Dk. Mwinyi ahimiza matumizi nishati salama
Apongeza ushirikiano wa Oryx, Vigor uwekezaji mradi wa gesi NA MWANDISHI MWAALUM RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amezipongeza kampuni za Oryx Gas Tanzania Ltd na kampuni ya TP Limited ambayo ni kampuni tanzu ya Vigor Turky’s Group of Companies kwa kujenga bohari ya kwanza ya kuhifadhi nishati ya gesi ili kuongeza usambazaji wa gesi ya iliyokandamizwa visiwani humo. Akihutubia wananchi wa Zanzibar baada ya kuzindua bohari hiyo huko Mangapwani, mkoa wa Kaskazini Unguja Dk. Mwinyi alieleza hatua hiyo itachochea utekelezaji wa mkakati wa taifa wa ulinzi wa mazingira na ongezeko la matumizi ya nishati safi kwa shughuli mbali mbali. Alieleza uwepo wa bohari ya kuhifadhi gesi pamoja na miundombinu mingine ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa bandari jumuishi inayojengwa katika ukanda huo ambayo itahusika bandari ya meli za mafuta, gesi pamoja na shughuli nyingine. Alisema kuanzishwa kwa bohari ya kuhifadhi ya gesi Zanzibar kutaongeza ch...