Mama Mariam aelekeza namna ya ulaji vyakula vya lishe

NA MWANDISHI WETU MKE wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mariam Mwinyi, ameitaka jamii kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe hasa kwa watoto na mama wajawazito ili kuwa na afya bora. 1. MKE wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na Msarifu wa taasisi ya zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, akihutubia wananchi wakati akifunga rasmi kampeni ya siku ya afya na lishe ya kijiji katika shehia ya Donge Vijibweni, mkoa wa Kaskazini Unguja. Mama Mariam alieleza hayo jana alipokua akifunga wiki ya afya na lishe ngazi ya shehia huko Donge Vijibweni wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, iliyoambatana na maonesho ya vyakula vya lishe na utoaji wa huduma na elimu ya afya. Alieleza kuwa ili kuwa na jamii bora kuna umuhimu wa kuimarishwa kwa elimu ya lishe katika ngazi ya jamii ili kuondoa changamoto ya utapia...