Wanahabari wanawake wapewa mbinu kukwepa udhalilishaji mitandaoni

NA AMINA MCHEZO WAANDISHI wa habari wanawake wananafasi na mchango mkubwa katika kuielimisha jamii kupitia mitandao ya kijamii kukizingatiwa usalama wao . Akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari wanawake Zanzibar, Mkufunzi na mwanahabari mkongwe kutoka nchini Kenya, Cecilian Maundu (pichani), amesema wanahabari wanawake wamekuwa wakipitia wakati mgumu wakiwasilisha kazi zao za kimtandao ukilinganisha na wanahabari wa kiume. Amesema hali hiyo huwawia vigumu baadhi ya waandishi kuendelea na kazi yao na wengine kuathirika kisaikolojia kutokana na baadhi ya wafuasi wa kimtandao kuwatolea maneno ya kashfa pasi na wao kuridhia. Maundu amesema hali hiyo inaweza ikaondoka au kusaidiwa endapo kutakuwa na ushirikiano wa pamoja kati ya waandishi na taasisi za kihabar ili kuunda kikosi kazi ambacho kitamlinda mwandishi pale tu anapopata kadhia ya kimtandao. "Zanzibar mnapaswa kutumia taasisi hizi kama ZPC, TAMWA, MCT na nyengine ili pale kuona mnashambulia Kwa ...