Mama Mariam aelekeza namna ya ulaji vyakula vya lishe

NA MWANDISHI WETU 

MKE wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF),  Mariam Mwinyi, ameitaka jamii kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe hasa kwa watoto na mama wajawazito ili kuwa na afya bora.

1.       MKE wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na Msarifu wa taasisi ya zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, akihutubia wananchi wakati akifunga rasmi kampeni ya siku ya afya na lishe ya kijiji katika shehia ya Donge Vijibweni, mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mama Mariam alieleza hayo jana alipokua akifunga wiki ya afya na lishe ngazi ya shehia huko Donge Vijibweni wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, iliyoambatana na maonesho ya vyakula vya lishe na utoaji wa huduma na elimu ya afya.

Alieleza kuwa ili kuwa na jamii bora kuna umuhimu wa kuimarishwa kwa elimu ya lishe katika ngazi ya jamii ili kuondoa changamoto ya utapia mlo na udumavu kwa watoto.

Alieleza kuwa tafiti zinaonesha kuwa Kufuatia changamoto ya vifo vya wajawazito ambavyo kwa mwaka 2022 vilifikia vifo 99 kwa vizazi hai 100,000, taasisi hiyo iliamua kubuni mradi huo ili kuzikabili changamoto zinazochangia vifo hivyo.

“Tatizo la upungufu wa damu pamoja na lishe duni na udumavu wa watoto wa chini ya miaka mitano ambao ni mtoto mmoja kati ya watoto watano. Mimi pamoja na taasisi yangu ya Zanzibar Maisha Bora Foundation kwa kushirikiana na wafadhili wetu Wizara ya Afya na Benjamin Mkapa Foundation tumekuja na mradi huu wa lishe ili kutokomeza changamoto hizi”, alieleza mama Mariam.

 MKE wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na Msarifu wa taasisi ya zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Fatma Fungo, wakifurahia jambo wakati wa ufungaji wa siku ya afya na lishe ya kijiji. 

Alifafanua kuwa mradi huu unalenga kuimarisha lishe kwa watoto umri chini ya miaka mitano, mama wajawazito na ustawi wa jamii kiuchumi kwa kuhakikisha kuna utambuzi na matumizi ya mbinu endelevu ya lishe kwa watoto na mama wajawazito.

Aliongeza kuwa; “Kwa kuanzia mradi huu unatekelezwa katika mikoa miwili ambayo ni Kaskazini Unguja and Kaskazini Pemba, katika wilaya mbili za Kaskazini ‘B’ and Wete”.

Akizungumzia matokeo ya utekelezaji wa mradi huo, mama Mariam alieleza kuwa siku za lishe na afya ya kijiji zilizofanyika mwezi Disemba, mwaka jana na Januari, mwaka huu, watoto 347 waligundulika kuwa na utapiamlo wa kati na wa wastani.

Aidha alieleza kuwa watoto 51 waligundulika kuwa na udumavu na 70 walikutwa na upungufu wa damu jambo linaloonesha uwepo wa tatizo bado na haja ya wadau kuongeza nguvu ya kukabiliana nalo.

“Niendelee kuhamasisha kutambua matumizi ya mbinu mbali mbali endelevu za kuimarisha lishe kwa watoto na mama wajawazito ambazo zitachangia katika hatua za awali za ukuaji wa mtoto tangu mimba inapotunga, wakati wa ujauzito na baada ya kuzaliwa hadi kufikia umri wa miaka miwili”, alisema Mwenyekiti huyo wa ZMBF.


1.       MKE wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na Msarifu wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, katika picha ya pamoja na wahudumu wa afya ya jamii alipotembelea banda lao kabla ya kufunga rasmi siku ya afya na lishe ya kijiji.

Alifafanua kuwa kipindi cha siku 1,000 za mwanzo wa maisha ya mtoto ni muhimu katika ukuaji wa ubongo wa mtoto na kuwasihi wananchi wa Shehia zilizofikiwa na mradi huo kutumia mbinu walizofundishwa kuongeza kiwango cha lishe kwa familia zao.

Alizitaja mbinu hizo kuwa ni pamoja na kuanzisha bustani viroba kwa ajili ya kilimo cha mboga mboga ili kusaidia familia kupata mboga kuimarisha hali zao za kiuchumi na lishe bora.

Pamoja na hayo aliwashukuru wadau mali mbali wanaoendelea kushirikiana na taasisi hiyo kutekeleza afua mbali mbali zinazolenga kuimarisha afya na ustawi wa jamii.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh ‘Diaspora’ aliwataka wanaume kuzipatia familia zao vyakula vyenye lishe vinavyopatikana katika mazingira yao ili kuwa na jamii iliyo bora.

Alieleza kuwa iwapo kina baba watakuwa mstari wa mbele na kuhudumia familia zao kwa kuzingatia muongozo wa lishe uliotolewa na wizara hiyo, kuna uhakika wa kuimarika kwa afya za wananchi na kupungua kwa vifo vinavyotokana na lishe duni.

MKE wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, akiwasili katika uwanja wa donge vijibweni kuhudhuria hafla ya siku ya afya na lishe ya kijiji. 

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa miezi sita, Ofisa Mtendaji Mkuu wa ZMBF, Fatuma Fungo, alieleza kuwa mradi huo ilitekelezwa kwa pamoja kati ya ZMBF, Benjamin mkapa foundation na wizara ya afya kwa ufadhili wa shiurika la chakula ulimwenguni (WFP).

Alieleza kuwa wilaya mbili za Kaskazini ‘B’ na Wete zimeshiriki katika mradi huo ambapo katika ufuatiliaji na tamthini waliyofanya, jumla ya vituo vya afya 30 kati ya 32 sawa na asilimia 94 ya vituo vilivyomo kwenye wilaya hizo ilifikiwa.

Alieleza pia shehia 67 kaya 4,496 kati ya 4320 na familia 623 zilianzisha bustani kiroba nyumbani mwao kwa msaada watoa huduma za afya ya jamii na kuongezeka kwa mahudhurio ya wajawazito kwa asilimia 40 kutoka kwa wajawazito 60 mwezi Oktoba hadi wajawazito 84 Novemba 2023.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango