Wanahabari wanawake wapewa mbinu kukwepa udhalilishaji mitandaoni
Akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari wanawake Zanzibar, Mkufunzi na mwanahabari mkongwe kutoka nchini Kenya, Cecilian Maundu (pichani), amesema wanahabari wanawake wamekuwa wakipitia wakati mgumu wakiwasilisha kazi zao za kimtandao ukilinganisha na wanahabari wa kiume.
Amesema hali hiyo huwawia vigumu baadhi ya waandishi kuendelea na kazi yao na wengine kuathirika kisaikolojia kutokana na baadhi ya wafuasi wa kimtandao kuwatolea maneno ya kashfa pasi na wao kuridhia.
Maundu
amesema hali hiyo inaweza ikaondoka au kusaidiwa endapo kutakuwa na ushirikiano
wa pamoja kati ya waandishi na taasisi za kihabar ili kuunda kikosi kazi
ambacho kitamlinda mwandishi pale tu anapopata kadhia ya kimtandao.
"Zanzibar mnapaswa kutumia taasisi hizi
kama ZPC, TAMWA, MCT na nyengine ili pale kuona mnashambulia Kwa pamoja mitandaoni
kukomesha udhalilishaji huu", ameongeza Cecilian.
Hata
hivyo amewatahadharisha wanahabar wanawake kuacha kuweka taarifa zao
binafsi mitandaoni kwani baadhi ya wakati huwageukia na kutumika katika
udhalilishaji.
"Kama mwanahabar anataka kuweka taarifa
zake binafsi basi lazima azifiche na aweke neno la Siri (password) ambayo watu
hawataweza kuingia la si hivyo taarifa hizo mwisho wake huwa mwiba kwake",
ameongeza.
Wakichangia wakati wa mafunzo hayo, baadhi ya waandishi walioshiriki mafunzo hayo Najjat Omar kutoka The Chanzo online na Khairat Haji kutoka Chama cha Waandishi wa Habar Wanawake Tanzania (TAMWA ZANZIBAR) wamesema hali bado ni mbaya kwa waandishi wanawake pale wanapowasilisha kazi zao mitandaoni kutokana na kukosa msaada kwenye taasisi husika.
Mafunzo
hayo ya siku mbili yaliyobeba ujumbe wa ‘Namna ya kuwa salama mtandaoni’ yamedhaminiwa
na shirika la Pen America la nchini Marekani.
Comments
Post a Comment