo na tija.

“Kwa kuzingatia kuwa vijana ni kundi kubwa hivyo kama hatutakuwa na njia nzuri ya kutumia nguvu kwa kweli wataipeleka mahali ambapo sio sahihi na matokeo yake tunaweza kuharibikiwa,” alieleza.

Akizungumza katika mdahalo huo uliohudhuriwa na vijana zaidi ya 250 kutoka taasisi mbali mbali za vijana na mabaraza ya vijana, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Rajab Khamis (katikati pichani), alisema serikali inaendelea kuratibu na kusimamia mipango ya maendeleo ya vijana hivyo alipongeza mchango wa sekta binafsi kusaidia vijana.

Aidha alisema vijana wana haki ya kutumia fursa zilizopo kujiimarisha kiuchumi na kupaza sauti zao ili kupiga hatua na kwamba wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa asasi za vijana na wadau wa maendeleo kufikia malengo ya vijana.

Mkurugenzi Mtendaji wa KYCo, alisema  mradi wa Kijana Imara Transformative Dialogue ni ubunifu ulioasisiwa na shirika lake Agosti 12, 2021 ili kutoa mchango kwa vijana katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana inayoadhimishwa kila ifikapo Agosti 12.

Aliongeza kuwa tokea kuanza utekelezaji wake, mradi umewafikia vijana milioni 3.8 huku lengo ni kufanya uchechemuzi kupitia vyombo vya mawasiliano kuwafahamisha vijana na jamii juu ya  sera ya vijana ya 2007 Tanzania Bara na sera ya vijana ya Zanzibar.

 

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango